Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 065 (Jesus reveals himself to the healed one)
This page in: -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
C - Safari ya mwisho ya Yesu kwenda Yerusalemu (Yohana 7:1 - 11:54) Neno Kuu: Kutenganisha giza na nuru
2. Kumponya mtu aliyezaliwa kipofu (Yohana 9:1-41)

c) Yesu ajifunua kuwa Mwana wa Mungu kwa yule mponywa (Yohana 9:35-41)


YOHANA 9:35-38
“Yesu alisikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu? Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini? Yesu akamwambia, Umemwona, naye anayesema nawe ndiye. Akasema, Naamini Bwana. Akamsujudia.”

Sasa tumesoma habari hii ya kutia moyo. Yesu aliposikia habari ya mponywa kutupwa nje, alimtafuta na kumpata katika hali ya kutaabika. - Basi hii ndiyo faraja inayopatikana kwa kila aaminiye, aliyewahi kutengwa na familia au marafiki kwa ajili ya kumwamini Kristo. Kama wewe umo katika hali hii, twakuhakikishia kwamba Yesu asikia kilio chako, naye atakujia mwenyewe, wala hatakuacha na upweke. Usiwaangalie watu, maana utatiwa huzuni. Umtazame Yesu peke yake. Usitegemee tumaini lolote hapo duniani au mbinguni ila ndani ya YEYE tu. Yeye anakupenda.

Ndipo Yesu akamwuliza yule kijana swali muhimu la ndani hasa: “Wewe wamwamini Mwana wa Mungu, ambaye naye ni Mwanadamu?” Hii inaonyesha kwamba Yesu alielewa habari ya uzoefu wa huyu kijana na maandiko ya Agano la Kale, akafahamu na kitabu cha Danieli 7:13-14 kwamba, yule Mwanadamu Mahidiwa ndiye hakimu wa ulimwengu pia naye ni Mwana wa Mungu. Yesu aliuliza hayo, ili apate kutambua kama huyu kijana alitamani kukubali enzi ya Mwana wa Mungu kwa wakati ule na daima, na asipate kurudi nyuma. Aliwaki kutambua kwamba Yesu hakuwa mtu wa kawaida tu akamtaja kuwa “Bwana”. Hata hivyo alipenda kujua zaidi huyu Mwana wa Mungu ni nani, ili asije kumsujududia mtu wa kawaida tu - ambalo lingekuwa kuabudu sanamu.

Hapo Yesu alimpatia jibu la kupendeza sana, “Ulimwona kwa imani mapema, kabla ya kumwona kwa macho. Mimi ndimi, Mwana wa Mungu anayesema nawe.” Hapo huyu kijana hakuweza kungoja ila kujitoa kabisa kwake Yesu. Akainama mbele yake, kana kwamba aseme: “Bwana, mimi ni wako na wewe ni mfalme wangu, mwalimu wangu na Bwana. Wewe ndiwe Upendo mwilini, najikabidhi kwako kwa nafsi yangu yote, niwe mtumwa wako kuanzia leo” - Ndugu, umewahi kumtambua Yesu, Mwana wa Mungu, aliye na Mwanadamu? Umejiunga naye kuwa mwumini wake? Unamwabudu kama mtumwa aliyefungamana naye daima?

YOHANA 9:39-41
“Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu. Baadhi ya Mafarisayo waliokuwapo pamoja naye wakasikia hayo, wakamwambia, Je, sisi nasi tu vipofu? Yesu akawaambia, Kama mgekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa.”

Wakati ule yule kijana alipoinama mbele za Yesu hakumzuilia kufanya hivyo, maana Yesu anastahili heshima yote. Lakini Yesu alisema kwamba, kuja kwake kutaleta hukumu kwa wenye kiburi, na kwa wacha Mungu waliojiona kuwa wenye kujitoa, lakini bila kutambua habari ya ukweli. Vipofu na wenye dhambi ndiyo wale waliotambua hayo na kutubu, hata wazinzi walipata kutakaswa. Yesu hakuhukumu wale ambao hawakutubu; walijihukumu wenyewe kwa kukatalia wokovu wake. Waliwahi kupokea nuru fulani hapo zamani, wakati wa manabii na kwa mafundisho ya Maandiko Matakatifu. Lakini wakiwa kinyume cha mahubiri ya Yesu kwa kusudi, watapinga na mengine yote ya mwangaza uliopatikana naye. Watakuwa vipofu, wenye mioyo migumu, wakaidi na wauaji wenye chuki. Kuja kwake Kristo na mahubiri yake yatakuwa na matokeo mawili: Wokovu au kuangamizwa - baraka au laana. Kuna tokeo gani moyoni mwako?

Katika wasikilizaji wake Kristo walikuwemo Mafarisayo, waliojisikia kwamba Yesu anawamaanisha wao kwa maneno yake. Wakauliza, “Je,sisi tu vipofu?” Yesu alichoma unafiki wao akisema, “Ikiwa ninyi kweli mlijiona wenyewe kuwa vipofu na kuhuzunika kwa ajili ya hali yenu ya kiroho, mgalitubu makosa yenu mbele ya Yohana Mbatizaji, na kuachana na makosa yenu; hapo mgalipokea msamaha na kubarikiwa . Lakini mnajidanganya wenyewe, na mnadai kufahamu mambo yote, mkijifikiria kuwa wenye hake. Ila kwa kujisifu hivyo, mwathibitisha upofu na ugumu wenu. Hamtapata hata mwali moja ya mwangaza kutoka kwake aliye Nuru ya ulimwengu.”

SALA: Bwana Yesu, wewe ndiwe Mwana wa Mungu ndani ya namna ya mwanadamu. Tunakuabudu na kujitoa kwako sasa na kwa wakati wote. Tuko tayari kwa ajili yako kwa uwezo wetu pia na mali yetu. Tunakusihi utusamehe na kutakasa mioyo yetu, ili dhambi lolote, hata liwe dogo namna gani, lisitutenge na wewe.

SWALI:

  1. Kuinama chini mbele ya Yesu kunaonyesha nini?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 18, 2014, at 11:28 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)