Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 121 (Jesus appears to the disciples)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 4 - Nuru Inashinda Giza (Yohana 18:1 - 21:25)
B - UFUFUO na KUTOKEA KWAKE KRISTO (YOHANA 20:1–21:25)

2. Yesu awatokea wanafunzi wake kwenye chumba cha orofani (Yohana 20:19-23)


Yohana 20:21
„Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba mimi, mimi nami nawapeleka ninyi.“

Yesu aliporudia salamu yake, „Amani iwe kwenu“, alizingatia habari ya utakaso wa dhambi na upatanisho, lakini aliwataka wapate kuwa „wafanya amani“ kwa kutolea wokovu kamili kwa ubinadamu uliopotea. Pale msalabani Mungu aliwasamehe wanadamu wote makosa yao. Hali halisi hiyo mpya inahakikisha radhi kwa wahalifu, pia na ahadi ya kuweka mbali habari ya hukumu kwa waaminio, pia na tumaini la kuwekwa huru na hali ya kupotea. Yesu aliwatuma wafuasi wake ndani ya ulimwengu, ili wahubiri amani ya Mungu kwa watenda dhambi.

Wote waliookoka kwa neema ya Mungu wamebadilishwa moyoni, nao watawasamehe hata adui zao, jinsi Mungu alivyowasamehe. Atachagua kuvumilia hila, kuliko kutenda yasiyo haki mwenyewe. Hivyo ataeneza harufu ya mbinguni kwa maeneo karibu naye, jinsi Yesu alivyotamka, „Heri wafanyao amani, nao wataitwa wana wa Mungu“. Shabaha yetu katika uinjilisti sio kubadilisha hali zilivyo au kuleta amani ya kijuujuu tu kati ya mataifa; bora tuombee roho za watu wapate kubadilishwa, na mioyo ya mawe yageuzwe kuwa laini. Kwa ugeuzi wa aina hiyo hata mabadiliko ya kisiasa yatatokea.

Yesu aliinua hali ya huduma ya wanafunzi wake kwenye usawa na hali yake akisema, „Jinsi Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka.“ Basi, jinsi gani Mungu alimtuma Mwana wake? Kwanza alimtuma akiwa Mwana, pili, atangaze ubaba wa Mungu, na utakatifu wake kwa maneno na matendo na katika kusali. Tatu, Yesu alikuwa ndiye mwenye Neno la Mungu, akifurika na upendo wa daima. Kwenye malengo hayo tutakuta maana na shabaha ya uinjilisti wetu. Kwa njia ya kifo chake, Yesu alitufanya sisi tuwe watoto wa Mungu, ili tuishi maisha ya utakatifu, bila mawaa mbele zake na mbele za watu katika upendo.

Wakristo ndiyo mabalozi wa Kristo, waliofanywa haki, waliotakaswa, ili waonyeshe kiini na upendo wa Baba yao wa mbinguni. Hiyo ndiyo hali halisi ya ujumbe wao, kwamba Baba, kwa njia ya kifo cha Kristo, amewafanya kuwa watoto wake. Msalaba ndiyo namna ya hali yao mpya , na imani ndiyo njia ya kufanywa wana.

Jinsi Yesu alivyozaliwa , ili afe na kuwa dhabihu, vivyo hivyo wafuasi wake wanaishi kwa kuonyesha maana ya sadaka. Hawajigambi, bali kujihesabu kuwa watumwa wa Mwenye Enzi na watumishi wa watu wote. Bwana wao aliwaweka huru na tabia yao ya umimi, ili wapende jinsi yeye alivyopenda.

Sala: Bwana Yesu, tunakushukuru, kwa sababu ulituita sisi tusiostahili, ili tumtukuze Baba na jina lako kwa mawazo yetu, maneno na matendo. Asante kwa kutusamehe dhambi zetu; wewe unatutakasa, ili kueneza amani yako kwa mioyo ya watu wengine, ili nao wapate kumulikiwa na kuishi kwa kweli. Tunakushukuru, ee Kristo, kwa sababu umetufanya tuwe wana wa upendo wako, ili na sisi tuweze kupenda na kusamehe, jinsi ulivyofanya wewe katika rehema zako.

Swali 125: Jambo gani ni kigeni katika kuwatuma wanafunzi kwa uinjilisti?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on June 29, 2017, at 05:51 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)