Previous Lesson -- Next Lesson
1. Ghadhabu ya Mungu dhidi ya mataifa imewekwa wazi (Warumi 1:18-32)
WARUMI 1:29-32
"29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji na fitina na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, wenye kusingizia, 30 wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, 31 wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; 32 ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.“
Paulo anaweka orodha ya madhambi machoni petu kuwa kielelezo cha Amri Kumi, kusudi si kwamba tuongelee maneno hayo kwa njia njema kama kuyachunguza sana, au kwa kuwapima watu wengine, na kuwapatiliza kwa vipimo vyetu, bali kwa ajili ya kujitambua sisi wenyewe kwa hofu, tukiangalia namna zote za dhambi zinazowezekana ndani yetu. Yule aishiye bila Muumbaji, amejaa na matendo yasiyo sawa wala si haki, maana roho wa yule mbaya huleta matunda ya namna nyingi ndani ya wale wasio na Roho Mtakatifu. Mtu huishi ndani ya Kristo au ndani ya yule mwovu. Hakuna eneo la katikati.
Bwana Yesu Kristo na Mtume wake Paulo wanaainisha uzinzi kuwa dhambi ya kwanza. Uzinzi unaachisha agano la upendo safi, unafuta tumaini ndani ya uaminifu wa mwenzake, na hivyo unafungua wazi mlango wa kumkataa na kutokuamini. Tamaa ya kidhambi inatawala ndani ya wote ambao hawakujikinahi wenyewe chini ya enzi ya Mungu; sehemu kubwa ya watu ni wazinzi, ikiwa ni katika mawazo, maneno au matendo. Wao ni wachafu na wenye kuharibu. Je, wajijua mwenyewe? Dhamiri yako inasema nawe waziwazi. Basi, usikataa yaliyopita maishani mwako, lakini ukiri yale uliyoyatenda!
Ulijua kwamba mtu bila Mungu hawezi kuwa mwadilifu, lakini mwovu? Kwa nini waalimu husema kuhusu adabu ya kibinadamu, elimu na huduma kwa ajili ya jamii, ikiwa ubinadamu yenyewe ni ovu na ya kuharibu? Hatuhitaji matengeneza au kustaarabisha zaidi, lakini tunahitaji kuumbwa kwa upya na kutengenezwa nia na mioyo yetu.
Yule asiyemjua Mungu hupenda pesa na kujenga maisha yake juu ya mungu hii ya kufa. Upendo wake wa pesa unakua kadiri ya pesa hizo zinavyokua. Hali hii inampeleka mbali na tumaini la kikristo kwenye kiburi na fahari ya maisha, na pia kwenye kutawaliwa na maovu na tamaa za kuchukiza.
Hao wote wanaotawaliwa na tabia ya kupotoshwa wamejaa na ukorofi, namna za kupunja, kisasi, unafiki, kusema uongo, kudanganya na ujanja. Mkorofi hutunga maovu dhidi ya adui zake sawa na dhidi ya jirani. Anajifanya kama anayo urafiki nao, lakini moyo wake ni kioto cha nyoka.
Kwa kawaida nia ya mtu mkorofi ni uchoyo na uwivu kwa ajili ya wengine. Hawezi kufurahia mafanikio mazuri ya mwenzake, maana anataka kuwa mwenye fahari na kufanikiwa kuliko wengine. Zaidi ya hapo, anataka kuwa na mali zaidi, mzuri zaidi, mwerevu zaidi na menye kupewa heshima zaidi ya mwingine yeyote. Unyimivu na choyo ndiyo asili ya matendo maovu karibu yote. Matangazo ya biashara siku hizi hutumia tamaa za kijicho na choyo ndani za watu kwa kusudi la kuendeleza biashara mpya ya vitu kwa gharama yoyote ile.
Hizo tamaa za kuharibu si kwamba zinapotosha akili kutoka kwa yale yaliyo bora, bali pia zinafungua mlango kwa uuaji, chuki, masingizio maovu na kuwasema wengine kwa ubaya. Basi, jaribu kukumbuka moyoni kwamba, Yesu alitufundisha kwamba, mawazo ya kukataa, kudharau au kuchukia wengine, hayo yenyewe ni dhambi sawa na uuaji, maana ndani ya hayo kusudi letu ni kuharibu wengine. Sisi sote tu wauaji na wana wa wauaji machoni pa Mungu.
Roho hiyo ya kuharibu hujionyesha haraka katika maneno na matendo yetu, tunapoanza kuwagawa watu na kupanga vikundi katika jamii na familia zetu, wakati ambapo Roho Mtakatifu hutusukuma kuleta amani na kusuluhisha kati ya vikundi au kuhojiana, ili tuwe watu wa kuleta amani. Je, wewe ni sababu ya vurugu au mgawanyiko kati ya wana wa kutokutii? Je, unatia na mafuta motoni? Au unaleta msamaha na upatanisho, na unapendelea kuweka mwisho kwa uadui, hata kama unatakiwa kujitoa kabisa hata kuumia moyoni katika kutenda mema haya?
Hila ndiyo namna yake ibilisi, ambayo haiwezi kuonekana kabisa ndani ya Bwana wetu. Yeyote anayeendesha mipango yake kwa njia ya ujanja na kuwawekea mitego watu wenye nia njema, wakitumia maneno matamu, huyu ni mwana wa yule mwovu. Matunda ya Roho Tukufu ni uaminifu, ukunjufu na uwazi. Lakini uongo na matawi yake yako mabaya sana.
Matunda mengine ya jehanum ni uchongezi na masingizio wa jamaa zetu kwa kusudi la kujionyesha na kukuza jina letu. Midomo yetu yamejaa sumu, na miguu yetu yaenda haraka kuwaharibu wengine. Tu tayari kutokumjua mwenzetu wa karibu kwa kusudi la kujiokoa mwenyewe na kujipeleka katika hali ya kuonekana vizuri .
Wote watendao dhambi kama hizo, kama ni kwa kusudi au bila kujichunga zaidi, Mungu huwachukia, maana yeyote ampendaye Bwana wake, huyu awapenda na watu pia. Lakini unapoongea na watu bila adabu na kuwadharau au kuwahukumu, ndipo ile roho inayesema toka kwako kwa udhalimu, ndiye wewe mwenyewe. Unapomchukia fulani, unamchukia Mungu, maana Mungu ni upendo, na yeye anayedumu ndani ya upendo anadumu ndani ya Mungu, naye anasamehe, anabariki na anapenda hata yale yasiopendeka, akidumu katika uhusiano na chemchemi ya upendo.
Jinsi shetani alivyo na kiburi kwenye undani kabisa ya moyo wake, ndivyo walivyo waovu wote. Wanajua tu mioyoni mwao madhambi yao yote, maovu na mapungufu yao, na kwa sababu ya ufahamu huo, wanajaribu kufunika mioyo yao ya kuharibu. Wanakuwa wenye kuringa na kutia chumvi ndani ya maneno yao, nao wanatamba na kujivuna kama tausi katika kufikiri kwao na kujifanya wenyewe wajulikane, huku kwa kweli wanajifanya wapuuzi. Watu kama hao ni wakali kwa maskini na wakorofi kwa wote wanaowategemea. Wanahudumia tu tamaa zao wenyewe, nao wamejaa na uovu na kuwa wenye mitego. Wanajionyesha kama wema, wenye vipawa na muhimu, lakini wakiwa peke yao, wanamsikia Mungu akiwahukumu kwa neno moja: „kukatazwa“.
Katika kufunua madhaifu za wengine, na katika kuambatisha ubora wao, wanazidisha mno ukosefu wao, na roho yao mbaya hujionyesha hasa ndani ya familia zao katika namna za kutokutii. Hawahesabu wazazi wao kuwa ni viongozi wao kufuatana na amri za Mungu, lakini kwa ukali wanadai fedha, kuachiliwa huru, na haki mbalimbali, bila kuwa tayari kutekeleza wajibu wao wa kujitoa, upendo na kazi. Kwa tabia hiyo wanakanyaga upendo waliopewa pamoja na uhai wao, pia na kudharau hali ya kutokutambua kwa wazazi wao waso na elimu. Hawajui kwamba, dhambi ni upumbavu wa juu, wakati kumcha Mungu ni hekima ya juu. Hao wote wasiojiweka chini ya Roho wa Mungu hawaelewi jambo lolote kwa usawa, lakini wanaona mambo yote yasivyo sawa. Wamepoteza hali ya usawa kwa ajili yao wenyewe na kwa jamii yote pia.
Katika hali hii hawaoni uwezekano kuwa waaminifu ndani yao, na kwa hiyo hawawezi kutegemewa. Hao wote wasiojitoa kwake Mungu hawawezi kushirikiana vema na watu. Uaminifu wa Mungu humfanya mtu kuwa mwaminifu, lakini aishiye bila Bwana wakeanaendelea katika hali ya upotovu, kutangatanga na maskini.
Mungu wetu ni upendo, rehema na huruma. Ole wao wanaoachana na chemchemi ya mema yote, maana moyo wao unapata kuwa gumu kama jiwe. Wanajipenda wenyewe na kuwachukia wengine. Ujichunguze mwenyewe! Unawapenda adui zako? Unasikia huruma kwa maskini? Yesu alisikia rehema kwa watu wake waliotawanywa, naye aliteseka kwa ajili ya dhambi zao. Unawapatiliza watu wako au unawapenda? Unaishi bila huruma na rehema , au Roho wa Mungu alipata kukufanya upya, ili upate kusimama mbele zake kama kuhani na kuwasimamia wenye dhambi?
Dhambi zetu ziko nyingi kuliko mchanga ufuoni mwa bahari. Umjue Mungu, ndipo utajijua na mwenyewe. Yeyote anayejitenga na tabia ya pekee ya chemchemi tukufu, huyu anastahili kufa tu na aangamie. Wanadamu wote tu wenye dhambi tangu utoto. Unahitaji kufia makosa na dhambi zako leo hii. Utakatifu wa Mungu unadai kuharibika kwako. Huna haki ya kuendelea kuishi. Haki zote za wanadamu ni uongo tu.Tuna haki moja tu ya kufa kwa ajili ya dhambi zetu. Unazunguka mjini kwako kama fulani aliyekwisha kupokea sentenso ya kufa, sio toka kwa watu, bali toka kwa Mungu. Hivyo basi, lini utabadilisha akili yako, na kuungama kabisa na kwa moyo na nia yote?
Usipotubu kabisa, dhambi zako zitafikia mahali ambapo badala yake utaridhika na matendo maovu ya watu wengine. Hapo wewe utatenda dhambi kwa kufurahia na pia utapendezwa na wale watendao dhambi; na hapo utawatia moyo kuyatenda, utawachokoza wayatende, ndipo utawakosesha watoke kwenye hali ya bila hatia, ukiwaambukiza na dhambi za kwako mwenyewe. Huu ndiyo uchokozi wa kusikitisha wa usumbufu huo. Je, haitoshi kwamba, wewe mwenyewe ni mwovu? Na inakupasa uchafue na jamii yako? Ujitazame mwenyewe! Unapendezwa na dhambi zako? Unaridhika na mioyo migumu ya wengine? Je, hujawahi kutiririsha machozi katika toba la kweli kwa ajili yako na ya watu wako? Roho wa Mungu je, amewahi kukufikisha kwenye ungamo wa kweli, au bado uko na kiburi?
SALA: Mungu naomba uwe mwenye rehema kwangu mimi mwenye dhambi. Unafahamu kwamba kila tone la damu yangu ni lenye dhambi, na kwamba ndani ya vijumba kuna chemchemi ya mawazo mabovu. Ninastahili kuangamizwa na ghadhabu yako na hukumu yako ni ya haki. Nivumilie na usiniharibu kufuatana na haki yako. Unibadilishe mimi pamoja na marafiki zangu na majirani wote, ili tsije wote kuanguka kuzimuni. Uwajalie watu wangu na mimi utambuzi wa dhambi na badiliko la mioyo yetu, ili upate kuanzisha ndani yetu viumbe vipya. Unihurumie, ee Mungu, kufuatana na rehema zako za upendo, wala usiniondolee Roho wako Mtakatifu.
SWALI:
- Taja dhambi zile tano katika orodha ya madhambi, ambazo unahisi ni zile zinazoenea zaidi katika ulimwengu wetu wa siku hizi?
Ghadhabu ya Mungu
imedhihirishwa toka mbinguni
juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu
(Warumi 1:18)