Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 114 (Burial of Jesus)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 4 - Nuru Inashinda Giza (Yohana 18:1 - 21:25)
A - Matokeo kuanzia kukamatwa kwake Yesu hadi kuzikwa kwake (Yohana 18:1 - 19:42)
4. Msalaba na kifo cha Yesu (Yohana 19, 16b – 42)

f) Kuzikwa kwake Yesu (Yohana 19 : 38 – 42)


Yohana 19:38
“Hata baada ya hayoYusufu wa Arimathaya, naye ni mwanafunzi wa Yesu, (lakini kwa siri, kwa hofu ya Wayahudi), alimwomba Pilato ruhusa ili aondoe mwili wake Yesu. Na Pilato akampa ruhusa. Basi akaenda, akauondoa mwili wake.”

Kwenye baraza la Wayahudi sio wote sabini waliokubali hukumu iliyopitishwa juu ya Yesu. Kutokana na machimbo ya maarifa ya mambo ya kale inaonekana kwamba, hukumu hutimizwa tu ikiwa kama kuna wawili au zaidi wasiokubali uamuzi; lakini kama wote wanakubali kupitisha uamuzi wa kifo, inamaanisha kwamba udhalimu wa kibinadamu dhidi ya mstakiwa imetawala, na hivyo kuonyesha kwamba, baraza limeanguka kwenye ukosefu wa haki. Kama ni hivyo, kesi huwa inarudiwa na ushahidi kuchunguzwa kwa uangalifu zaidi.

Kwa kuamini kwamba kawaida hiyo ilifuatwa wakati wa siku za Yesu, ina maana kwamba, kwa vyovyote wajumbe wawili walikataa uamuzi. Mmoja alikuwa ni Jusufu wa Arimathaya, mwanafunzi wa siri (Mathayo 27:57 na Marko 15:43). Alihofia kupoteza kiti chake ndani ya baraza, au shirika lake katika uongozi wa taifa, na tunashukuru kwa hekima yake ya kukomaa. Yusufu alimchukia Kayafa kwa ajili ya kutokuendesha mambo kwa haki na kusimamia vikao vya baraza kwa madanganyo. Yusufu aliendelea kwa kutokupendelea, na hadharani alikiri uhusiano wake na Yesu; ila uamuzi wake huo ulichelewa, na ushuhuda wake ikawa ni kukanya uamuzi wa Baraza; lakini mambo yalivyoendelea yakafikia hatua ya kupitisha uamuzi wa kumsulibisha Yesu.

Baada ya kifo cha Yesu, Yusufu alimwendea Pilato (alikuwa na haki ya kufanya hivyo). Pilato alikubaliana na haja yake, akampatia ruhusa kushusha mwili wake Yesu kutoka msalabani na kumzika.

Hivyo Pilato mara nyingine akawalipiza kisasi Wayahudi, ambao wao huwaburuta wahalifu waliouawa na kuwatupa ndani ya bonde la Hinnom waliwe na mbwa mwitu mahali pa kuchoma takataka. Mungu alimlinda Mwanawe na aibu ya namna hiyo. Alitimiza huduma yake kama dhabihu tukufu msalabani. Baba yake wa mbinguni alimwongoza Yusufu kumzika kwa taratibu ya heshima.

Yohana 19:39-42
„Akaenda naye Nikodemo (yule aliyemwendea usiku hapo kwanza), akaleta machanganyiko ya manemane na uudi, yapata ratili mia. Basi wakautwaa mwili wake Yesu, wakaufunga sanda ya kitani pamoja na yale manukato, kama ilivyo desturi ya Wayahudi katika kuzika. Na palepale aliposulibiwa palikuwa na bustani; na ndani ya bustani mna kaburi jipya, ambalo hajatiwa mtu ye yote ndani yake. Humo basi, kwa sababu ya maandalio ya Wayahudi, wakamweka Yesu; maana lile kaburi lilikuwa karibu.“

Mara moja, Nikodemo naye akatokea karibu na msalaba. Alikuwa ndiye mjumbe wa pili aliyekataa maamuzi ya Baraza. Alijaribu mapema kufuta hukumu hiyo ya siri iliyopitishwa na Baraza dhidi ya Yesu na akadai kikao kingine yenye uaminifu zaidi kuthibitisha mambo (7:51). Huyu shahidi wa Yesu akafika, akileta na kilogram 32 wa manukato ya thamani, pamoja na nguo za kuzika (sanda) ili kufungia mwili ulioraruliwa sana, pia na kumsaidia Yusufu kuutelemsha mwili na kuizika baada ya kuitayarisha na yale manukato, taratibu iliyofuatwa na watu wenye uwezo. Ilipasa kuharakisha shughuli hizo, ili kuikamilisha kabla ya saa sita Ijumaa jioni (kwa kiswahili saa 12 jioni), ndiyo saa inapoanza Sabato, na kazi zozote hazitakiwi tena. Walibakiza muda mfupi tu.

Baba wa Bwana wetu Yesu aliwaongoza watu hao wawili kumheshimu Mwana wake mfu, ili na ahadi ya Isaya 53:9 ipate kutimia kwamba, atazikwa na watajiri na wenye heshima kwenye kaburi safi. Ili kuchonga kaburi ya namna hii ndani ya mwamba ilikuwa ni kazi kubwa ya gharama. Basi hapakuwa na njia bora zaidi ya kumheshimu Yesu, ila Yusufu kumpatia kaburi lake mwenyewe lililokuwa karibu na mahali pa usulibisho, hapo nje ya kuta za jiji. Hapo basi wakailaza mwili wake Yesu juu ya kiti cha mwamba, bila sanduku, ila kuvingirishwa ndani ya sanda, ikiwa imepakwa na kunyunyizwa manukato na marashi zilizoletwa na Nicodemo.

Kweli, Yesu alifariki; maisha yake ya hapo duniani yalimalizika, akiwa bado kijana wa miaka thelethini na mitatu. Alizaliwa ili afe. Hakuna upendo kubwa zaidi inayoweza kugunduliwa ila hiyo ya kutoa uhai wake kwa ajili ya wapendwa wake.

Sala: Bwana Yesu Kristo, asante sana kwa ajili ya kufa kwako kwa ajili yetu. Pamoja na waumini wote mimi nami nakupenda, kwa sababu upendo wako ulituokoa kutokana na ghadhabu tukufu, na hivyo kutuunganisha na umoja wa Utatu Utakatifu. Pokea maisha yangu kama ASANTE kwako, na mimi nitukuze msalaba wako.

Swali 118: Kuzikwa kwake Yesu kunatufundisha nini?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on June 25, 2017, at 02:44 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)