Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 013 (The Wrath of God against the Nations)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
A - Ulimwengu Wote Umekaa Chini Ya Utawala Wa Yule Mwovu, Na Mungu Atahukumu Wote Kwa Uadilifu (Haki) (Warumi 1:18 - 3:20)

1. Ghadhabu ya Mungu dhidi ya mataifa imewekwa wazi (Warumi 1:18-32)


WARUMI 1:26-28
"26 Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yaziyo ya asili; 27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. 28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.“

Paulo aliandika maneno hayo ya kutisha, „Mungu aliwaacha“ tena mara tatu katika sura hii ya kwanza. Maneno hayo yanaonyesha mpaka, hasira, pia na hatua ya kwanza ya kuangamiza. Ole wao ambao Mungu aliwaacha wapotee katika utawala wa uovu, maana watakuwa wameanguka kutoka kwenye utunzaji na ulinzi wa Mwenyezi.

Kutengwa na Mungu namna hii inajionyesha yenyewe katika mvuto mkali wa tamaa, pia na mawazo ya kumkataa Mungu. Wanazunguka kama mnyama katika hali ya joto, naye huwaza jambo moja tu ya kutimiza tamaa yake ya kimwili. Ambapo Roho Mtakatifu hatawali ndani ya moyo wa mtu, na asipoitawala mwili wake na nia ya ndani, mtu hugeukia kuwa mzinzi, hata kama amejifunika na kinyago ya adabu nzuri na ya heshima.

Hasa hasa siku hizi, wakati wa usawa wa wanaume na wanawake, baadhi ya wanawake wanadai kuwa na haki kuridhisha tamaa zao bila mwanaume. Zaidi ya hapo, mashirika fulani yanaeneza tabia ya kutwaana waume kwa waume, ili kukomesha mwenendo wa kuzidisha watu duniani. Hata hivyo, Paulo anawafikiria hao wote wanaojipeleka kwenye tamaa katika njia zisizo za asili kwamba, wamepotea katika kujidanganya wenyewe na kuwa chini ya ghadhabu ya Mungu.

Hao wote wanao madhara makuu ndani yao, pia na tabia ya upotovu katika ubongo wao. Hao sio watu wa kawaida tena, lakini wako kama katika ndoto na wanatenda wasiotaka kutenda, maana yeyote atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. Pia kuna shughuli na funganisho mazito yenye dhambi, zinazowafunga wote wasioendelea ndani ya maagizo ya Mungu.

Sababu ya mshuko kwa maendeleo mazuri ina kina kirefu. Wala kiini cha maovu sio upotovu wa kutwaana, lakini ni wale wanaoharibu, wasiotaka kumkubali Mungu mawazoni mwao.Kwa sababu wanajipenda wenyewe na dunia zaidi ya Mungu, walianguka kutoka uchafu hadi uasherati. Mtu anaposoma ushuhuda wa watu waliookolewa na Kristo watatambua haraka kwamba, watu hao kabla ya kuokoka walikuwa mbali sana na Mungu. Kama tokeo la kutokuamini kwao watu hao, walikuwa watumwa wa namna zote za upotovu wa zinaa na uchafu. Lakini wakati Kristo alipowapata, aliwapa msamaha, safisho, badiliko, raha, nguvu, tumaini na furaha.

Lakini basi, anayekaa mbali na Mungu kwa kusudi, na anayezuia mvuto wa Roho Mtakatifu apate kutubu na kukombolewa, atakuwa na ubongo wa kushushwa. Basi hakuna tamko liwezalo kutajwa yenye uzito zaidi kuliko neno hilo: „kushushwa“ limeandikwa juu yake kwa mkono wa Mungu; maana kwa hali hiyo hawezi kurudi kwake Mungu, kwa sababu hatua ya kurudi inahitaji mabadiliko kabisa. Neno la kiyunani „kuungama“ kwa kinaganaga linamaanisha: Mabadiliko ya ubongo (au akili au nia au moyo). Mungu hutazamia mbadiliko kimsingi na kwa uangalifu ndani ya mioyo ya watu, unaotatanisha mgeuzo kabisa ya mawazo yaliyokuwepo pamoja na utendaji wake, kusudi Mungu apokee hayo yote na kuyafanya yawe mapya.

Sasa basi, habari ya moyo wako, je? Akili yako iko wazi kwa sauti ya Roho wa Mungu na wokovu na usafi wake? Ikiwa wewe bado unaishi na wasiwasi, mbali na Mungu, basi umgeukie wakati huo ambapo bado iitwapo „Leo“. Umwulize Bwana wako asafishe utambuzi wako wa ndani na kubadilisha moyo wako. Usiache yale yaliyopita maishani mwako yabakie chafu. Bwana wako ndiye Mponya wako pia. Yeye pekee aweza kukuweka huru na shughuli zako zote ukitaka tu kwa moyo wako wote akufungulie na tamaa zako. Hutaweza kabisa kujiokoa mwenyewe kwa nguvu zako. Unapaswa tu kutaka, kuamua, kuomba na kupokea wokovu wa Bwana, aliye tayari kabisa kukuokoa.

SALA: Ee Mungu mtakatifu, wewe wanijua, na mawazo yangu yote yako wazi mbele zako. Unajua yaliyopita maishani mwangu na pia kila mmoja ambaye nimemtendea dhambi. Nisamehe tamaa zangu na utakase utambuzi wangu wa ndani.Univute karibu na neno lako, ili nipate kukupenda. Sitaki kutenda dhambi tena. Naomba uumbe ndani yangu hali ya kutaka sana, ili nipokee uhuru wangu toka mkononi mwako. Uniokoe na akili yangu ya upotovu na mwili uliochafuka. Wewe ndiwe Mponya wangu na Mwokozi wangu. Ndani yako nategemea.

SWALI:

  1. Jinsi gani Paulo alifafanua jambo la kutokea kwa ghadhabu ya Mungu?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 15, 2022, at 01:20 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)