Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 014 (Testimonies of the Baptist to Christ)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
B - Kristo anaongoza wanafunzi wake kutoka hali ya kutubu kwenye furaha ya karamu ya arusi (Yohana 1:19 - 2:12)

2. Ushuhuda zingine za Mbatizaji za kuvutia sana, za kumhusu Kristo (Yohana 1:29-34)


YOHANA 1:29-30
29 “Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu. 30 Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.”

Wajumbe waliporudi Yerusalemu, waliendeleza dharau lao kwa Mbatizaji. Hadi hapo Mbatizaji aliamini kwamba Kristo anakuja kwa kuwarejesha na kuwasafisha watu wake, kama kupepeta ngano, Kristo awe kama mwenye hasira, shoka mkononi ili akate kila mti mwenye maradhi. Hivyo ujumbe wa kuja kwa Kristo ungetangulia siku ya ghadhabu. Wakati aliposema, “Masihi yuko katikati yetu”, wanafunzi walichokozwa kuyaondolea makosa yao, maana walifikiria hukumu itadondoka mara bila kuonywa.

Kumbe, Kristo mwenye umri wa miaka thelathini tu alimjia Mbatizaji na kwa utulivu alimwomba ambatize. Unyenyekevu huu ulimtingisa Mbatizaji ajizuie na kumwomba yeye Yesu ambatize na kumsamehe dhambi zake. Lakini Yesu alisisitiza akimtaka ambatize, ili haki yote itimie.

Hapo ndipo Yohana alitambua kwamba Mtakatifu hakuja kuangamiza wanadamu, lakini kubeba dhambi zao. Alikubali ubatizo kama mjumbe wa huruma. Kuja kwake Bwana haikuwa njia ya kutimiza hasira, lakini kwa kuleta upatanisho na kusamehe dhambi. Alipojitambua akisimama ukingoni mwa Agano la Kale, Mbatizaji alipata kuelewa kina cha mambo mapya ndani ya upendo wa Mungu. Badiliko hilo kuu lilipindua kabisa msimamo wake.

Kesho yake Yesu alipoonekana tena, Yohana alielekeza kwake Yesu akisema, “Angalieni na mpate kujua, fungueni macho yenu, huyu ndiye!” Hapo haikutokea ngurumo wala jeshi la malaika, bali Neno la Mungu lilimwagwa, kila mtu apate kutambua: Huyu kijana ndiye aliyengojewa tangu muda mrefu, ndiye Bwana mwenyewe, aliye tumaini la ulimwengu.

Tangu hapoYohana hakutaka watu wamzunguke yeye na wafikirie juu ya tazamio la Masihi, mwenye nguvu ya kijeshi. Huyu alikuwa Mwana Kondoo wa Mungu, wala si “Simba wa Juda”, aliyetazamiwa mwenye enzi na ushindi, bali mnyenyekevu na mvumilivu.

Akiwa amejazwa na nguvu za Roho Mtakatifu Yohana alitangaza, “Huyu Kristo ndiye mwenye kubeba dhambi za ulimwengu. Yeye ndiye dhabihu la mwisho au Mwana Kondoo wa Mungu, mfano wa desturi zetu za zamani za sadaka. Yeye anastahili kutolewa badala ya wanadamu kuhukumiwa. Upendo wake ni mwenye nguvu na wa kufaa. Yeye ndiye Mtakatifu, hata anapotwishwa dhambi za kila mwanadamu.” Yeye aliyekuwa bila dhambi akawa dhambi kwa ajili yetu. Hivyo akafanywa kuwa haki yetu mbele ya Mungu.

Ushuhuda huu wa Mbatizaji ndio kilele cha injili na msingi wa Biblia. Alitambua kwamba utukufu wa Kristo ni kuteswa kwake kwa ajili yetu. Wokovu wa Kristo ni wa ulimwengu mzima na kumkumba kila mtu, wa kabila na taifa lolote, awe mwenye rangi yoyote ile. Inachukua wakuu na maskini, watajiri na wadhaifu, wazee na vijana. Inadumu wakati wa zamani, sasa na wakati ujao. Kifo chake kinatosha kwa makosa yote. Fidio lake kwa ajili yetu ni kamili kabisa.

Kuanzia siku ya kwanza ya kuja kwake kama Mwana Kondoo aliumia kwa sababu ya maovu, lakini hakuwatupa waovu au kuwadharau wenye kiburi, bali aliwapenda. Alijua uzito wa kifungu cha dhambi zao, akajiweka tayari kuwafia wao na sisi.

Kwa waliomsikiliza Mbatizaji aliwatangazia kwamba, Mwana Kondoo wa Mungu amewaondolea ghadhabu ya Mungu. Yeye ndiye mwenye kuhukumiwa, akifa kama Mwana Kondoo kwa niaba yao. Wale waliokuwapo pale walishangaa ni vipi mtu mmoja atatwishwa malipo ya dhambi za watu wote. Maneno ya Yohana yalifungua macho yao, lakini neno la msalaba haijawa wazi kwao. Tukio lingine la ajabu lije baadaye kutimiza mpango wa Mungu ndani ya Kristo.

Mara nyingine Mbatizaji alirudia kwamba, Yesu atafanya wokovu kuwa kamili, kwa sababu alikuwa Bwana wa milele. “Yeye ni mkuu kuliko mimi na alikuwepo kabla yangu”.

Utukufu wa Kristo ulikuwa kuu, lakini upendo wake msalabani udhihirisha kiini cha utukufu wake. Mwinjilisti akakiri, “Tuliona utukufu wake, alitundikwa msalabani akiumia mno, na hivyo kudhihirisha kipimo cha upendo uliotuweka huru”.

SALA: Ewe Mwana kondoo wa Mungu, mtakatifu, uliyebeba dhambi za dunia, utuonee huruma. Ewe Mwana wa Mungu wa milele, ulioingia mwilini mwetu, utusamehe dhambi zetu. Ewe Mnazareti mnyenyekevu, ambaye hukuona aibu kwa makosa yetu, tunainua jina lako, kwa sababu ulitupenda na kukamilisha upendo huo msalabani. Tunakupenda na kukushukuru, maana hukuja kama hakimu bali kama Mwana Kondoo. Tunakuamini, kwa vile uliondoa dhambi za watu wote nchini kwetu. Tujalie hekima ili tukawambie wengine nao kwamba, uliwaokoa na wao.

SWALI:

  1. Ni nini maana ya “Mwana Kondoo wa Mungu”?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 24, 2013, at 07:53 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)