Previous Lesson -- Next Lesson
e) Kuabudu kwake Mtume Paulo (Warumi 11:33-36)
WARUMI 11:33-36
"33 Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani! 34 Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? 35 Au ni nani aliyekuwa mshauri wake? Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza , naye atalipwa tena? 36 Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina.
Paulo alikuwa na hofu kwa ajili ya hali ya kiroho ya Wayahudi, lakini wakati ule ule alijaa na shukrani na sifa kwa ajili ya waumini wa kwanza wa Wayahudi kule Yerusalemu. Alimhimidi Yeye Mtakatifu kwa ajili ya kuongezeka kwa namba ya waumini kutokana na watu wengine, na hapo kujisikia kwake hofu kulitulizwa kwa sababu ya upendo kuu wa Mungu. Alikiri rehema zake, wala hakukana maadhibu yake. Paulo alitambua sana upendo wa Mwenyezi, aliamini ndani ya njia zake ambazo mara nyingine hazikueleweka, na mwishoni alishuhudia kwa kukiri: „Mungu ni ng‘ambo ya ufahamu wetu. Tunamtegemea, nasi tunaweka mawazo yetu chini ya mapenzi na mafunuo yake“. (Isaya 40:13 na 45:15 na 55.8-9; pia Warumi 11:33).
Abarikiwe yeye anayemwabudu Bwana wake kwa uaminifu, akimtukuza, na akumshukuru, kwa sababu anamtambua Mtakatifu ndani ya upendo wake. Roho wa kweli anamwongoza kwenye kina cha tukufu, na kwa uhakika wa utajiri wa roho yake katika vipawa vyake kwa utendaji wake wa kila siku. Katika sehemu ya pili ya waraka wake Paulo anafikia mwisho na madhumuni wa shughuli yake. Anakiri wazi ile hali ya watu wa Yakobo kuwa ngumu, naye anatambua ya kwamba, sababu nyuma yake ilikuwa ni kutokuamini kwao na namna yao ya kupinga mapenzi ya Mungu; Paulo hakatai ukweli huo.
Pamoja na hayo anawatia moyo hao waumini wa kutokana na Wayahudi, pia na mabwana wengine wa kule Rumi kwamba, Mungu atawakubali tena na kurudia kwa ajili ya neema yake isiyo na mwisho. Hata hivyo, Bwana aliwachochea Wayahudi kwa njia ya hao waumini wapya watokao kwa Mataifa, akiwaonyesha upendo wao, uvumilivu, usafi, pia na huduma yao katika eneo la Anatolia, huku akiwaongoza kwenye huduma ya utendaji wa kila siku kwa kushirikiana na kwa uaminifu.
Lakini mambo yalivyoendelea kihistoria yalienda kinyume cha matazamio ya Paulo.Yeye mwenyewe akapata kuwa madhabuha ya kwanza ya ukorofi wa Wayahudi. Alikatwa kichwa kule Rumi kwa matokeo ya mashitaka yao ya uongo. Paulo alitambua hali hiyo ya kuwa wagumu dhidi yake mwenyewe na ya injili, naye akarudia huo ukweli wa kiroho kwa Wayahudi, jinsi nabii Isaya alivyoeleza.Aliandika: „Kusikia, mtasikia wala hamtafahamu; Na kuona mtaona wala hamtatambua; Kwa maana mioyo ya watu hawa imepumbaa, Na masikio yao ni mazito ya kusikia, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kufahamu kwa mioyo yao, na kubadili nia zao, nikawaponya. Basi ijulikane kwenu ya kwamba wokovu huu wa Mungu umepelekwa kwa Mataifa, nao watasikia!“ Alipokwisha kusema hayo, Wayahudi wakaenda zao, wakiulizana mengi wao kwa wao. (Matendo ya mitume 28: 26-29).
Paulo aliendelea kubaki katika magereza ya Kirumi kwa miaka kadhaa kwa sababu ya sentenso ya baraza la Kiyahudi dhidi yake (Matendo ya Mitume 23:1 hadi 28:16). Kwa matokeo ya ukaidi na ukorofi wao ilimpasa asafiri hadi Rumi ambapo Kaisari mwenyewe alimhukumu (Matendo ya Mitume 27:1-28:16). Hata hivyo kufungwa kwake kulikuwa na unafuu, maana Warumi walimruhusu kuhubiri injili kwa wote wale waliopenda kumsikiliza.
Hesabu ndogo ya Wayahudi kule Rumi waliamini, wakati wengi wa wazee wao na ma-rabbi hawakukubali mafundisho yake, bali waliangalia Ukristo kuwa ni dhehebu la Kiyahudi (Matendo ya Mitume 28:22). Wao walikuwa na mvuto mkubwa kwa upande wa mahakimu, hata baada ya yeye kukatwa kichwa.
Ule Ukorofi wa Wayahudi dhidi ya mtume wa mataifa ulifikia mwisho wake, lakini nyaraka zake Paulo ziliendelea kuenea bila zuio lolote. Hata na siku hizi maandiko yake Paulo zinavuta hesabu kubwa isioweza kuhesabika za Wayahudi na za Mataifa wapate kuamini ndani ya Kristo. Ni dhahiri kabisa kwamba Paulo, anayeishi ndani ya Kristo, basi anatembea kwa ushindi wa Kristo hadi mwisho wa ulimwengu.
SALA: Ee Baba wa mbinguni, tunakuabudu pamoja na Mtume Paulo. Tunakutukuza kwa ajili ya upendo wako pia na kwa uchungu wako, twakutukuza kwa ajili ya rehema na maamuzi yako; na tunafurahia ndani ya njia zako za hekima na neema ya uaminifu. Kipekee kabisa tunakushukuru kwa sababu ya kutuletea Kristo, ili tweze kuwa watoto wako wapendwa. Amina.
SWALI:
- Kwa ukamilifu wa neema na hekima ya Mungu inamaanishwa nini?
- Jinsi gani Mungu anaendelea kuwa mwenye haki, ikiwa anafanya migumu watu wake wateule, ndipo mwishoni anaikubali baki lake takatifu, na akiwakumbuka hao kutokana na watoto wote wa Yakobo?
QUIZ - 3
Mpendwa msomaji,
Baada ya kusoma maelezo hayo kuhusu barua ya Paulo kwa Warumi katika mfululizo huo, bila shaka sasa utaweza kujibu maswali yafuatayo. Ukiyajibu kwa usawa kwa 90% ya maswali, tutakutumia mfululizo ufuatao ya masomo hayo kwa ajili ya maongozo yako mema. Unapotuma majibu kwa Posta, usisahau kuweka jina lako kamili na anwani yako waziwazi kwenye karatasi ya majibu yako.
- Huzuni kuu ya Paulo ilikuwa na sababu gan?
- Paulo alikuwa tayari kutoa sadaka gani kwa ajili ya wokovu wa watu wake?
- Mapendeleo mangapi Paulo alitaja kuhusu watu wa Agano la Kale? Ipi katika hizo unaona ni muhimu zaidi kwako?
- Kwa nini neema ya Mungu haikufaulu kuwaokoa wengi wao wa wateule wake, nao wakaanguka katika hukumu moja hadi nyingine?
- Maana ya kuchaguliwa kwake Isaka ni nini na ya uzazi wake, pia na kuchaguliwa kwake Yakobo na wana wake?
- Je, siri ya uchaguo wa Mungu ni nini?
- Kwa nini hakuna mtu anayestahili kuchaguliwa na Mungu? Jambo gani basi ni sababu ya kuchaguliwa kwetu?
- Kwa nini Mungu alimfanya Farao kuwa ngumu? Jinsi gani ugumu wa mioyo ya watu unajionyesha, ikiwa ni ya mtu mmoja, ya ukoo au ya watu kwa jumla?
- Nani ndiyo vyombo vya ghadhabu ya Mungu, na zipi ni sababu za kutokutii kwao?
- Kusudi la vyombo vya rehema ya Mungu ni nini, na ipi ni mahali pao pa kuanzia?
- Kwa nini mamilioni ya waumini kutokana na watu mbalimbali waliweza kupokea haki ya Mungu na kuimarika ndani ya neema hiyo?
- Kwa nini watu walio wacha Mungu wa dini zingine wanajaribu kwa bidii kutimiza sheria zao ili wapokee haki za Mungu?
- Je, maana ya usemi wa Paulo ni nini, anapotamka: Kristo ni mwisho wa sheria?
- Kwa nini Wayahudi wanatazama mbele kwa ajili ya kuja kwa Masihi wao?
- Je, uhusiano kati ya imani na ushuhuda ni nini?
- Jinsi gani imani na ushuhuda zinaendelea kukua maishani, kufuatana na mtume Paulo?
- Jinsi gani mtu yeyote anaweza siku hizi, kama anataka, kusikia, kuelewa na kukubali injili?
- Kwa nini Mungu alifanya watu wapya kutoka kwa mataifa yoyote kuwa wateule wake?
- Je, ipi ni maana ya maneno ya Mungu kwa Eliya kwamba, alibakiza watu elfu saba kati ya Waisraeli, wale wote ambao hawakupiga magoti mbele ya Baali?
- Je, ipi ni maana ya maneno ya Paulo kwamba, yeye na wafuasi wote wa Kristo kutoka kwa Wayahudi ni washiriki katika baki takatifu ya wateule wa Mungu?
- Ugumu ule wa Wayahudi ulikuwa na maana gani kwa ajili ya watu najisi ya Mataifa?
- Jinsi gani Wakristo wataweza kuwasihi wasioamini waingie kwenye imani ya kweli?
- Kupandikizwa ndani ya mwili wa kiroho wa Kristo inamaanisha nini?
- Nani atakuwa hatarini, kama kule kupandikizwa kutaharibika?
- Kwa nini ahadi za Mungu hazikosi kutimia, bali zadumu milele?
- Israeli ya kiroho yote ni ya wakina nani?
- Kwa ukamilifu wa neema na hekima ya Mungu inamaanishwa nini?
- How does God continue righteous if he hardens his chosen people, and in the end he accepts the holy remnant, and considers them of all the children of Jacob?
Ukikamilisha masomo ya mihula yote ya mfululizo kwa Warumi na kututumia majibu ya mwisho wa kila muhula, sisi tutakutumia
CHETI CHA
masomo ya kuendelea katika kufahamu barua ya paulo kwa Warumi
ili utiwe moyo kwa ajili ya huduma yako kwa Kristo hapo mbeleni.
Tunataka kukutia moyo ukamilishe na mitihani kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi, ili upate hazina ya kudumu. Tunangojea majibu yako na tunakuombea. Anwani yetu ni hii:
Waters of Life
P.O.Box 600 513
70305 Stuttgart
Germany
Internet: www.waters-of-life.net
Internet: www.waters-of-life.org
e-mail: info@waters-of-life.net