Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 043 (Jesus offers people the choice)
This page in: -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
B - Yesu ni chakula cha (mkate wa) uzima (Yohana 6:1-71)

4. Yesu anawapa watu chaguo: “Kubali au kataa!” (Yohana 6:22-59)


YOHANA 6:34-35
34 “Basi wakamwambia, Bwana, sikuzote utupe chakula hiki. 35 Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima, yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.”

Yesu alitamanisha ndani ya wasikilizaji wake njaa kwa mkate wa Mungu, na akawaweka huru na vifungu vya mawazo ya matendo fulani ya pekee. Aliumba ndani yao fikira ya wokovu, akiwatayarisha kupokea ile zawadi ya Mungu; aliwaelezea haja ya imani ndani ya nafsi yake.

Kwa tamko hilo wengi wao wakakubali kwa shauku ya juu juu wakisema, “Wewe mtoaji wa mkate wa kweli, utupatie zawadi hii ya pekee daima, ili kutusalimisha na taabu zetu. Tunakutegemea wewe, tujalie na uzima wa milele, tushirikishe na nguvu zako!” Hata hapo bado waliendelea kufikiria mkate wa asili, lakini hata hivyo wakaelewa kwamba, zawadi ya Mungu ni ya pekee.

Yesu hawezi kumdharau yeyote atakaye kumkaribia. Aliweka wazi kwamba, yeye kwanza ni mkate wa Mungu kwa ulimwengu wote, wala siye mtoaji wa chakula tu. Yeye nafsini mwake aliwatolea yaliyotakiwa kwa uzima wa milele. Alidokeza, “Mbali na mimi hamtaona uzima wa milele. Mimi ndimi zawadi ya Mungu kwenu; bila ya mimi mtaendelea katika hali ya kufa.”

“Kama vile mkate unavyomezwa na kupatia nguvu ya kuishi, vivyo hivyo mimi natamani kuja ndani yenu, ili nihuishe fikira na dhamiri zenu, hata mweze kuishi kiroho. Bila ya mimi hamtaweza kufanya kitu. Mnanihitaji kila siku. Mimi najitolea kwenu bure kabisa. Hamtahitaji kutoa chochote. Mniruhusu tu kuingia mioyoni mwenu.” - Ndugu yangu, wewe unamhitaji Kristo. Kusoma neno lake au kushika mawazo yake tu haikutoshi. Unamhitaji yeye binafsi. Yeye ndiye kwako ni ya lazima kama vile chakula na maji kwa kila siku. Ni juu yako kumpokea, au utapotea.

Pengine utauliza, jinsi gani yeye ataingia ndani ya kiini cha utu wangu? Yeye anajibu: Ruhusu moyo wako kunitamani, tena uje karibu nami na kunipokea kwa shukrani,uniamini tu. Kuingia kwa Yesu mioyoni mwetu inakamilishwa kwa imani. Mshukuru Yesu, kwa sababu ndiye zawadi ya Mungu kwako, akijitoa kwako bure. Umtukuze kwa furaha, kwa sababu yeye ni tayari kukaa ndani yako daima. Atakujia ukimhitaji na kumwomba kwa kweli. Umsihi adumu ndani yako daima.

Ndipo Yesu atakuhakikishia kwamba, “Kwa sababu umenipokea, nitaendelea kuwa ndani yako, nami nitaridhisha hamu yako ya uhai wa kweli. Usiendelee kujadili dini za ulimwengu na filosofia zake kama kutafuta iliyo ya kweli. Usielekee kwa kila dimbwi ili uinywee. Bali mimi nitakujalia nguvu, shabaha za kweli na amani.”

YOHANA 6:36-40
36 “Lakini naliwaambia ya kwamba mmeniona wala hamwamini. 37 Wote wanipao Baba watakuja kwangu; wala yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe. 38 Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka. 39 Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika wote alionipa nisimpoteze hata mmoja, bali nimfufue siku ya mwisho. 40 Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.”

Yesu alikwisha kuwapatia Wagalilaya mkate wa neema bure. Walimwona kama mwenye mamlaka ya kung’aa. Lakini kumtambua hivyo haikufikia thibitisho, wala kuwaendeleza kukiri imani. Bado walikuwa wa kutanga-tanga bila uhakika. Walikuwa hodari kumhusu Yesu kama Bwana wa mikate, lakini wenye kusita kwa kutegemea nafsi yake. Kwa jumla hawakumkubali kwa shukrani.

Yesu aliwasisitizia, jinsi alivyofanya kule Yerusalemu, sababu ya kutengana naye. Kwa nini watu wengi hawamtegemei Yesu? Kiajabu, Yesu hawaambii moja kwa moja: “Ni kosa lenu”, bali anawaelekeza kwa Baba, na kuwaonyesha jinsi imani inavyojengeka hatua kwa hatua kama shughuli tukufu.

Yesu hana nia ya kumshawishi hata mmoja kwa hila au kwa hoja ya maneno tu. Mungu mwenyewe anamtolea watenda dhambi, akijua ukweli juu yao, pia na kiasi cha utayari yao kwa kuungama na kugeuka. Ni wale tu wanaokubali kuvutwa na Roho ndio watakaovutwa kwake Yesu. Kristo hachukizwi na waongo, wazinzi au wezi, mradi waje kwake tu kwa hali ya kutubu. Hajamkataa yeyote aliyehitaji kumkaribia, hata adui zake. Alikuwa na huruma kwa ajili yao na kuwatolea msamaha wa wokovu.

Kristo hakuishi duniani kwa ajili yake binafsi, wala hakupanga maisha yake kwa mambo aliyoweza kuyatamani. Alishuka ili atimize mapenzi ya Baba yake na kuambatana kikamilifu na makusudi ya upendo wake: Kuwaokoa wote wale walio tayari kuokolewa, ndipo kuwatunza wale waumini wenye hamu ya kudumu ndani yake. Ukarimu wa rehema zake na uwezo wa kuokoa ni kubwa mno. Si kifo wala shetani, wala hatia zozote zitaweza kuwashika wale walio ndani ya mikono yake. Kwa rehema zake atawafufua wafuasi wake siku ya hukumu na kuwafikisha kwenye uzima wa milele.

Wewe je, unafahamu mapenzi ya Mungu? Anakutaka umtazame Mwana wake, umfahamu na kumtegemea. Yeye ametokana na Roho wa Mungu, akijaa neema na kweli. Ndipo anakutaka uunganike na huyu Mwokozi, pamoja na waumini wote katika agano la milele, isiyoweza kuachanishwa tena; kwa njia hiyo shabaha ya Mungu kwako itakamilika. Mara moja mwumini atapokea uhai wa milele kupitia kwa Roho Mtakatifu akiingia mwili wako dhaifu. Imani yako ndani ya Yesu inakuhakikishia uzima huu wa milele ndani yako, uzima unaojionyesha maishani mwako katika upendo, furaha, amani na unyenyekevu. Uzima huu wa Mungu ndani yako haina mwisho. Hatua ya mwisho katika mapenzi ya Mungu ni kwamba atakufufua kutoka kwa wafu. Hii ndiyo tumaini kuu la kila mwumini. Ndipo kilele cha maisha kitakachotolewa kwako na Mwana kitaonekana - utukufu wa Mwana wa Mungu na mwangaza wa pendo lake.

SALA: Tunakuabudu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Asante, huko mbali nasi. Lakini ulitujia wakati umati wa wengi sana walikukataa. Wewe ulitumulikia hata tukakuona wazi na kukupokea kama mkate wa kweli. Asante sana kwa kutokutukataa. Wewe umeridhisha mioyo yetu yenye njaa, nawe utatufufua kwa kipeo cha furaha ya milele na shukrani za heri daima.

SWALI:

  1. Neno la „Mkate wa uzima“ lina maana gani?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on October 07, 2013, at 11:56 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)