Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 085 (Christ predicts Peter's denial; God is present in Christ)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 3 - Nuru yang’aa ndani ya shirika la Mitume (Yohana 11:55 - 17:26)
B - Mambo yaliyofuatana na chakula cha Bwana (Ushirika utakatifu) (Yohana 13:1-38)

4. Kristo anatabiri jambo la kukana kwa Petro (Yohana 13:36-38)


YOHANA 13:36-38
„Simoni Petro akamwambia, Bwana, unakwendapi? Yesu akamjibu, Niendako huwezi kunifuata sasa; lakini utanifuata baadaye. Petro akamwambia, Bwana, kwa nini mimi nisiweze kukufuata sasa? Mimi nitautoa uhai wangu kwa ajili yako. Yesu akamjibu, Je, wewe utautoa uhai wako kwa ajili yangu? Amin, amin, nakuambia, Jimbi hatawika hata wewe utakapokuwa umenikana mara tatu.“

Petro alikuwa amechanganyikiwa moyoni, na hakuweza kusikiliza vema yale ambayo Yesu alieleza juu ya upendo. Jambo ambalo alitambua lilikuwa kwamba, Bwana wao alikuwa anawaondoka, tena katika kuzungukwa na taabu kuu, katika kuteseka na kusalitiwa. Alijitegemea mwenyewe, katika uaminifu na shabaha yake. Alimhakikishia Yesu kwamba, atamfuata hata kwa gharama yoyote ile. Hakutambua kutokuweza kwake na mipaka yake. Alitegemea kabisa kutimiza matamshi yake. Aliwaka kwa juhudi kwa ajili ya Yesu, tayari kumpigania na hata kufa kwa ajili yake.


C - Hotuba ya kuaga kwenye chumba cha orofani (Yohana 14:1-31)

1. Mungu yupo ndani ya Kristo (Yohana 14:1-11)


YOHANA 14:1-3
“Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi nanyi mwepo.”

Wanafunzi walivurugwa mawazo na habari kwamba Yesu alikuwa anawatoka, na ya kwamba hawataweza kufuatana naye mahali pake. Yesu naye alikuwa ametabiri kwamba Petro atamkana, iwapo yeye alisisitiza kumfuata na kujivuna na imani yake imara. Pengine baadhi ya Wanafunzi walijisikia kwamba wataeleweka vibaya katika kumfuata Yesu, wakati alipoeleza kuondoka, hata na kufa kwake. Yesu alitamka kinyume cha huzuni na masikitiko yao kwa kuwapa agizo: Mtegemeeni Mungu kabisa, yeye ndiye msingi imara wakati wowote, hawezi kutingishwa wakati hata mengine yote yatatetemeka. – Yesu anakemea hata mashaka yetu ya siku hizi; hofu maana yake ni kutokuamini. Baba yako wa mbinguni hawezi kukupotosha au kukuacha. Yeye ndiye ushindi anayeshinda yote ya duniani. Hii iwe imani yako!

Yesu alidai kipimo hicho hicho cha imani kwa wafuasi wake, pamoja na tumaini na maombi, jinsi Baba yake anavyostahili. Maana yeye ni umoja na Baba. Jinsi Baba anavyothibitisha siku zetu za mbeleni, ndivyo na Mwana anavyohahikisha. Ndani ya Mwana pia Baba alikuwa yupo ulimwenguni. Upendo wake unastahili tegemeo letu. Ukweli wake ni mwamba imara.

Kwa sababu hiyo yeye alifunua jambo kwa wanafunzi wake litakalotokea baada ya kifo na kupaa kwake mbinguni: Kwake Mungu kuna makao makubwa na bora zaidi kuliko majumba ya starehe ya matajiri yote mijini au pote mashambani. Jumba la Mungu la juu launganika kama jiji kuu, pana na kwa kuwatosha watakatifu wote toka pote duniani na ya wakati wote. Hata kama wakati huu unaishi ndani ya hema au kibanda kidogo, usihangaike. Ndani ya jumba la Baba yako kuna vyumba vingi mno na nafasi ya kuishi kwa raha. Ametayarisha pa nyumbani kwa ajili yako, safi, lenye joto njema na nuru ya kutosha. Unakaribishwa kuishi huko karibu na Baba yako daima.

Mungu mwenyewe huwapenda wanaomwamini Kristo na kuwatayarishia makao. Yesu aliporudi mbinguni, alichunguza makao hayo na kukamilisha matayarisho yake. Lakini pia aliamua kurudi kwetu; hakusudii kuwa mbali nasi. Atarudi ili awavute wafuasi wake kwake. Anawapenda jinsi bwana arusi anavyompenda bibi arusi; hivyo anakusudia kuonyesha kanisa lake, bibi arusi yake, mbele ya Baba; sio kwa ajili ya kujulishwa kwa Baba, lakini wawe kama yeye alivyo ndani ya familia ya mbinguni. Tutakuwa naya daima, hali tunaongozwa chini ya ulinzi wake na kufurahia wema wake.

YOHANA 14:4-6
“Nami niendako mwaijua njia. Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? Yesu akamwambia, Mimi ndimi nja, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”

Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Ninyi mnajua niendako, nanyi mnajua njia kwake Mungu.” Tomaso aliitika, “Twawezaje kujua nia ile, wakati tusipojua uendako hapo karibuni?” Katika huzuni zake alishindwa kuona lengo la mbali. Hofu alimtingisha; alipoteza akili yake ya kutambua mwelekeo.

Yesu akamhakikishia kwa upole, “ Mimi ni njia kwenda kwa Mungu; upendo na ukweli wangu ndiyo sheria kamili ya kuwaongoza kwa yale ya kimbinguni. Mimi ndimi kanuni ya huruma, na kwa hiyo Mungu atawahukumu. Msijipime kwa vipimo vya kibinadamu visioweza kuwa sawa. Shikeni sana njia inayoongoza kwake Mungu. Njooni kwangu, mkajilinganishe na mimi; hapo mtatambua kwamba ninyi hamna kitu, ila kuwa wenye dhambi na wachafu.”

Kristo hatakusukuma toka hofu kwenye hofu nyingine, toka kukata tama kwenye hali ya kukata tama tena. Unapofikia sehemu za chini kabisa maishani mwako, yeye hunyosha mkono wake kwako, ili akuokoe, akisema, “ Sasa nakupatia ukweli mpya, ukweli ule wa zamani ulioiacha nyuma. Mimi nimekufia, nami nimetokeza Agano Mpya ya rehema. Dhambi zako zimesamehewa; imani yako imekuokoa. Shikamana nami na kutulia ndani ya hali halisi ya kupokelewa kama mtoto. Ndani yangu utapokea ukweli wa kumwelekea Mungu. Pasipo mimi basi utapotea.”

Pengine wewe utasema, “Nayasikia hayo yote, lakini napungukiwa imani, nguvu na utakatifu.” Yesu anakujibu, “Mimi nakupatia uzima wa milele; mimi ndimi chemchemi ya uhai. Nishike tu kiimani nawe utampokea Roho Mtakatifu. Ndani ya Roho huyu utaona uhai tele.” Yeyote anayemtegemea Kristo ataishi milele. Usije ukasogea mbali naye; maana yeye ndiye uhai wako. Ama unaendelea kama mfu dhambini, au unakuwa hai ndani ya Kristo. Hakuna njia ya tatu katikati. Kristo ndiye uhai wa mwamini.

Wote waliounganika na Kristo, hao wanasimama mbele ya Mungu wakimwona kuwa Baba wa huruma. Hakuna dini, filosofia, sheria au sayansi iwezayo kukusogeza kwake Mungu. Kipekee Kristo, Mwana wa Mungu ndiye awezaye; ndani yake Baba mwenyewe asimama mbele yako. Jesu ndiye ufunuo kamili wa Mungu. Hakuna awezaye kumfahamu Baba isipokuwa ni yeye tu. Tunayo mvuto ya kuweza kumfahamu Mungu; twamwelekea, kwa sababu Kristo ni upendo na kuweza kutufanya kuwa watoto wa Mungu.

YOHANA 14:7
„Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; Tangu sasa mnamjua, tene mmemwona.“

Watoto wa ulimwengu huu wako mbali na Mungu kwa sababu ya dhambi zao. Hakuna mtu awezaye kumfahamu Mungu kutoka kwa mapenzi yake mwenyewe. Hakuna aliyewahi kumwona Mungu, ila Mwanawe pekee, aliye kifuani mwa Baba. Naye atueleza: Kama mnaglinijua mimi, mngalimjua pia na Baba. Ila hawakufahamu hilo. Kufahamu hivyo haimaanishi kuyaelewa kisayansi tu, lakini inamaanisha kubadilishwa moyoni na kufanywa kwa upya. Kumfahamu Mungu hivyo inaingia ndani ya utu wetu na kujionyesha katika utendaji ya kila siku. Usijidanganye, kusoma sana mambo ya kidini bado haimaanishi kumfahamu Mungu. Linalofanya hayo ni kukubali nuru linaloangaza Injili. Hapo utabadilishwa na kuwa nuru pia.

Kwa kutushangaza, saa ya kusalitiwa Yesu aliwaambia wanafunzi wake, „Tangu sasa ninyi mtanijua. Mimi sio mshindi wa mwisho, mwenye hekima yote na tukufu, bali ni Mwana Kondoo wa Mungu achukuaye dhambi ya ulimwengu pia na kuiondoa. Ndani ya kifo changu cha kuridhisha, Mungu anajidhihirisha mwenyewe kuwa Baba wa upatanisho; maana hataki kuhukumu makosa yako kwa ghadhabu au kuangamiza, lakini ataniadhibu mimi, Mwana wake, ili ninyi mwekwe huru na kubadilishwa kuwa watakatifu, mkiingia ushirikiano naye kama watoto wake.“

Msalabani Mungu ajiweka wazi kuwa Baba. Yeye Mwinuliwa hayuko mbali nasi, lakini yeye ni upendo, rehema na ukombozi. Mungu ndiye Baba yako wa binafsi. Ninyi ndiyo wale mnaoamini ndani yangu, na ninyi pekee mwajua ukweli wa Mungu. Ufahamu huo utawabadilisha, ili mpate kuelewa katika mambo ya maisha yenu kustaajabiwa, jinsi mnavyoyaendesha maisha yenu kwa maadili.

YOHANA 14:8-9
„Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha. Yesu akamwambia, Mimi nimekuwepo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?”

Yesu aliposema, “ Mmemwona Baba nanyi mnamfahamu.” Filipo alikuwa anashangaa na karibu aseme, “Hapana, hatujamwona”, lakini alihangaishwa na enzi ya Bwana wake. Badala yake akatamka maneno haya, “Bwana, utuonyeshe Baba, ndipo itatosha.” Jibu hilo latuonyesha kwamba alitambua enzi ya Yesu na mamlaka yake. Siri hiyo ilitegemea ule umoja na Baba. Iwapo ilipasa sasa kutengana nao, basi ilitosha kuwaonyesha Baba hata dakika moja tu, ili wao wapate kujitoa kabisa jinsi alivyokuwa yeye, pia na kuongozwa na enzi ya Mwenyezi. Maana ndipo wangefahamu Mungu alipo, na hivyo kupokea mamlaka juu ya watu, nguvu ya kuponya na kuchuchia.

Lakini kwa ombi hilo Filipo alikiri kwamba, hadi hapo bado hajamfahamu Baba wala Mwana alivyo. Alikosa kutambua uungu wake na ukweli. Yesu hakumkemea, lakini alikuwa na huruma; na kwenye jioni yake ya mwisho alitamka ukweli ulio kuu, “Aliyeniona mimi, amemwona na Baba”. Kwa neno hilo la kulenga shabaha, Yesu alirarua kifuniko kilichowazuia hao wanafunzi. Basi hakuna maono wala ndoto zinazoweza kufunua ukweli kumhusu Mungu; ila ni nafsi ya Yesu Kristo tu awezaye hayo. Maana yeye hakuwa mtu mwenye hali kubwa, lakini ndani yake tulimwona Mungu hasa. - Siku hizi unaweza kuwa na maono juu ya Mungu ikiwa unamwona Yesu na kumtambua vema. Tomaso naye alisikia maneno haya, na akakosa kutambua uzito wa maneno hayo. Lakini baada ya ufufuo wa Yesu yeye akavunjika mbele ya Bwana wake na kulia, “Bwana wangu na Mungu wangu!”

YOHANA 14:10-11
“Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu ; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba na Baba yu ndani yangu; la, hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.”

Pengine inawezekana kwa mwanafunzi kukumbuka injili kimoyomoyo na bado amwona Yesu kwa uhafifu tu, bila kutambua shabaha yake hasa, kama hajapata kufanywa upya moyoni kwa njia ya Roho Mtakatifu. Jesu alimchochea Filipo na swali, ili kumfikisha kwenye imani kamili zaidi juu ya uungu wake, “Je, hujaamini kwamba mimi ni ndani ya Baba? Lengo la maisha yangu ni kumtukuza Baba. Mimi nimo ndani ya Baba. Yu ndani yangu kimwili. Ukamilifu wa uungu inakaa ndani yangu. Nimezaliwa na nguvu ya Roho Mtakatifu, nami naishi kati yenu bila kuwa na dhambi. Namjua Baba tangu milele, na ufahamu huo umekuwa ndani ya utu wangu. Ndani yangu anafunua wema wake wa kibaba na rehema zake halisi”.

“Ninayo thibitisho kwa ushuhuda huo: Ni maneno yangu yenye enzi pamoja na matendo yangu matukufu. Ikiwa mnaona vigumu kuwa na imani kwa kuwepo kwa Baba ndani yangu, basi sikilizeni maneno yangu, maana kwa hayo Baba anasema kwenu kupitia kwangu. Maneno hayo yawahakikishieni uhai, nguvu na ujasiri. Kama hamwelewi maneno yangu, basi angalieni matendo yangu; Mungu mwenyewe hutenda kazi kati yenu kwa ishara za mbinguni. Anawaokoa kwa njia ya mimi, ninyi mliokuwa mmepotea. Sasa mtaona saa ya kusulibiwa kwangu tendo la Mungu lililo kuu kuliko yote, akipatanisha binadamu na nafsi yake kwa njia ya kufa kwangu. Fungueni macho yenu, msizibe masikio yenu. Mtamtambua Mungu katika tendo la usuluhisho. Huyu ndiye Mungu wa kweli asiyekusudia kuwaangamiza, bali kuwaokoeni.”

SALA: Bwana Yesu Kristo, kwa neema nathubutu kusema: “Bwana wangu na Mungu wangu!” Nisamehe kutokuamini kwangu na upungufu wa upendo. Nifungulie macho yangu ya ndani kwa ajili ya Roho wako Mtakatifu, ili niweze kumwona Baba ndani yako, na kubadilishwa ndani ya upendo wake; ili na kule kukufahamu wewe sawasawa kuweze kuniletea uzima badala ya kifo. Ufunue kiini cha utukufu wako kwa watu wasioamini, ili wao nao washike maisha mapya kwa imani.

SWALI:

  1. Uhusiano wa Kristo na Mungu Baba ni wa namna gani?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on September 01, 2014, at 04:43 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)