Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 083 (The traitor exposed and disconcerted)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 3 - Nuru yang’aa ndani ya shirika la Mitume (Yohana 11:55 - 17:26)
B - Mambo yaliyofuatana na chakula cha Bwana (Ushirika utakatifu) (Yohana 13:1-38)

2. Msaliti anawekwa wazi na kuharakishwa (Yohana 13:18-32)


YOHANA 13:21-22
„Naye alipokwisha kusema hayo, Yesu alifadhaika rohoni, akashuhudia akisema, Amin,amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti. Wanafunzi wakatazamana, huku wakiona shaka ni nani amtajaye.“

Yesu aliwaeleza wanafunzi wake habari ya kupendana wao kwa wao na kuhudumiana. Yeye mwenyewe alikuwa ni mfano wa unyenyekevu na upole mbele zao, na aliwatabiria kwamba, enzi yake itamulikia katikati ya hali ya udhaifu, ili watambue mapema kwamba yeye ndiye Bwana, mtendaji na kiongozi wa matokeo, hata saa ya kufa. Kwa sehemu ya kuweka mambo wazi hivyo, Yesu alionyesha na usaliti wa Yuda na alimkubali afanye udhalimu huo, ili kwamba Yuda asionekane anatenda hayo kufuatana na shauri lake la binafsi tu, lakini katika usawa na mipango ya mbinguni.

Yesu alidhihirisha kwa wanafunzi wake kwamba mmojawao aliamua kumkabidhi kwa Baraza kuu la Wayahudi. Tangazo hilo likaja kama mlipuko wakati wa sherehe ya furaha. Yesu hakutangaza jambo hilo kwa bahati tu, lakini mwenyewe alikuwa anasumbuka sana rohoni, kwa vile alikuwa amefikia kaburi la Lazaro. Alihangaika hasa kwa wazo kwamba hata Baba yake atamwacha peke yake. Yesu alikuwa amempenda na Yuda na kumchagua; ilionekana kwamba haiwezekani kabisa kwamba rafiki wa kuchaguliwa angemsaliti Mwana wa Mungu. Lakini hata Biblia linataja hilo jambo katika Zaburi 41:9, „Aliyekula chakula changu, ameniinulia kisingino chake.“

Basi, kwa hali hiyo, kila mwanafunzi alimchunguza mwenzake kwa kuwaze, „Je, huyu ndiye msaliti?“ Walikuwa na mashaka kama kweli itawezekana kwa yeyote kati yao kukusudia huo usaliti. Kila mmoja alikuwa na wazo la kumwacha Yesu, mara njia yake ikienda chini kwenye kudhihakiwa na kukataliwa. Walijitambua wazi mbele zake, wakaona aibu na bila uwezo wa kukabili jaribu tukufu ndani ya nuru ya Yesu ichunguzayo mioyo.

YOHANA 13:23-30
„Na palikuwapo mmoja wa wanafunzi wake, ameegama kifuani pa Yesu, ambaye Yesu alimpenda. Basi Simoni Petro akampungia mkono, akamwambia, Uliza, ni nani amtajaye? Basi yeye, hali akimwelekea Yesu kifua chake, akamwambia, Bwana, ni nani? Basi Yesu akajibu, Ndiye mtu yule nitakayemtowelea tonge na kumpa. Akatowelea tonge, akalitwaa akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskariote. Na baada ya hilo tonge Shetani alimwingia. Basi Yesu akamwambia, Uyatendayo yatende upesi. Wala hakuna mtu katika wale walioketi chakulani aliyeijua sababu ya kumwambia hivyo. Kwa maana wengine walidhania, kwa kuwa Yuda huchukua mfuko, ya kwamba Yesu alimwambia kama, Nunua mnavyovihitaji kwa sikukuu; au kwamba awape maskini kitu. Basi huyo, akiisha kulipokea lile tonge, akatoka mara hiyo. Nako kulikuwa ni giza la usiku.“

Katikati ya hiyo vurugu lililotokea, kwa sababu ya usaliti kuwa karibu kutokea, bado tunasoma ushuhuda safi ya upole wa upendo. Yohana alikuwa amepumzika kifuani mwa Yesu. Huyu mwinjilisti hataji jina lake mwenyewe hata mara moja ndani ya Injili yake, lakini anataja waziwazi ukaribu wake na Yesu, kama ishara ya upendo. Hakuwa na heshima kubwa zaidi kuliko kupendwa na Yesu. Kwa namna ya ustahi wake anaacha kutaja jina lake, huku akimtukuza Mwana wa Mungu.

Petro alikuwa na aibu, asimwulize Yesu moja kwa moja kuhusu kuthibitisha nafsi ya msaliti, hata hivyo wakati huo hakuweza kujizuia kutafuta jibu. Akampungia mkono Yohana, ili yeye ajaribu kugundua huyu msaliti ni nani. Yohana akamwegemea Yesu na kuuliza, „Ni nani?“

Yesu akajibu swali hilo kimya-kimya, bila kutamka jina la msaliti, lakini kwa ishara ya kimya. Yesu hakupenda kufunua jina la msaliti wazi wakati huo. Maana kulikuwa na nafasi kwa Yuda angesikitikia kusudi lake. Yesu akamega mkate wa neema uliomwunganisha na wanafunzi wake, akachovya kidonge kwenye bakuli na kumpatia Yuda. Kusudi la tendo hilo ilikuwa kumwimarisha mwanafunzi kwa uzima wa milele. Lakini kwa sababu Yuda alikuwa anakusudia kusaliti, kidonge hiki hakikuwa na maana hiyo, bali kilimfanya kuwa mgumu zaidi. Moyo wake ilikuwa imefungwa kwa kupokea neema, na Shetani alimwingilia. Je, si picha ya kutisha hiyo! Kwa mapenzi yake mwenyewe sasa Yesu alimfanya mwenye moyo mgumu kuwa mgumu zaidi. Wakati Yesu alipomtolea Yuda kidonge cha mkate, Shetani alichezea mawazo yake. Baada ya kupokea ule mkate, uovu ulimshukia. Hukumu ya Yesu juu ya msaliti wake ulimwondolea ule ulinzi mtukufu na kumwachilia kwa Shetani.

Mara hii Yuda alijikuta amewekwa wazi wakati wa kupokea kidonge kile. Ndipo agizo la kifalme la Yesu lilimpiga: „Usicheleweshe kutimiza shauri lako ovu, uifanye mara hii, ili kukamilisha mwenendo mbaya huo, maana pengine inaweza kuleta mema badala yake.“

Wanafunzi walishindwa kutambua agizo hilo la Yesu kwa Yuda kwamba awahi. Kawaida angemwagiza kwenda kununua chakula kwa kundi lao. – Yohana hakuweza kabisa kusahau picha hii ya kutisha ya Yuda, alipoondoka kwenye nuru ya kuwepo kwake Yesu na kwenda kwenye giza nene la nje.

YOHANA 13:31-32
„Basi huyo alipokwisha kutoka, Yesu alisema, Sasa ametukuzwa Mwana wa Adamu, naye Mungu ametukuzwa ndani yake. Mungu naye atamtukuza ndani ya nafsi yake; naye atamtukuza mara.

Jinsi gani Yesu alitukuzwa kwa tendo hilo la udanganyifu? Namna gani matunda mema yaweza kutokana na matendo mabaya?

Yesu alihuzunika wakati mwanafunzi wake aliyemchagua, sasa alipomsalita. Alimfuata na mtazamo huo wa upendo, kama labda huyu msaliti wake angerudi. Lakini mwenyewe akakimbilia kwenye baraza la Wayahudi, ambapo waliwapatia silaha hao walinzi, ili wamkamate Yesu wakati wa usiku uo huo.

Krista alishinda jaribu la kishetani kwamba, ajifanye kuwa Masihi wa kisiasa, wakati alipomtuma Yuda kukamilisha ule usaliti. Akachagua kufa kama Mwana Kondoo wa Mungu, ili kukomboa binadamu kwa njia ya unyenyekevu na unyonge, akitangaza kwa njia ya kifo chake kwamba, dhabihu hiyo ya upendo ndiyo asili ya utukufu wake.

Yesu hakutafuta utukufu wa binafsi, bali utukufu wa Baba yake ndani ya kifo chake. Baba yake alikuwa amemtuma ulimwenguni ili awaokoe waliopotea. Mwana alitamani kufanya upya sura ya Baba ndani ya wanadamu walioanguka. Kwa ajili ya kufanya tena upya binadamu, Yesu alimfunua Baba na kuwalisha imani ndani ya wema wa kibaba wa Mungu. Mazoezi peke yao hayatoshi, maana dhambi zimekuwa nyingi sana, hata kuinua kizuizi kati ya Mungu na viumbe vyake. Ilimpasa Mwana afe, ili kizuizi hiki kibomolewe tena, kilichotutenga na Mungu, na mahitaji ya haki yatimie. Kifo cha Yesu ndiyo ufunguo kwa ajili ya kutukuzwa kwa jina la Baba. Bila kifo hiki haiwezekani kuwa na ufahamu wa kweli juu ya Baba, wala kupokelewa kisheria kama watoto wake, wala kufanywa upya kwa kweli.

Wakati Yesu alipojikana mwenyewe, na hivyo kifo chake kuleta utukufu kwa Baba, pia alitangaza kwamba, Baba yake atamimina utukufu wake juu yake, ili naye apate kuwa chemchemi ya vipawa vyote vya utukufu. Katika saa hizo chache kabla ya kukamatwa na kusulibiwa kwake, Yesu aliona kufufuka kwake, kupaa kwake na kuketishwa kwake kwenye kiti cha enzi mbinguni. Ilimpasa Kristo afe, ili aingie katika utukufu wake.

Wote wanaokataa mateso na kifo cha Kristo, au wanaoyaeleza kama dalili za udhaifu, basi wanashindwa kutambua mapenzi ya Mungu yaliyokusanyika ndani ya Msalaba, pamoja na utakatifu wa Mwana, aliyeshinda kufungua kaburi. Alionyesha utukufu wake kwenye madhabahu tukufu, alipoteketea juu yake kwa niaba yetu sisi sote, ili na wote wanaoamini ndani yake wajaliwe haki.

SALA: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, tunakutukuza kwa ajili ya wokovu wako, unyenyekevu na kuteseka, kifo chako na ufufuo. Tunaamini kwamba tumekombolewa na damu ya Kristo. Tunakuhimidi na upewe utukufu katika nguvu ya Roho. Umetuokoa kutoka katika taabu na hatari za maisha. Uhai unaotutolea ni wa milele. Tunaamini kwamba Mwana wako atatokea mapema katika utukufu; Amina

SWALI:

  1. Nini ni maana za utukufu iliyoonyeshwa na Yesu wakati Yuda alipotoka kwake?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on September 01, 2014, at 04:39 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)