Previous Lesson -- Next Lesson
d) Siri ya ukombozi na wokovu wa watoto wa Yakobo siku za mwisho (Warumi 11:25-32)
WARUMI 11:25-32
"25 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili. 26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa,Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. 27 Na hili ndilo agano langu nao, nitakapowaondolea dhambi zao. 28 Basi kwa habari ya Injili wamekuwa adui kwa ajili yenu; bali kwa habari ya kule kuchaguliwa wamekuwa wapenzi kwa ajili ya baba zetu. 29 Kwa sababu karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake. 30 Kwa maana kama ninyi zamani mlivyomwasi Mungu, lakini sasa mmepata rehema kwa kuasi kwao; 31 kadhalika na hao wameasi sasa, ili kwa kupata rehema kwenu wao nao wapate rehema. 32 Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi, ili awarehemu wote.“
Paulo aliwaangalia wapokeaji wa waraka wake kama ndugu zake katika damu, na kwa njia ya tamko hilo alikiri kwamba, Mungu ni Baba yake sawa alivyo na Baba yao. Mawazo yote kabisa, uchunguzi, na matamko kuhusu amri ya Mungu juu ya kila mtu na hali yake ya milele hayawezi kutimizwa kimawazo kwa njia ya kutambua ya kwamba, Mungu ni mkuu kuliko yote, bali yatajulikana mbele za Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo aliye hai, Baba yetu aliye takatifu, ambaye amejaa na upendo na rehema kwetu.
Baada ya utangulizi huu Paulo anasema habari ya siri, ambayo mwenyewe hakuielewa hadi Baba wa mbinguni alivyomfunulia wazi. Kwa hiyo Paulo anawataka wote watoao maelezo, wahubiri na wajuzi wa theologia wajizuie, ili wasilete filosofia yao wenyewe kuhusu watoto wa Yakobo, bali wasikilize kwa makini kwa neno la Mungu na kulishika kabisa. Yeye anayehubiri mawazo yake mwenyewe anaingia hatarini, kwa sababu mwenyewe anawaza vema na kwa busara, lakini mapema anaweza kupotelea kimawazo; lakini anayekamatana kwa nguvu na neno la Mungu tu na kwa maombezi, tena anaposikiliza vema kwa neno la Roho Mtakatifu, hatua kwa hatua atakua ndani ya ufahamu wa siri za upendo wa Mungu, Baba yetu wa mbinguni.
Siri ambayo Paulo anazungumzia na heshima kwa ajili ya siku za mwisho inajumlisha mambo mengi: Ugumu wa Waisraeli ulikuwa kama hema ya mablanketi mazito, ambayo inawalinda wale wanaoketi chini yake, wasipate miali ya jua, bali inaficha uwezo wa kuona wazi machoni pao, pia na kusikia vema kwa masikio yao. Wao hawaoni, hawasomi wala hawasikii, ingawa wanao uwezo wa kufanya hayo yote (Yeremia16:9-10).
Sio wote, lakini wengi wao wa watoto wa Yakobo ni wagumu. Wanafunzi na Mitume wa Yesu pamoja na watu wa kanisa la kwanza waliungama kwa moyo wakati wa Yohana Mbatizaji. Yeye aliwatayarisha kwa kuja kwake Kristo na wokovu wake, nao waliishi katika ushirikiano wake, wakatambua na nuru ya fahari tukufu.
Kufuatana na kitabu cha Isaya, hali ya ugumu ulianza miaka 700 kabla ya kuja kwake Kristo (6:5-13), naye Yesu alithibitisha jambo hilo wazi (Mathayo 13:11-15), pia na Paulo analieleza kwa huzuni (Matendo ya Mitume 28:26-28). Ndipo ugumu huo ukageuka ukawa tisho kuu, wakati Wayahudi walipomkabidhi Mfalme wao asulibiwe, nao wakazuia huduma ya Roho Mtakatifu. Ndipo Warumi waliwauza kama watumwa kwa sehemu zote za dunia.
Ugumu huo wa Wayahudi hautaendelea daima. Kwa sasa utaendelea hadi hesabu ya waumini kutoka kwa watu wengine itakamilika. Wakati wito huo kwa watenda dhambi wa mataifa mengine utakapokuwa kamili, ndipo Bwana atawapa Wayahudi nafasi ya mwisho ya kutubu na kufanywa wapya.
Lakini hao Waisraeli wote ni wakina nani wataokuwa wanaokoka siku ya mwisho, ambao Paulo anasema habari zao kama jambo la kugusia sana katika historia ya kanisa na watu? (Kumbuka: Uchunguzi huo hauhusiki na mambo ya siasa. Ni uchunguzi wa kiroho tu.)
Jumlisho: Sisi hatuna sababu ya kuharakisha kwamba, sasa tunajua ni nani walio Israeli wa kweli machoni pa Kristo. Biblia Takatifu inatufundisha kwamba, jina hilo „Israeli wa kweli“ halidokezi mwungano wa kisiasa, wala si taifa au ujamaa fulani, bali kwanza kabisa ni jamaa ya ukweli wa kiroho. Siku hizi tunakuta kwamba, maelfu ya watu waliozaliwa mara ya pili ni watoto wa Yakobo kwenye nchi za Mashariki ya kati, Ulaya na Marekani, ambao ni watu waliochaguliwa wa keli, nao ni mwili wa kiroho wa Kristo. Hatuwezi kujua kiasi gani namba yao itakavyoongezeka, lakini tunafahamu kwamba, wanateseka na dhulumu hata ya damu kwa mkono wa yule Antikristo (mshindani dhidi ya Kristo na watu wake), hata ndani ya nyumba zao wenyewe. Hata hivyo, Kristo mwenyewe atawakusanya roho za wafia dini, naye atawapeleka juu kwenye kiti chake kitakatifu cha enzi mbinguni (Ufunuo 13:7-10 na 14:1-5).
Yeyote akitaka kuchimba chini kwenye waraka wa Paulo kwa Warumi (11:26-27) atatambua kwamba, utabiri huo kuhusu ukombozi wa watoto wa Yakobo inaonyesha alama fulani:
Paulo pia alishuhudia kwamba, taifa la Wayahudi wenye kicho cha Mungu, basi walipata kuwa adui wa Injili, kwa sababu ya hiyo agano jipya. Ugumu huo hata hivyo, ulitokeza faida kuu kwa hao watu waliotawanywa, kwa sababu hapo walitambua wokovu kutokana na Kristo hata kwa ajili yao, nao wakashikamana na neema ya Mungu kwa imani.
Lakini vilevile mtume wa Mataifa aliwahakikishia Wayahudi, wale waliokuwa maadui wa kanisa la Rumi kwamba, wao bado ni wapendwa wa Mungu kutokana na imani ya babu zao, na chaguo lao katika uaminifu wao. Hivyo, yule aliyechaguliwa na Mungu anaendelea katika hali hiyo ya kuchaguliwa bila kukatisha, hata kama ametenda dhambi au kukataa hali yake ya kuchaguliwa. Zawadi zote za kiroho na mapendeleo ya imani, ambazo Mungu amewajalia watu mmoja mmoja wenye kuamini wanajumlishwa ndani ya uaminifu wake usioweza kufutika (Warumi 11:29). Kwa hiyo tisitie mashaka yoyote katika kuchaguliwa kwetu na utakaso wa maisha yetu, bali tutegemee kabisa ndani ya neno la Mungu, jinsi mtoto anavyotegemea katika maneno ya babaye.
Katika waraka kwa Warumi 11:30-31 Paulo anarudia kusudi na shabaha ya sehemu ya pili ya barua yake pamoja na ustahi kwa ukombozi wa watoto wa Yakobo. Anajitahidi kuingiza kwa nguvu hizo kanuni ndani ya akili za hao maadui wa kanisa la Rumi:
Kutokana na hayo yote, yeye apendaye kufahamu vema sehemu ya pili ya barua ya Paulo kwa Warumi inampasa achimbe sana ndani ya hizo kanuni, ndipo azigeuze ziwe sala zake na maombezi kwa ajili ya hao watu waliopotea, ili nao wapate kuokoka.
Kwa uhodari Paulo alichunguza kanuni hizo, ndipo akaziweka kuwa msingi kwa kusudi lake la kumhimidi na kumwabudu Mungu. Alimtukuza Yeye Mtakaatifu, kwa sababu aliruhusu kuanguka kwa Wayahudi katika hali ya kutokutii na ya maasi, ili apate kuwarehemu tena wote, ikiwa watakubali ukombozi uliotayarishwa kwa ajili yao kwa imani (Warumi 11:22)
Paulo hata hivyo hahubiri upatanisho kamili kwa ajili ya kila mtu, kana kwamba anasema Mungu angewaokoa watenda dhambi wote siku ile ya mwisho kwa sababu ya upendo wake, na angefuta jehanum kuwa tupu hata na wale wakufuru wanaotaka au kutokutaka kuokoka. Hivyo ndivyo wanavyosadiki wakimtaka mungu kumwokoa Shetani, na kwa hiyo wanamwabudu Shetani, ili wapate kuingia ndani ya paradiso pamoja naye. Hayo ndiyo maono ya uwongo na udanganyifu, maana Mungu ni upendo na ukweli, na haki yake haiwezi kugawanyika.
Paulo alitamani kwamba, Wayahudi wote wataungama na kuokoka kwa njia ya imani ndani ya Mwokozi, wakati Yesu naye alikuwa na uwazi zaidi katika swali hilo. Siku ile ya hukumu yeye atawaambia wale wasiowapenda maskini, kufuatana na ufunuo wake: „Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake“ (Mathayo 25:41). Ufunuo wa Yohana nayo unathibitisha ukweli huo wa kuogofya (Ufunuo wa Yohana 14:9-14 na 20:10+15 na pia 21:8)
SALA: Baba yetu wa mbinguni, tunashangilia na kupata furaha kwa sababu ahadi zako ni za kweli na zinatimia kila wakati. Tunakushukuru kwa ajili ya baki lile takatifu la watoto wa Yakobo, ya kila kabila waliokubali kuungama kweli, wakakubali kupokea malipo ya Kristo, nao wakapokea zawadi ya amani. Utusaidie sisi na watu wetu tuweze kutembea katika nguvu ya Roho wako Mtakatifu, tutii maagizo yako kwa nguvu yake, na tuweze kutazama mbele kwa kuja kwake Mwokozi wetu mpendwa. Amina.
SWALI:
- Kwa nini ahadi za Mungu hazikosi kutimia, bali zadumu milele?
- Israeli ya kiroho yote ni ya wakina nani?