Previous Lesson -- Next Lesson
4. Yesu anawapa watu chaguo: “Kubali au kataa!” (Yohana 6:22-59)
YOHANA 6:41-42
41 „Basi Wayahudi wakamnung’unikia, kwa sababu alisema, Mimi ni chakula kilichoshuka kutoka mbinguni. 42 Wakasema, Je! Huyu siye Yesu, mwana wa Yusufu, ambaye twamjua babaye na mamaye? Sasa anasemaje huyu, Nimeshuka kutoka mbinguni?“
Yohana mwinjilisti aliwaita Wagalilaya „Wayahudi“, ingawa hawakuwa watu wa kundi hili la watu. Lakini kwa vile walivyokataa Roho wa Kristo, hawakuwa bora kuliko hao Wayahudi na wakaaji wote wa kusini (Uyahudi karibu na Yerusalemu).
Wale waandishi wakatokeza sababu nyingine ya kwao, ili wamkatae Yesu, kwa sababu mawazo yao ya kisheria, wakiamini uwezekano wa kujiboresha wenyewe, ikagongana na upendo wa Yesu. Lakini wale wa Galilaya wakajikwaa na jamii wa Yesu, maana walijua familia yake, kwa sababu „baba yake“ (seremala Yusufu) aliishi nao, mtu wa kawaida, bila kipawa cha unabii au uwezo mwingine wa kipekee. Na mamaye Mariamu hakuwa na lolote la kumtofautisha na wanawake wengine, isipokuwa baadaye akawa mjane, ambalo jambo hilo lilidhaniwa kuwa dalili la ghadhabu ya kimungu. Kwa sababu hizo Wagalilaya hawakuamini kwamba Yesu ndiye mkate kutoka mbinguni.
YOHANA 6:43-46
43 „Basi Yesu akajibu, akawaambia, Msinung’unike ninyi kwa ninyi. 44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho. 45 Imeandikwa katika manabii, Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Basi kila aliyesikia na kujifunza kwa Baba huja kwangu. 46 Si kwamba mtu amemwona Baba, ila yeye atokaye kwa Mungu; huyu ndiye aliyemwona Baba.“
Yesu hakujaribu kueleza mwujiza wa kuzaliwa kwake kwa wale waliomkataa, maana wasingeamini hata hivyo. Wala sisi hatuwezi kuelewa peke yetu uungu wa mwanadamu Yesu, ni kwa kumulikiwa na Roho Mtakatifu tu. Yeyote amjiaye kwa imani atamwona na kutambua ukuu wa ukweli wake.
Yesu aliwakatalia mikutano wasinung’unike mafunuo hayo matukufu. Roho zetu kaidi za kibinadamu hazisikii kitu kuhusu ufalme wa Mungu. Bali yule anayejihimiza kwa moyo wazi ataona haja yake, na atatambua upendo wa Mungu.
Mungu kwa upendo wake huwavuta watu kwake Yesu Mwokozi, akitamani wamulikiwe, na atawafundisha mmoja mmoja, jinsi tusomavyo kwa Yeremia 31:3. Katika Agano Jipya twaelezwa kwamba, si mapenzi ya mtu wala akili yake inayotokeza imani; ila ni Roho Mtakatifu anayetumulikia na kuumba ndani yetu maisha tukufu, hata tutambue kwamba Mungu mwenye enzi yote kweli ni Mungu na Baba. Anawafundisha watoto wake kuendeleza uhusiano wa moja kwa moja naye. Anaumba imani mioyoni mwetu kwa njia ya mvuto wa Roho. - Je, umewahi kusikia mvuto huo katika dhamiri yako? Uko wazi kwa ajili ya mvuto wa upendo wa Mungu?
Roho wa Baba hutuongoza kwake Yesu na kutusukuma tumkaribie yeye. Yeye anaanzisha hamu yetu kwa ajili yake, hadi tunainuka na kwenda kukutana na Yesu na kumpenda. Yeye hutukubali jinsi tulivyo, wala hatatutupa nje. Atapanda ndani yetu uhai wa milele, ili tuweze kushiriki nguvu ya ufufuo, na mwishowe kuingia katika utukufu wa Babaye.
Hata hivyo inabakia utofauti kati ya Yesu na mwumini aliyezaliwa mara yapili. Hakuna mtu aliyemwona Mungu, ila Mwana tu. Alikuwa pamoja na Baba tangu mwanzo akimtazama. Baba na Mwana hawakuweza kutenganishwa. Yesu alishiriki katika amani ya mbinguni na katika hali zote tukufu za Baba.
YOHANA 6:47-50
47 „Amin, amin, nawaambia, yeye aaminiye yuna uzima wa milele. 48 Mimi ndimi chakula cha uzima. 49 Baba zenu waliila mana jangwani; 50 hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu akile wala asife.“
Baada ya kutangaza umoja wake na Baba na kazi ya Roho ndani ya wasikilizaji wake, Yesu tena akatambulisha ukweli wa asili yake kwao, ili waweze kumtegemea. Alieleza kiini cha kikristo kwa kifupi: Yeye aaminiye ndani ya Yesu ataishi milele. Ukweli huu unayo uhakika ambao hata kifo hawezi kufuta.
Yesu ni kama mkate kutoka kwa Mungu kwa ajili ya dunia. Kama vile mkate wakati ule haukwisha hapo ulipopitia mikono yake wakati wa mwujiza wa kuwalisha elfu tano, ndivyo Yesu anavyo tosheleza haja za ulimwengu wakati wowote, maana ukamilifu wa Mungu hukaa ndani yake. Kutoka kwake utapokea tumaini, furaha na baraka. Katika neno lake anatolea kwa ulimwengu uhai wa Mungu, ila ulimwengu ulimkataa.
Chakula cha mana kilichoshuka jangwani kilikuwa ni zawadi toka kwa Mungu; kuwatunza hivyo kuliendelea kwa muda tu. Wote waliokula, hapo baadaye wakafa. - Hayo nayo tunaona katika huduma za ufadhili, maendeleo ya ufundi na mafumbuzi ya kisayansi, kwamba yasaidia kwa muda na kwa sehemu tu. Hakuna dawa ya kifo na mambo ya kutazamiwa, wala ushindi juu ya dhambi. Bali yeyote amwaminiye Kristo, hatakufa. Hii ndiyo kusudi la Kristo, kuja na kutulia ndani yetu. Anatamani kuishi ndani yako wewe binafsi, ili roho yoyote nyingine isiweze kutawala juu yako. Yeye aweza kuondoa tamaa zote mbaya na kutuliza hofu zako zote pamoja na kuimarisha udhaifu wako. Yeye ndiye mkate wa Mungu kipekee kwa ajili yako. Ule, ukaishi, wala usipotee kama watenda dhambi wengine.
SWALI:
- Jinsi gani Yesu aliitikia kwa manung’uniko ya wasikilizaji wake?