Previous Lesson -- Next Lesson
a) Mwujiza wa kuvua samaki wengi (Yohana 21:1–14)
Yohana 21:1-3
“Baada ya hayo Yesu alijidhihirisha tena kwa wanafunzi wake penye bahari ya Tiberia, naye alijidhihirisha hivi: Simoni Petro , na Tomaso aitwaye Pacha, na Nathanaeli wa Kana wa Galilaya, na wana wa Zebedayo, na wengine wawili wa wanafunzi wake, walikuwapo pamoja. Simoni Petro aliwaambia, naenda kuvua samaki. Nao wakamwambia, sisi nasi tutakwenda nawe. Basi wakaondoka, wakapanda chomboni; ila usiku ule hawakupata kitu.”
Baada ya kufufuka kwake, Yesu aliwaagiza wanafunzi wake waende Galilaya, penye wilaya yao ya nyumbani, karibu na ziwa la Tiberia (iitwayo pia ziwa la Galilaya). Yeye kama Mchungaji Mwema atawatangulia na kuwakuta kule; lakini kwa ajili ya upendo wake kwao ilimvuta kuwatokea mapema zaidi, wakiwa bado Yerusalemu na kutuliza hofu zao. Hii ndiyo wakati wa jumapili jioni baada ya Pasaka, alipowasalimia na Amani tukufu, pia na kuwatuma wafanye uinjilisti ulimwenguni kote (Marko 16:7; Mathayo 28:10).
Haya basi, wanafunzi baada ya utume huo kuvua watu, waliitika kwa agizo hilo la Yesu? Je, mwujiza wa ufufuo ulibadilisha msimamo wa mawazo yao, hata wakahimiza kufanya uinjilisti ulimwenguni kwa ujumbe wa uzima wa milele, iliyotokea ndani yake? Kwa huzuni twasema, hapana. Waligeukia tena shughuli zao za zamani na kugawanyika katika vikundi vikundi, baadi peke yao kabisa, wengine wakashirikiana na wavuvi.
Basi, jioni fulani Petro alitoka avue samaki, akiwaambia rafiki zake, “Mimi naenda kuvua samaki.” Aliwaachia wakate shauri wenyewe wafuatane naye au la. Wakaungana naye kwenda pwani, wakapanda chombo na kupiga makasia kufika katikati ya ziwa. Wakatupa jarifa zao mara nyingi kwa kuchosha usiku kucha, lakini hawakupata kitu. Walikuwa wamesahau neno la Yesu, “Bila mimi hamwezi kufanya kitu.”
Yohana 21:4-6
“Hata asubuhi kulipokucha, Yesu alisimama ufuoni; walakini wanafunzi hawakujua ya kuwa ni Yesu. Basi Yesu akawaambia, Wanangu, mna kitoweo? Wakamjibu,La. Akawaambia, Litupeni jarife upande wa kuume wa chombo, nanyi mtapata. Basi wakatupa; wala sasa hawakuweza kulivuta tena kwa sababu ya wingi wa samaki.”
Yesu hakuwaacha wanafunzi wake, ingawa walienda kwenye njia za kando. Alisimama ufuoni na kuwangojea warudi. Angaliweza kutupia samaki ndani ya jarife zao, lakini alipenda kuwafundisha kwamba, wasingaliweza kutenda mambo kwa mapenzi yao tu baada ya ushindi wake kuu, wala kurudi kwenye kazi zao za awali. Waliwahi kukubali maungano na yeye; sasa yeye alikuwa ni mshiriki wao, lakini walikuwa wamemsahau katika huzuni na matatizo ya kila siku, na wakafanya kana kwamba yeye hayupo au yu mbali.
Yeye hakusalimu wafuasi wake kama mitume, lakini kama watoto au vijana. Walikuwa wamesahau mengi ya yale aliyokuwa amewaambia, wala hawakutenda kufuatana na mausia yake. Mbali na tabia mbaya hiyo, Yesu kwa unyenyekevu alijizuia kuwakemea, bali aliwaulizia habari ya chakula. Iliwapasa kukiri kwamba hawakukamata kitu, na ya kwamba Mungu hakuwa nao safari hii. Kwa kifupi wakakiri makosa yao.
Kulipokucha, Yesu aliwajia; ilikuwa kama tumaini mpya ilianza kufahamika ndani yao. Yeye hakuwaambia, “Si kitu kama mmekosa”, au “Jaribuni tena, labda mtafaulu. Kwa agizo la kifalme alisema, “Tupeni jarife upande wa kulia wa chombo nanyi mtapata”. Ingawa hawakuwa mbali ziwani, ila karibu na pwani, ambapo samaki wakubwa ni haba sana, hata hivyo, wakahimiza kufuata shauri hili na kutupa jarife upande wa kulia.
Yesu aliwaona samaki majini - jinsi ilivyo hata siku hizi, yeye ajua waliko wale wanaomtamani na kungoja kufikiwa. Yeye akusudia kukutuma kwao. Hasemi, “Kamata wote ndani ya nyavu yako”, lakini kirahisi asema, “Tupa injili - nyavu yako mahali pale ambapo mimi nakuhitaji, ndipo utaona jinsi maneno yangu yanavyofanya kazi.” Wanafunzi walitii hilo agizo geni, hata bila kumtambua kabisa Yesu, aliyeonekana kama mtu wa kawaida tu. Labda alikuwa akitumia salamu ya kawaida, lakini ilikuwa ni sauti ya tumaini. Basi wakashika moyo na kutupa jarife zao, ingawa kwa kuchoka; na ajabu, jarife zikajaa! - Hivyo kuna miongozo ya kiroho zinazotumwa na Bwana kwa mahali ambapo samaki wapo, ndipo anapowatuma, na kumbe, jarife zao zajaa samaki wengi mno, hata wakashindwa kuvuta yote peke yao. Wakahitaji wenzao wenye nia kuwasaidia kwa upendo.
Sala: Bwana Yesu Kristo, tusamehe shughuli zetu za mambo ya kila siku tu, zinazozidi hamu zetu za kuwapata wengine kwa ajili yako. Twakushukuru, kwa sababu unatujia, hata wakati tunapotangatanga. Wewe watuongoze tukiri makosa yetu. Utufundishe kutii neno lako na utuelekeze kwa wale wanaokutafuta, ndipo uwaongoze waingie ndani ya navu zako za Injili, ili nao wapate kuwa wako daima.
Swali 130: Kwa nini kukamata samaki wengi hivi ilikuwa ni sababu ya aibu kwa wanafunzi?