Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 058 (Sin is bondage)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
C - Safari ya mwisho ya Yesu kwenda Yerusalemu (Yohana 7:1 - 11:54) Neno Kuu: Kutenganisha giza na nuru
1. Maneno ya Yesu kwenye sikukuu ya Vibanda (Yohana 7:1 – 8:59)

e) Dhambi ni utumwa (Yohana 8:30-36)


YOHANA 8:30-32
„Naye alipokuwa akisema hayo, wengi walimwamini. Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.“

Unyenyekevu wake Kristo, jinsi alivyojishuhudia kwa nguvu iliwagusa wasikilizaji wengi. Walielekea kumwamini kwamba anatoka kwa Mungu. Yesu alisikia tumaini lao ndani yake akakubali utayari wao wa kusikiliza. Akawasihi wasiamini tu Injili yake hivi hivi, bali watafakari sana maneno yake na kujiunga naye, kwa shabaha ya kudumu ndani yake kama vile tawi la mzabibu ndani ya shina la mzabibu; kusudi Roho yake aweze kumiminwa ndani ya mioyo na mawazo yetu bila vizuizi; kusudi tusukumwe kutimiza mapenzi yake kwa matendo maishani mwetu. Yeyote atakayetekeleza maneno ya Kristo hivyo, atatambua kweli yenyewe. Maana kweli sio wazo tu, bali ni hakika ya kufaa tunayoshiriki katika kuendesha maisha yetu.

Kweli ya Mungu kwanza ni usemi wa uaminifu na ya hekima; pili ni kumtambua Mungu kuwa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu katika umoja wa upendo na shabaha. Tunapopata kuweka mizizi yetu ndani ya Kristo, tunazidi kufunuliwa uzuri wa Utatu Utakatifu.

Kumfahamu Mungu inabadilisha maisha yetu. Tumfahamu Mungu kiasi cha kuwapenda na wengine. Yeye asiyependa basi hamfahamu Mungu. Katika kumfahamu Mungu kwa njia ya maneno ya Kristo tunawekwa huru na ubinafsi wetu. Kusemea tu toba au wajibu wa kisheria haitatuweka huru na utumwa wa dhambi; inatakiwa kufahamu upendo wa Mungu, kukubali msamaha wa Mwana na kuja kwa Roho ndani ya maisha yetu. Upendo wa Mungu tu inayoweza kurarua minyororo ya ubinafsi na majisifu yetu.

YOHANA 8:33-36
„Wakamjibu, Sisi tu uzao wa Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru? Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikusote. Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.“

Wayahudi wakawa wanatatanishwa; babu zao waliishi miaka mia nne chini ya utumwa wa Farao kule Misri, wakajihesabia kuwekwa huru kwa enzi ya Mungu, maana ndiye aliyewatoa utumwani (Kutoka 20:2). Hivyo maneno ya Yesu yakawachokoza, alipokataa kwamba waliwekwa huru.

Yesu alihitaji kupooza kiburi cha wale walioanza kuamini ndani yake. Aliwaonyesha kwamba wao wote ni watumwa wa dhambi na watekwa wa shetani. - Nasi tukishindwa kutambua uzito wa kifo wa utumwa wetu, hatutatamani habari ya wokovu. Yeye ajijuaye kwamba mwenyewe hawezi kushinda dhambi zake, ndiye atakayekuwa tayari kumwomba Mungu amwokoe. Hapo tunaona sababu kwa nini watu wengi hawamtafuti Yesu; ni kwa sababu wanafikiri kwamba wenyewe hawahitaji wokovu wake.

Yesu anaeleza kwa msukumo, „Kila atendaye dhambi atakuwa mtumwa wa dhambi.“ Wengi wa vijana huanza maisha yao na uongo, uzembe na hafifu. Hucheza - cheza na dhambi na kugaagaa ndani yake na ndani ya mawazo yao; hatimaye hukusudia kuyatafuta yasiofaa na hivyo kupanga mapito yao kwa hila. Wanajaribu uovu kadhaa na kurudia, halafu yakawa ni uzoefu wao. Basi wanapoanza kutambua uchafu na ufisadi wao na kusikia kukemewa na dhamiri zao, nafasi kuyaacha huwa imepita; sasa wako watumwa wa dhambi zao. Mwishowe husukumwa kutenda ujangili hata bila kutaka. Hapo watalaumu saa walipoanza kusikiliza mawazo yao mabaya. – Wanadamu wameesha kuwa waovu, ingawa wanaficha ukweli unaochukiza nyuma ya maficho ya kicho na adabu za uongo. Kila mtu bila Yesu ni mtumwa wa tamaa zake. Shetani hucheza na neva zao, kama vile upepo unavyocheza na jani kavu.

Mwana wa Mungu hutamka neno lake la enzi, „Wakati huu mimi nipo pamoja nanyi na kutambua vifungo vyenu. Naweza, nami niko tayari kuwaweka huru na kufuta dhambi zenu. Sikuja ulimwenguni kwa ajili ya mageuzi ya juujuu tu, wala si kuwakemea kwa njia ya sheria kali zaidi. Hapana, nipo kwa kuwaweka huru kutoka kwa nguvu ya dhambi na utawala wa kifo na haki anazozidai shetani. Nitawaumba kwa upya, niwahuishe, ili nguvu ya Mungu ndani yenu ipate kuwa kinga ya dhambi. Bila shaka, hata hivyo shetani atawajaribu kwa mitindo elfu. Mtajikwaa, lakini si kama watumwa, bali kama watoto wanaoshika kwa juhudi haki zao mpya na kushinda.“

„Ninyi mmeokolewa kwa milele, mmelipiwa kwa damu yangu, mmenunuliwa kwenye soko la dhambi. Sasa mmekuwa wa pekee kwake Mungu. Amewatolea uhuru, ili mwe watoto huru kabisa. Hali mmewekwa huru na dhambi, mimi nawasafirisha kwenye ushirikiano na Mungu, mpate kumhudumia na kumshukuru kwa hiari kabisa. Mimi pekee ni mweka huru anayekuokoa kutoka kwa gereza la hatia, ukaingie kwenye utawala wa Mungu. Mimi ndimi Mwana wa Mungu, mwenye mamlaka ya kuwaweka huru wote wanaosikiliza sauti yangu.“

SALA: Bwana Yesu, tunakuabudu na kukusifu, maana wewe ndiwe mwokozi mwenye enzi zote, uliyetuweka huru kabisa msalabani kutokana na ujeuri wa shetani. Umetusamehe makosa yetu yote. Umetusafisha, ili tusiendelee kuwa watumwa wa uchungu na chuki, bali tumtumikie Mungu kama wana wa huru na kufurahia.

SWALI:

  1. Jinsi gani twaweza kuwekwa huru kweli kweli?

NAMBA - 3

Mpendwa msomaji, ututumie majibu sahihi 17 kutokana na maswali hayo 19. Ndipo tutakutumia masomo yanayofuata katika mfululizo huo wa Injili ya Yohana.

  1. Siri ya kuwalisha watu elfu tano ilikuwa ni nini?
  2. Kwa sababu gani Yesu alikataa kufanywa Mfalme na umati wa watu?
  3. Jinsi gani Yesualiwaongoza watu watoke kwenye hamu ya mkate, na wapate imani ndani yake?
  4. Neno la “Mkate wa Uzima” lina maana gani ?
  5. Jinsi gani Yesu aliitikia kwa manung’uniko ya wasikilizaji wake?
  6. Kwa nini Yesu aliwaambia wasikilizaji wake kwamba, lazima wale mwili wake na kuinywa damu yake?
  7. Jinsi gani huyu Roho mtoa uzima alikuwa ameunganika na nafsi ya Yesu?
  8. Maana halisi ya ushuhuda wa Petro ni nini?
  9. Kwa nini dunia ulikuwa unamchukia Yesu?
  10. Kuna thibitisho gani kwamba Injili inatoka kwa Mungu?
  11. Kwa nini Yesu ni mtu wa pekee ambaye anamfahamu Mungu kwa kweli?
  12. Yesu alitabiri nini kuhusu wakati wake ujao?
  13. Kwa nini Yesu anayo haki ya kusema:”Mtu akiona kiu na aje kwangu anywe”?
  14. Kwa nini makuhani na Mafarisayo waliwadharau watu wa kawaida?
  15. Kwa nini hao washitaki wa yule mwanamke mzinzi walitoka usoni pa Yesu?
  16. Je, ushuhuda wa Yesu juu yake kwamba yeye ni nuru ya ulimwengu, inahusiana namna gani na ufahamu wetu juu ya Baba wa mbinguni ?
  17. Imani ndani ya yule ajiitaye “Mimi ndiye”, inayo maana gani?
  18. Jinsi gani Yesu alitangaza uthabiti wake ndani ya Utatu Utakatifu?
  19. Jinsi gani twaweza kuwekwa huru kweli kweli ?

Kumbuka kuandika jina lako na anwani kamili kwenye karatasi ya majibu yako ya Quiz, sio kwenye bahasha nje tu. Ndipo uitume kwa anwani hii:

Waters of Life
P.O.Box 600 513
70305 STUTTGART
GERMANY

Internet: www.waters-of-life.net
Internet: www.waters-of-life.org
e-mail: info@waters-of-life.net

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 18, 2014, at 11:14 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)