Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 082 (The traitor exposed and disconcerted)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 3 - Nuru yang’aa ndani ya shirika la Mitume (Yohana 11:55 - 17:26)
B - Mambo yaliyofuatana na chakula cha Bwana (Ushirika utakatifu) (Yohana 13:1-38)

2. Msaliti anawekwa wazi na kuharakishwa (Yohana 13:18-32)


YOHANA 13:18-19
„Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliyowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aliyekula chakula changu ameniinulia kisingino chake. Tangu sasa nawaambia kabla hayajatukia, ili yatakapotukia mpate kuamini ya kuwa mimi ndiye.“

Yuda aliishi na wasiwasi, bila kupenda unyenyekevu au huduma. Alichagua ukorofi, kuongoza kwa nguvu na udanganyifu. Alitamani kutawala juu ya Yesu kwa hila. Pengine alikuwa na shabaha kulazimisha mkono wa Kristo kutumia nguvu. Hivyo moyoni alikuwa kinyume chake, akitamani kumkanyaga Yesu na kushauri auawe. Alishindwa kutambua ukuu wa upendo uliokuwamo, akawa na kiburi, wakati Yesu alipojinyenyekeza. Yuda alikusudia kuringa, atawale hata kwa kutumia ujeuri, wakati Yesu alichagua kuendelea kwa unyenyekevu na huduma ya upole.

Yesu alikuwa akiwatayarisha wanafunzi wake kwa saa ya kusalitiwa kwake, ili wasipatwe na mashaka juu ya Ubwana wake, hata atakapokabidhiwa kwa watu wa mataifa. Yeye ndiye Bwana binafsi, akishuhudia juu ya saa yake ya unyonge mapema, akijiita mwenyewe „Ndiyo ni mimi“. Kwa maneno kama hayo Mungu alijifunua zamani kwa Musa jangwani katika kijiti kilichowaka moto bila kuteketea. Yesu alihitaji kuwathibitishia wanafunzi wake imani kwa uhakika wa namna hii kuhusu uungu wake, ili wasianguke katika mashaka wala majaribu.

YOHANA 13:20
„Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeaye mtu yeyote nimpelekaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenipeleka.“

Yesu aliwaweka huru wanafunzi wake toka kwa hofu kwa sababu ya kukamatwa na kuuawa kwake. Utume wake kwao pamoja na ulinzi wake utawafunika. Yesu anapowatuma wafuasi wake anaenda pamoja nao. Watumishi wake hawaendi katika jina lao wao wenyewe, bali katika jina lake Bwana aliyeinuliwa sana. Yeyote atakayewapokea, anapokea Utatu Utakatifu. Naye atakayeamini maneno yao, atakuwa mtoto wa Mungu. Utume huu ni ngumu hasa: Inatakiwa kujikinahi na kuwapenda maadui, pamoja na kuvumilia umaskini na dharau. Lakini mbali na hayo wanajua kwamba Mungu anatawala ndani yao. Popote waendapo Yesu anaenda nao, na kokote anapowataka watumike, Roho yake atawaelekeza kwa shabaha zake, ili malengo yake yapate kukamilika.

SALA: Bwana Yesu Kristo, nisaidie nitambue kwamba siwezi kudumu ndani yako, nisipojikabidhi kwako kuwa mtumishi wako. Napenda nione daima wewe kuwa mfano kwa maisha yangu, niendelee kuwa mnyenyekevu katika mikutano yetu na niwe mtumishi kwa familia zetu. Nisitoe nafasi kwa Shetani ndani ya moyo wangu. Nisaidie nisiseme tu habari ya kuhudumia, lakini nitende mwenyewe katika nguvu na hekima yako.

SWALI:

  1. Tunajifunza nini kutokana na mfano wa Kristo?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on September 01, 2014, at 04:37 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)