Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 125 (Conclusion of John's gospel)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 4 - Nuru Inashinda Giza (Yohana 18:1 - 21:25)
B - UFUFUO na KUTOKEA KWAKE KRISTO (YOHANA 20:1–21:25)

4. Mwisho wa Injili ya Yohana (Yohana 20:30–31)


Yohana 20:30-31
“Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki. Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.”

Mwisho wa sura hii tunafikia neno kama alivyoandika Yohana mwenyewe. Mwandishi huyu mwenye kutafakari sana habari za Mungu na mwinjilisti alitangaza kutokea kwa nuru ya Mungu katika giza iliyoshindwa kuipokea. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. Mwinjilisti huyu mkuu alituvuta kwenye kina cha ushirikiano tukufu ndani ya nafsi ya Yesu. Alitufafanulia kifo na ufufuo wa Kristo, kwa namna tupate kuamini ndani yake na kumwona aishivyo kati yetu.

Kwa jumla, huyu Mtume ametuandalia shabaha nne, ili kutuwekea wazi maana ya injili yake na lengo la maandiko hayo.

Yohana hakuandika vitabu vingi, ili ataje maneno na matendo yote ya Yesu. Maana angehitaji kuandika magombo ya vitabu. Alichagua ishara zile na matamshi yale, ambayo yatasisitiza nafsi ya Yesu ya pekee isiyokuwa na fani. Uandishi wake haikuwa namna ya kuandikishwa na Roho wa Mungu, kana kwamba ilikuwa ni mawazo yaliyomjia wakati akiwa bila kujitambua. Hapana, alikuwa akiwajibika, alipofunuliwa na Roho Mtakatifu, ili achague yale matokeo ya pekee, na kwa upendo mwingi alichora sura ya Mwana Kondoo wa Mungu achukuaye na kupeleka mbali dhambi ya ulimwengu, - kafara aliyechinjwa.

Yohana aliandika injili hii kwa ajili yetu tutambue kwamba huyu mtu Yesu wa Nazareti, dhahiri na wa kudharauliwa, ndiye Kristo yule aliyeahidiwa, na pia Mwana wa Mungu wakati uo huo. Kwa vyeo hivi viwili aliungana na matazamio ya Wayahudi wakati wa Agano la Kale. Kwa njia hiyo alihukumu taifa lake iliyomsulibisha mwana wa Daudi aliyeahidiwa. Mtu Yesu alithibitisha kuwa ndiye Kristo kweli na kuwa Mwana wa Mungu. Upendo kuu wa Mungu na utakatifu wake usio na waa haiwezikani kufikika, wala si kwa yeyote mwenye nia safi. Yohana anamtukuza Yesu kwa namna ya juu kabisa. Picha yake safi ya Yesu aliyeichora kwa maneno yake kwetu haina mfano, ila itusaidie tu kutambua upendo wa Mwana wa Mungu, aliyekuja kuwa mwanadamu, ili sisi tupate kuwa watoto wa Mungu.

Yohana hakusudii kuunda tu ndani yetu aina ya kukiri kanuni, lakini anakusudia tupate kuwa na pingu za kutuunganisha na Mwana wa Mungu. Kwa vile Yesu ni Mwana, basi Mungu anakuwa Baba yetu. Tangu huyu wa juu sana ndiye Baba yetu, yeye naye aweza kutokeza watoto wengi watakaojaliwa na uzima wake wa milele. Kuzaliwa mpya kwa damu ya Kristo na Roho yake ndani yetu, hiyo ndiyo shabaha kuu ya injili ya Yohana. - Haya je, wewe umezaliwa kiroho, au wewe bado u kama mfu katika dhambi? Je, uzima wa Mungu unaongoza ndani yako, au wewe hujawa na Roho yake Mtakatifu ndani yako?

Tendo la kuzaliwa mara ya pili inakamilika kwa imani ndani ya Mwana wa Mungu. Yeyote amtegemeaye atapokea uhai huo tukufu. Tunao huo uzima tukiwa na uhusiano wa kudumu naye kwa imani. Yeye anayedumu ndani ya Yesu, atagundua kwamba Yesu naye atadumu ndani yake. Mwumini wa namna hiyo atakua kiroho na katika ukweli, na matunda ya maisha tukufu yatastawi ndani yake. Uzima wa milele ni upendo wa Mungu ukitusukuma kuwaongoza na wengi wapate imani ndani ya Yesu, nao wapate kupenda na kudumu ndani yake na yeye pia ndani yao daima.

Sala: Bwana Yesu, twakushukuru kwa ajili ya injili jinsi mwinjilisti wako Yohana alivyoiandika. Kwa njia ya kitabu hiki cha kipekee tunatambua enzi na ukweli wako. Tunakuinamia kwa furaha, kwa sababu ulituongoza tufikie imani ndani yako, ukatujalia kuzaliwa kwa upya kwa neema yako. Utushike kabisa ndani ya ushirikiano wako, tukupende kwa kuzishika amri zako. Tujalie tushuhudie kwa jina lako waziwazi, ili na marafiki zetu wapate kukutegemea na kupokea uzima kweli kwa imani.

Swali 129: Jambo gani Yohana anafanyiza sana katika maneno ya mwisho ya injili yake?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on June 29, 2017, at 05:57 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)