Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 072 (Jesus meets Martha and Mary)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
C - Safari ya mwisho ya Yesu kwenda Yerusalemu (Yohana 7:1 - 11:54) Neno Kuu: Kutenganisha giza na nuru
4. Kumfufua Lazaro na matokeo yake (Yohana 10:40 - 11:54)

b) Yesu akutana na Martha na Mariamu (Yohana 11:17-33)


YOHANA 11:17-19
“Basi Yesu alipofika, alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne. Na Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu, kadiri ya maili mbili hivi; na watu wengi katika Wayahudi walikuwa wamekuja kwa Martha na Mariamu, ili kuwafariji kwa habari ya ndugu yao.”

Siku nne zilikuwa zimeisha kupita tangu Lazaro amelazwa kaburini; alikuwa amezikwa siku alipofariki, na habari hiyo ilimfikia Yesu siku hiyo. Hapakuwa na sababu kwa Yesu afike haraka, maana rafiki yake tayari amezikwa. Kifo ilikuwa imekwisha kuthibitishwa pasipo shaka lolote.

Bethania ilikuwa mashariki wa mlima wa mizeituni kuangalia bonde la Yordani, meta 1.000 chini ya hapo. Mbele zaidi ilionekana Bahari ya Chumvi. Upande wa magharibi kwa umbali wa kilometa tatu Yerusalem ilionekana ng’ambo ya bonde la Kidroni.

Marafiki wengi wa huyu aliyepigwa na ugonjwa walikusanyika nyumbani kwake wakilia na kuvipiga vifua vyao. Huzuni kuu ilionekana wazi, kwa vile Lazaro alikuwa ni wa kuleta mapato yake kwa ajili ya kutunza familia. Uvuli wa mauti uliwafunika waliokutanika.

YOHANA 11:20-24
“Basi Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alikwenda kumlaki; na Mariamu alikuwa akikaa nyumbani. Basi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. Lakini hata sasa najua ya kuwa yo yote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa. Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka. Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho.”

Martha aliposikia kwambaYesu amekaribia, akakimbilia kwake akilalamika; huku akiwaza ndani yake, kama yeye angalifika mapema, jinamizi hiyo isingalitupiga. Hata hivyo alithibitisha imani yake wakati walipokutana, akitegemea kabisa enzi yake isiyokoma. Hakupoteza muda wa kueleza huzuni zake, bali alitaja tumaini lake kwamba yeye angeweza kuzuia kifo; hakujua ni namna gani, lakini aliamini uhakika wa enzi yake, na kwamba ameunganika na Mungu, ambaye angejibu sala ya Mwana wake wakati wowote.

Mara moja Yesu aliitikia juu ya imani yake kwa ahadi nzito sana: “Ndugu yako atafufuka”. Hakuelewa kwa ndani sana kiini cha maneno yake, lakini aliyachukua kuwa ahadi kwake kwa ajili ya ufufuo ule wa mwisho. Hapo amepata tumaini, akitambua kwamba, kifo bado si mwisho. Ufufuo kwa uzima wa melele ndiyo tumaini la waumini.

YOHANA 1:25-27
“Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Unayasadiki hayo? Akamwambia, Naam Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni.”

Mbele ya masikio ya wanafunzi wake Yesu alimwambia Martha tamko hilo zito, “Uhakika ufufuo utakuja, tena upo hapa kwa namna ya nafsi yangu (au ndani yangu). Si kwamba atafufuliwa baadaye siku ya ufufuo, bali atafufuka leo kwa kuwepo kwangu. Mimi ndimi Mwumbaji; toka kwangu hutokea Roho Mtakatifu kwenda kwenu. Mimi nitakufa kwa niaba yenu na kuondoa dhambi zenu, ili niwahakikishie uzima tukufu. Mauti haitaweza kutawala juu yenu. Mapema nitathibitisha ufufuo wenu kwa njia ya ufufuo wangu. Ili hata ninyi mkazikwe na kufufuka tena pamoja nami kwa imani. Kifo changu ni chenu, uzima wangu ni wenu. Mimi naishi na ninyi mtaishi ndani yangu.”

Sharti ni moja tu kwa kupokea uzima wa Kristo ni agano la imani pamoja na Yesu. Namna na desturi za uzima wake hayatatoka kwake na kuja kwako, isipokuwa wewe umeunganika naye kwa agano hilo. Imani yetu ndani ya Kristo inatufungulia ufahamu kumhusu Baba na uzima wa milele. – Upendo wake unapanda furaha, amani na upendo ndani yetu ambazo hazipungui daima wala kukoma. Mtu aliyejazwa upendo wa Kristo hatakufa, kwa sababu Roho wa Mungu ni wa kudumu daima. Roho huyu hutawala mioyo ya wale wanaomwamini Kristo.

Yesu hakufanya hotuba ya kugusa, kwa ajili ya kutangaza ushindi wake juu ya kifo, wakati wa kumfufua Lazaro. Aliwahakikishia wale waliokuwa wa hai kiroho, kwamba kifo haitakuwa na uwezo juu yao, kwa vile wamekwisha kushiriki tayari katika ufufuo wake. - Je, umewahi kutambua uwezo wa ahadi toka mdomoni mwake zisizo na sharti? Ikiwa unaamini ndani yake, na wewe hutakufa. Usiwaze-waze juu ya kifo chako kitakachokuja lazima, wala si juu ya kaburi wazi; badala yake geuzia macho yako kwake Yesu. Mshukuru kwa sababu ya kujitoa kwa ajili yako kabisa, maana atakusimamisha ndani ya uzima wa milele.

Mpendwa Ndugu, unaamini ndani ya Yesu aliye mtoa-uzima? Umepata kuonja mwenyewe kwamba, amekuweka huru na utawala wa mauti, na kukunyofoa kutoka katika uchafu wa dhambi? Kama hujapata kuonja ufufuo huo wa kiroho, twakuhakikishia kwamba, Bwana wa uzima asimama mbele yako akikunyoshea mkono wake uishike. Amini ndani ya upendo na nguvu yake. Kamata kabisa mkono wake, naye atakuinua kutoka kwa dhambi zako, na kukupeleka kwenye uzima wa milele. Yeye pekee ndiye Mwokozi wako mwaminifu.

Martha alikubali ahadi ya Kristo. Yeye hakuonja tu uzima wa milele, lakini alimwona Mtoa-uzima mwenyewe. Aliamini kwamba Yesu ndiye Masihi aliyeahidiwa, aliye hata na uwezo wa kufufua wafu. Yeye naye ni mwenye enzi ya kusimamia hukumu ya mwisho. Martha alionja nguvu yake ikimiminwa ndani yake, kwa kumwamsha na kumtakasa. Alikuwa na ujasiri kutamka wazi ushuhuda wa imani yake hapo njiani, ingawa alifahamu uamuzi wa Wayahudi kumpiga Yesu kwa mawe afe, kwa ajili ya kueleza kwamba ndiye Mwana wa Mungu. Martha hakuhofia kifo, bali kumpenda sana Mwokozi wake. – Mwanamke ambaye ushujaa wake unawafanya wanaume waaibike. Tumaini lake lilikua linaimarika pamoja na upendo wake.

SALA: Bwana Yesu, wewe daima ni mkuu. Kifo haikuwa na uwezo juu yako. Wewe ulifia kifo chetu, pia na kutufufua kwa njia ya ufufuo wako. Tunakuabudu na kukushukuru. Umeshirikisha maisha yako na sisi, ili hata kifo kisipate tena kutawala juu yetu. Tunakupenda na kukushukuru kutuweka huru na hatia, hofu na mauti.

SWALI:

  1. Jinsi gani sisi tunafufuka toka kifoni siku hizi?

YOHANA 11:28-31
“Naye alipokwisha kusema hayo, alikwenda zake; akamwita umbu lake Mariamu faraghani, akisema, Mwalimu yupo anakuita. Naye aliposikia, aliondoka upesi, akamwendea. Na Yesu alikuwa hajafika ndani ya kijiji; lakini alikuwa akalipo pale pale alipomlaki Martha. Basi wale Wayahudi waliokuwapo na Mariamu nyumbani, wakimfariji, walipomwona jinsi alivyoondoka upesi na kutoka, walimfuata; huku wakidhania ya kuwa anakwenda kaburini ili alie huko.”

Labda Yesu alimtaka Martha kumleta Mariamu kwake, ili naye asikie toka kwake maneno ya tumaini na faraja, mbali na umati wa waombolezaji. Kwa njia hiyo angeendelea kiimani na kwa upendo wake. Yesu hushinda kwa ujasiri wa imani, sio kwa kuangalia mazito tu na huzuni. Alitamani kumleta Mariamu aliyehuzunika kwenye nuru ya kuwapo kwa Mungu, ili apumue na aishi tena kwa tumaini na kuchangamka kiroho.

Pengine Mariamu alikuwa hajasikia habari ya kufika kwake Yesu kwa hali yake ya kuzama ndani ya huzuni. Basi, Martha aliporudi kwake nyumbani na kumweleza kwamba, Yesu anamwulizia, aliinuka kwa kuchangamka, ili akutane na Bwana. Hivyo wale waliokuwa naye walishituka walipoona anainuka haraka hivyo, wakiulizana kama anaenda kabirini alie machozi pale. Wote wakainuka na kumfuata kaburini - mfano wa maisha ya kibinadamu unaotuonyesha jinsi wanavyofuatana kwenda kupotea milele, wakimezwa na taabu na giza. Wakati filosofia na taratibu za dini haziwezi kuleta jibu kamili kwa matatizo ya maisha hata kifo, iwapo kifoni ukweli wa tumaini ya kikiristo itapata kuonekana wazi pamoja na faraja yake imara.

YOHANA 11:32-33
“Basi Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake;”

Mariamu akamwona Yesu, kwa kuvutwa na konyezo akajitupa miguuni pake, akivunjika kiroho. Akakiri imani yake hivi kifudifudi, akitumaini kwamba ataweza kutenda mwujiza wa kimungu. Ila, angalikuwapo tu mapema, kaka yake asingalikufa. Hayo yalielekeza kwa imani imara iliyoonekana nyumbani kwao, na ya kwamba Mungu alikuwapo ndani ya Yesu. Hata hivyo kifo ilitikisa imani hiyo na kuwaacha wadada hao katika hali ya kufadhaika.

Yesu alipoona imani hiyo yenye hofu ndani ya wafuasi wake waaminifu, tena pamoja na kutokutambua kwa umati, basi akahangaika rohoni. Alitambua jinsi wote walivyoshindwa na uwezo wa mauti. Alihuzunika kwa kuona walivyolia machozi, akatambua kwamba ulimwengu umefungwa na enzi ya uovu. Tena akasikia uzito wa dhambi za ulimwengu ukimkandamiza mabegani mwake; Rohoni mwake akaona ulazima wa msalaba, na kaburi tupu kuwa ndiyo njia ya pekee kushinda huzuni ya namna hii. Alikuwa na uhakika ya ufufuo uliokuwa karibu kutukia. - Hii ndiyo hukumu halisi ya kifo, kutokuamini na taabu.

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 18, 2014, at 11:38 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)