Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 095 (The world hates Christ)
This page in: -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish? -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 3 - Nuru yang’aa ndani ya shirika la Mitume (Yohana 11:55 - 17:26)
D - Kuagana njiani kwenda Gethsemane (Yohana 15:1 - 16:33)

3. Ulimwengu humchukia Kristo na wanafunzi wake (Yohana 15:18 - 16:3)


YOHANA 16:1-3
„Maneno haya nimewaambia, msije mkachukizwa. Watawatenga na masinagogi; naam, sasa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi.“

Yesu aliwajulisha wanafunzi wake, kwamba watachukiwa kwa sababu tatu hizo:

Kwa sababu wamezaliwa na Mungu wala si na ulimwengu.

Kwa sababu watu hawamtambui Kristo, Mwana wa Mungu wala sura ya Mungu.

Kwa sababu hao washupavu wanaojidhania kuwa na dini hawamjui Mungu wa kweli, na ibada yao ni kwa ajili ya mungu asiyejulikana na ya giza.

Bila shaka lolote, chuki ya kuzimu inaendelea. Yule amgeukiaye Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ataweza kuuawa na washupavu kama kafiri kote atakapopatikana, wakidhani kwamba wanamtumikia Mungu. Lakini kwa kweli, wanamtumikia ibilisi. Hawajui kwamba Mungu wa kweli ndiye Baba Mtakatifu; Hawakuweza kuelewa nguvu ya damu ya Yesu. Wao hawana nguvu ya Roho Mtakatifu. Hivyo roho fulani wa kigeni inawaongoza kuharibu wale wanaoshuhudia Utatu Utakatifu hata kwa mateso, kuuawa au majaribu mbalimbali. Ndivyo walivyofanya Wayahudi kwake Yesu na kabla yake kwa manabii, na ndivyo itakavyokuwa hadi Kristo atakaporudi.

Usidhani kwamba siku za mbeleni zitakuwa bora zaidi, kwa sababu wanadamu wanaendelea kuongeza elimu na utambuzi na mafunuo. Hapana, roho hizo mbili zinazoshindana zitakuwepo duniani hadi mwisho: Huyu Roho wa kutoka juu, na mwingine toka chini. Wala hakuna daraja la kuunganisha mbingu na kuzimu. Ama unaingia kabisa ndani ya ushirikiano na Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, au utaanguka ndani ya kifungo cha kuzimu na gereza la makosa yako. Ukimfuata Yesu, utakuwa mtu wa kupendeza, ukimheshimu Baba kwa njia ya ushuhuda wako. Lakini ukiacha kuwa mtoto wake, utaendelea kufungamana na roho na mawazo mengine, hata kuingia polepole katika hali ya uadui na Mungu.

Yesu akukumbusha habari ya gharama ya kukufanya kuwa mtoto wa Mungu, ikiwa utadumu kwa kweli ndani yake. Maisha yako ya mbeleni itakuwa ngumu na yenye maumivu, kwa vile kuzimu italipuka dhidi ya Kristo na wafuasi wake. Dunia huchukia kila mfuasi mwaminifu wa Yesu; hivyo utakuwa na Mungu akiwa Baba yako na katika njia hiyo utakuwa mgeni ndani ya dunia hiyo; au utabaki kuwa adui wa Mungu, na dunia itakukaribisha kuwa mmojawao. Basi, chagua katika uzima au mauti ya milele.

SALA: Bwana Yesu, asante sana kwa ajili ya kuchagua kifo kwa ajili yetu; uliendelea kuwa mwaminifu kwa Baba yako. Utuvute mbali na roho ya dunia hii, na tuweze kushika mizizi ndani ya upendo wako, tuendelee kudumu kuwa watoto wa Mungu. Upendo wako ndiyo nguvu yetu na uongozi wetu. Amina.

SWALI:

  1. Kwa nini dunia inawachukia wale wanaoamini ndani ya Kristo?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 13, 2015, at 11:50 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)