Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 073 (The raising of Lazarus)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
C - Safari ya mwisho ya Yesu kwenda Yerusalemu (Yohana 7:1 - 11:54) Neno Kuu: Kutenganisha giza na nuru
4. Kumfufua Lazaro na matokeo yake (Yohana 10:40 - 11:54)

c) Kumfufua Lazaro (Yohana 11:34-44)


YOHANA 11:34-35
“Akasema,Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo utazame. Yesu akalia machozi.”

Yesu hakujibu kwa maneno. Kuzungumza na mtu anayehuzunika sana haifai. Mahali hapa matendo yalifaa zaidi ya maneno. Aliwataka waliokuwa karibu wampeleke kwenye kaburi. Wakamwambia, “Njoo ukaone”. Hayo yalikuwa ni maneno yale yale aliyotumia Yesu alipowaita wanafunzi wake mwanzo wa huduma yake. Aliwaita ili waone uhai; hao watu walimwita ili aone mauti. Basi akalia kwa kuona uchelevu wa kutambua, ujinga na kutokuamini kwao. Hata wale bora katika wafuasi wake hawakuweza kuonyesha imani kweli. Mwili haufai na roho unapungua imani. Roho Mtakatifu alikuwa hajamiminiwa juu yao bado. Kifo cha kiroho kilitawala, na Mwana wa Mungu aliweza kulia tu juu ya hali dhaifu ya wanadamu.

Yesu alikuwa ni Mwanadamu kamili, akifurahi pamoja nao waliofurahi na kulia na wale waliolia. Roho yake ilifadhaika. Usikivu wa utu wake wa ndani uliguswa sana kwa kuona shida ya kifo upande wa wafuasi wake na upungufu wao wa upendo kwa Mungu aliye hai. - Yesu hata leo analia machozi juu ya hali ya makanisa yetu, pia na juu yetu sisi na wote wanaonang’ania dhambi na hali ya kifo cha rohoni.

YOHANA 11:36-38a
“Basi Wayahudi wakasema, Angalieni jinsi alivyompenda. Bali wengine wao wakasema, Je, Huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife? Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake ...“

Wayahudi waliona majonsi ya Yesu, wakaeleza sababu zake kuwa ni upendo wake kwa Lazaro. Upendo sio baridi kimawazo tu au kiakili, lakini inawasiliana na namna ya wanavyojisikia wengine nafsini mwao. Upendo wa Kristo unazidi sana uwezo wa ufahamu wetu na kuendelea hata ng’ambo ya kifo. Alimwona Lazaro ndani ya kaburi lake lililofungwa kabisa, akahuzunika kwa ushindi wa mauti juu ya rafiki yake. Lakini moyo wake ulikata-kata jiwe la kizuizi na kutayarisha maiti kusikia wito wake.

Baadhi ya wenyeji waliokuwepo walimlaumu Yesu kwa namna yake ya unyofu na wakajadiliana juu ya uweza wake. Kwa hayo Yesu alikasirika. Maana upungufu wa imani na upendo na udogo wa tumaini hutokeza ghadhabu ya Mungu. Yesu alikusudia wokovu wetu kutoka gizani, tena kutuokoa na namna yetu ya utambuzi kuwa finyo, ili tuweze kushikamana na upendo wake, na kuisha kwa imani yake na kutulia katika uhakika wa tumaini lake, wala tusirudi tena kwenye namna ya kawaida ya kibinadamu, na hivyo kuimarika katika kutegemea enzi yake. Yeye anatamani kuwainua wale waliokufa dhambini mwa mazingira yao. - Je, Yesu anasikia kuvurugwa kwa kutokuamini kwako, au anafurahia upendo wako wenye juhudi?

SALA: Nisameha, Bwana Yesu, kwa kupuuza nafasi nyingi katika kutumaini na kupenda. Unisamehe na upungufu wa imani na uwe radhi kwa kujiangalia binafsi tu. Unihimize niwe na tumaini hai, ili nikuheshimu na kunielekeza kwako wakati wowote.

SWALI:

  1. Kwa nini Yesu alifadhaika na kwa nini alilia machozi?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 18, 2014, at 11:39 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)