Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 064 (The Jews interrogate the healed man)
This page in: -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
C - Safari ya mwisho ya Yesu kwenda Yerusalemu (Yohana 7:1 - 11:54) Neno Kuu: Kutenganisha giza na nuru
2. Kumponya mtu aliyezaliwa kipofu (Yohana 9:1-41)

b) Wayahudi wanamhoji yule aliyeponywa (Yohana 9:13-34)


YOHANA 9:24-25
“Basi mara ya pili wakamwita yule mtu aliyekuwa kipofu, wakamwambia, Mpe Mungu utukufu. Sisi tunajua ya kuwa mtu huyo ni mwenye dhambi. Basi yule mtu akajibu, Kwamba yeye ni mwenye dhambi sijui. Najua neno moja, kuwa mimi nalikuwa kipofu na sasa naona.”

Mafarisayo walijaribu kwa nguvu kupata jambo la tatizo ndani ya Yesu, ili wawe na sababu ya kumhukumu. Wakamleta tena yule aliyeponywa mbele zao, wakamfanya aape na kusema kinyume cha Yesu kwa kumshitaki kwa kosa fulani. Kama wajuzi wa sheria walitetea kwamba walimgundua Yesu kuwa mwenye dhambi; walilohitaji ilikuwa ni thibitisho la wazi. Walitumia mkazo kwake, akubali maoni yao na kumshitaki Yesu, wakipendelea akiri kwamba, kuponywa kwake haikuwa kwa utukufu wa yule Mnazarene. Lakini alijibu kwa hekima, “Mimi sijui kama yeye ni mwenye dhambi, Mungu ajua. Mimi najua jambo moja - nilikuwa kipofu na sasa naona.” Jambo hilo haliwezi kukataliwa. Linamaanisha mwujiza, enzi tukufu iliyotenda kazi, na kwake rehema na msamaha. Ushuhuda wa huyu kijana ni mfano wa maelfu wa waumini watakaothibitisha. Pengine hawajui siri za mbinguni na kuzimuni, lakini ni watu waliopokea hali ya kuzaliwa mara ya pili. Kila mmoja wao aweza kuthibitisha, “Nilikuwa kipofu na sasa naona.” (Mimi mtafsiri kwa kiswahili ni mmojawao).

YOHANA 9:26-27
“Basi wakamwambia, Alikutendea nini? Alikufumbua macho jinsi gani? Akawajibu, nimekwisha kuwaambia, wala hamkusikia; mbona mnataka kusikia tena? Ninyi nanyi mnataka kuwa wanafunzi wake?“

Bila kuridhika na majibu ya yule kijana, Mafarisayo walijaribu kupata maneno yanayopingana ndani ya maelezó yake, wakamtaka arudie habari zake tena. Akakasirika na kusema, “Hamkuelewa mara ya kwanza? Mnapenda kusikia taarifa yangu tena, ili nanyi mate kuwa wanafunzi wake?”

YOHANA 9:28-34
“Basi wakamshutumu wakasema, Wewe u mwanafunzi wake yule; sisi tu wanafunzi wa Musa. Sisi tunajua ya kuwa Mungu alisema na Musa; bali yule hatujui atokako. Yule mtu akajibu, akawaambia, Hii ni ajabu! Kwamba ninyi hamjui atokako, naye alinifumbua macho! Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo. Tokea hapa haijasikiwa ya kuwa mtu ameyafumbua macho ya kipofu, ambaye amezaliwa hali hiyo. Kama huyo asingalitoka kwa Mungu asingeweza kutenda neno lo lote. Wakajibu, wakamwambia, Ama, wewe ulizaliwa katika dhambi tupu, nawe unatufundisha sisi? Wakamtoa nje.”

Baada ya yule kijana kuwadhihaki Waandishi na wasomi, wakalia na kumshutumu wakisema, “Sio sisi, bali ni mwanafunzi wa yule mdanganyi. Sisi twamfuata Musa, mtu aliyesema na Mungu.” Yesu kabla ya hapo alikuwa amewajulisha kwamba, kama wangemfahamu Musa kweli, wangesikiliza maneno yake na kumwelewa. Lakini tangu walipopinda maneno ya Musa na kuyatumia ili kujisafisha wao wenyewe, hawakuweza kumwelewa na yeye, wala kuweza kumtambua Roho, ambaye alisema kwa nguvu yake.

Na hapo yule mponywa akaitika, “Mwenye kufumbua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu, anayo uwezo wa uumbaji. Ni mwenye Enzi na anaweza. Katika rehema zake hakuniaibisha mimi; hakuhitaji fedha, ila akanitolea huduma ya upendo bure. Wala hakuningojea nimshukuru. Sikuona upungufu au lawama ndani yake.”

Ndipo yule kijana akakiri; “Kila mshiriki wa Agano la Kale afahamu kwamba Mungu hataitika kwa sala za wenye kiburi. Dhambi ndani ya mtu huzuia mtiririko wa baraka toka kwa Mungu. Lakini mwenye kuvunjika kiroho mbele ya huyu Mtakatifu, akitubu dhambi, kutafuta imani na upendo kwa shukrani, kwake huyu Mungu binafsi atasema.”

“Hata mmojawenu asingeweza kufumbua macho yangu, hakuna mtu awezaye hilo, kwa sababu wote wametenda dhambi, isipokuwa Yesu tu. Yeye aliweza kuniponya, thibitisho kwamba yeye hana dhambi. Mungu aishi ndani yake.” Jinsi alivyolazimisha kutafakari habari ya Yesu wakati wa kuhojiwa, alipata kumtambua Yesu zaidi katika usafi na uungu wake.

Hapo basi, hao waliojiona katika haki yao wenyewe na kujijua kuwa wacha Mungu, wakamlaani wakisema, “Hakuna aliyepevusha zaidi ya wewe, hata na wazazi wako nao wako hivyo. Upungufu wako unajionyesha katika upofu wako.” Hao wachaji hawakutambua kwamba walikuwa vipofu kuliko huyu maskini. Yesu alimtumia kama mtume kwao kwa niaba yake, ili kuwaonyesha mambo, ambayo angeweza kuwatendea hata wao. Lakini walikataa mafundisho ya Kristo aliyowapa kwa ushuhuda wa mtume wake, yule aliyeponywa. nBasi wakamtupa nje ya sinagogi kwa nguvu. Vurugu hilo lilianzia ndani ya chumba cha baraza, ndipo nje mbele za watu, walipomwita mtumishi wa Yesu. Basi yeye siku ile alikuwa mponywa, na hata hivyo mkataliwa na taifa lake, hakikisho kwamba roho zao zilishindwa kuvumilia Roho ya Kristo.

SWALI:

  1. Jambo gani huyu kijana alifaulu kutambua polepole wakati alipohojiwa?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 18, 2014, at 11:24 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)