Previous Lesson -- Next Lesson
1. Yesu kupakwa mafuta Bethania (Yohana 11:55 - 12:8)
YOHANA 11:55-57
“Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; na wengi wakakwea toka mashambani kwenda Yerusalemu kabla ya Pasaka, ili wajitakase. Basi wao wakamtafuta Yesu, wakasemezana hali wamesimama hekaluni, Mwaonaje? Haji kabisa sikukuu hii? Na wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikuwa wametoa amri ya kwamba mtu akijua alipo, alete habari, ili wapate kumkamata.”
Pasaka ilikuwa ndiyo sikukuu ya kwanza katika Agano la Kale, ikiadhimisha kuokolewa kwa Waebrania kutoka kwa ghadhabu ya Mungu. Hivyo, waliishi chini ya ulinzi wa Mwana Kondoo wa Mungu aliyotayarishwa kwa ajiöli yao. Walistahili kufa, lakini imani iliwaokoa.
Kila mwaka Wayahudi walikuwa wakitembelea Yerusalemu, ili wamshukuru Mungu kwa kuwalinda na ghadhabu yake. Hapo walikuwa wakichinja maelfu ya kondoo kwa sadaka na kula. Wengi wao walizoea kukwea Yerusalemu mapema, ili wajitakase kwa kuungama ndipo kuwa tayari kwa kujifunganisha na Kondoo wa Mungu. Ikiwa mtu aliwahi kugusa maiti, alitakiwa kushika mfululizo wa kujitakasa kwa siku saba, ili astahili tena kuingia ndani ya hekalu la Mungu (Hesabu 19:11)
Kwa majira haya wahiji wakaanza kumwulizia Yesu, Mnazarene, “Atakuja au hawatamwona kabisa?” Maana yake wote walijua kwamba, Baraza la kidini kwa siri walikuwa wameamua kumhukumu kufa. Walikuwa wamewaagiza wengi katika taifa nzima wamchunguze Yesu, na wawajulishe kama wamemwona mahali Fulani, ili akamatwe. Utaya wa mauti ilikuwa wazi, ili kummeza Yesu.
YOHANA 12:1-3
“Basi siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alifika Bethania, alipokuwapo Lazaro, yeye ambaye Yesu alimfufua katika wafu. Basi wakamwandalia karamu huko; naye Martha akatumikia; na Lazaro alikuwa mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye. Basi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya nardo safi yenye thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya marhamu.”
Yesu hakuwa na hofu na ujanja wa maadui zake, bali aliendelea kwenye jia yake kuelekea Yerusalemu, sawasawana mapenzi ya Baba yake. Hakutafuta upweke tena, lakini alirejea Yerusalemu wiki moja kabla ya sikukuu. Akapitia Bethania, kilomita tatu kabla ya Mji Mkuu. Akafikia nyumbani alipoonyesha enzi yake na kumtukuza Baba yake kwa kushinda kifo. Lazaro aliishi na kuendelea kula, lunywa na kutembelea sokoni. Watu wakamwona kwa kushangaa, hata hivyo wenye hofu kwa kutazama kifo na pia kumtazama aliyefufuka kama sio ya kweli.
Mariamu, Martha na Lazaro wenyewe walipata kutambua utukufu wa Mungu, wakashuhudia hayo, ingawa kulikuwa na matisho ya baraza. Lazaro alimkaribisha Yesu na wanafunzi wake na kuwafanyia karamu kwa furaha kuu. Alikuwa rafiki wa Yesu wa karibu, akaketi upande wake YEYE aliyemfufua toka kifoni. Je, picha hii haituonyeshi mambo yatakavyokuwa kwenye paradiso? Mungu hatakuwa mbali, lakini tutaketi naye katika utukufu.
Martha, mwenye juhudi wa kushughulikia mambo ya nyumbani, alifungua hazina ya nyumba yao, akitoa yale aliyokuwa nayo, kwa kutambua kwamba Yesu ndiye Masihi wa kweli, pia na mshindi juu ya mauti.
Mariamu, mwenye kutafakari zaidi mambo ya ndani, alimheshimu Yesu kwa namna yake, akitoa chupa chenye marhamu safi ya thamani kubwa ya kulingana na mshahara wa mfanya kazi kwa mwaka mzima. Alitamani kumtolea Yesu kile alichokithamini sana. Lakini alijisikia hastahili kupaka kichwa chake; badala yake alipaka miguu yake kwa uthamani wa maisha yake. Upendo sio hafifu, tena inajitoa kikamilifu. Baada ya hapo alipangusa miguu yake na nwele zake. Tendo hilo la upendo, kwa moyo mweupe na takatifu, lilijaza nyumba yote na harufu safi ya marhamu. Wote waliokuwapo nao walijazwa na marashi ya sadaka ya Mariamu.
YOHANA 12:4-6
“Basi Yuda Iskariote, mmojawapo wa wanafunzi wake, ambaye ndiye atakaye kumsaliti, akasema, Mbona marhamu hii haikuuzwa kwa dinari mia tatu, wakapewa maskini? Naye alisema hayo, si kwa kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwivi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo.”
Yuda alipenda pesa zaidi kuliko kumpenda Yesu, akipendelea vya thamani kuliko imani ya kweli. Basi alijaribu kueleza sadaka hii kwa namna ya fedha taslimu, bila kujali baraka za kiroho iliyoenda pamoja nayo. Alishindwa kutambua maana ya adhimisho la Mariamu, kushukuru kwake na kujitoa kwake Kristo. Yeyote apendaye pesa atakuwa shetani. Kiajabu, alificha chuki yake kwa Yesu kwa utawa wa uongo, kana kwamba alikusudia tendo la huruma kwa kuwasaidia maskini. Kwa kweli hakusikia huruma kwa ajili yao, wala kutaka kuwatolea kitu, badala yake alitamani kujipatia fedha kwa ajili yake mwenyewe. Namna ya utoaji kwake ilikuwa ni funiko la kufaulu kuiba, akibakiza mfukoni mwake zaidi kuliko kuwapa maskini. Kutokuwa mwaminifu katika vitu vidogo kunamfanya mtu kuwa mwizi kwa kukusudia na katika mawazo.
Yesu hakukagua hesabu za mtunza fedha wake, lakini alimvumilia hadi mwisho, ingawa alifahamu habari ya udanganyifu wake na matendo yake mabaya. Yuda alikuwa ni mwizi na mdanganyi, akijipenda mwenyewe na kuelekea kwenye ushawishi wa utajiri, akawa mtumwa wa hayo. - Ndugu, huwezi kumtumikia Mungu na pesa. Utapenda kimoja na kuchukia kingine. Usijidanganye mwenyewe. Je, Mungu ndiye lengo lako, au ni maisha ya raha?
YOHANA 12:7-8
“Basi Yesu alisema, Mwache aiweke kwa siku ya maziko yangu. Kwa maana maskini mnao sikuzote pamoja nanyi; bali mimi hamnami sikuzote.”
Mungu hatuhitaji tufanye mambo ya kiajabu, kama vile kumwaga machupa ya manukato kwenye miguu yetu sisi kwa sisi, lakini kwa uwazi kuangalia na kushughulikia mahitaji ya maskini wanaotuzunguka. Hakuna chama, dini wala shirika la msimamo fulani inayoweza kufuta tamko la Yesu kwamba, maskini watakuwa nasi wakati wo wote. Kujipendelea wenyewe ni pana, upendo wetu mara nyingi ni nyepesi. Haiwezekani hapo duniani kuwa na namna ya kushirikiana mambo yote kwa roho ya kidini; wala hatutalingana wote kwa uwezo, utajiri na heshima. Daima tutawakuta fukara, wanaokataliwa au kutengwa kote tuendako, mashariki au magharibi. Kwenye mji yoyote au kijijini wewe uwatafute maskini ukiwasaidia, na ndani yao utaona uso wa Yesu.
Yesu alielewa kwamba mioyo ya watu ni migumu kama jiwe na baridi ya kuganda. Yeye amekuja na joto la upendo wake ili awafie wote. Pamoja na hayo alifahamu kwamba Roho Mtakatifu alimwongoza Mariamu afute miguu yake na kuyapaka mafuta kwa ajili ya mazishi yake. Kama upendo tukufu inawaingilia watu, Roho Mtakatifu itawaongoza kwa mambo ya ajabu ambayo hayakutazamiwa nao. Mariamu alikusudia kumtukuza huyu mgeni wa kimungu, hivyo Roho akamwongoza kumpaka mafuta kabla ya wakati wake. Basi, hapo Kristo anaanza kutengeneza upatanisho wa dunia hii ovu na Mungu wa rehema na neema.
SALA: Bwana Yesu, tunakupenda kwa kumfufua Lazaro. Hukuwa na hofu kwa kaburi ya huzuni. Utufundishe kutoa mioyo yetu na hazina zetu kwa kukutumikia kwa moyo wote na chochote tulicho nacho. Utuweke huru na unyonge, unafiki, uwizi na chuki. Tujaze na upendo wako, na utuongoze kwenye njia ya kujitoa kweli kwa shukrani.
SWALI:
- Kwa nini Yesu alikubali kupakwa mafuta na Mariamu?