Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 057 (Jesus the light of the world)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
C - Safari ya mwisho ya Yesu kwenda Yerusalemu (Yohana 7:1 - 11:54) Neno Kuu: Kutenganisha giza na nuru
1. Maneno ya Yesu kwenye sikukuu ya Vibanda (Yohana 7:1 – 8:59)

d) Yesu, nuru ya ulimwengu (Yohana 8:12-29)


YOHANA 8:25-27
“Basi wakamwambia, U nani wewe? Yesu akawaambia, Hasa neno. lilo hilo ninalowaambia. Ninayo mengi ya kusema na kuhukumu juu yenu; lakini yeye aliyenipeleka ni kweli, nami niliyoyasikia kwake, ndiyo ninenayo katika ulimwengu. Wala hawakutambua ya kuwa anawatajia Baba.”

Mbali na kusisitiza kwake Kristo juu ya uungu wake, Wayahudi wakanang’ania kuuliza, „Wewe ni nani? Tupatie ishara; eleza wazi jambo hilo, ili tuweze kulishika!” Hata hivyo alikuwa amejidhihirisha kabla ya kuuliza kwao waziwazi iwezekanavyo.

Yesu akaitika, “Kwanza kabisa, mimi ndiye Mungu wa kweli; ila mlikosa kuelewa maneno yangu. Roho yangu hajaweza kuingiza mguu ndani ya mioyo yenu. Ninyi hamna namna ya kushika mafunuo yangu kuhusu majina na tabia yangu. Mimi ndiye Neno la Mungu mwilini. Lakini ninyi hamnisikii wala kuelewa, kwa sababu ninyi ni wa dunia ya chini, wala si wa Mungu. Hivyo hamtaruhusu roho yangu kuumba uangalifu mpya ndani yenu. Kwamba nimesema nanyi tena na tena haikuwafaa bado, maana mnayo mioyo migumu. Kwa sababu hii maneno yangu yatawahukumu, ingawa mimi nawapenda na kujifunua kwenu. Mmoja au wawili kati yenu pengine ataanza kutambua enzi yangu. Natamani sana kuwaokoa na kuwahuisha. Mungu ndiye ukweli, sawasawa na mimi. Lakini ukweli huo utawaangamiza, kwa sababu mnakataa kushuka kwa Roho ndani ya mioyo yenu.” Hata hivyo Wayahudi hawakushika maana iliyofichwa ndani ya mafunuo hayo, wala kutambua umuhimu wa umoja wake na Baba. Walisikiliza maneno yake, lakini kuelewa hakuna, kwa sababu hawakutaka kuamini ndani yake.Imani rahisi ndani yake inafunulia kwa akili zetu ukweli wake uliyo wazi.

YOHANA 8:28-29
“Basi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye; na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba anavyonifundisha ndivyo ninenavyo. Naye aliyenipeleka yu pamoja nami, hakuniacha peke yangu; kwa sababu nafanya sikuzote yale yampendezayo.”

Yesu alielewa kwamba maadui zake na hata wanafunzi wake walikosa kutambua ukweki kabisa juu yake. Maana Roho Mtakatifu alikuwa bado hajaja chini. Lakini Yesu hakuwa na mashaka kwamba, kuinuliwa kwake juu msalabani kutafuta kabisa dhambi za ulimwengu. Wakati wa kupaa kwake juu kwa Baba kutatayarisha kumwagwa kwa Roho Mtakatifu. Kwa jambo hilo utambuzi kuwa yeye ni nani utapiga kama radi ndani ya akili za Wayahudi na wasio Wayahudi. Uungu wa Kristo haitambuliki isipokuwa kwa kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya mtu. Kuhojiana juu ya hilo ni msaada mdogo sana tu. Kuzaliwa mara ya pili ndiyo inaumba imani thabiti ndani ya mtu, jinsi imani ya kweli kuhusu upole wa Kristo inavyoumba hatua ya kuzaliwa mara ya pili.

Kristo hakusema kwamba yeye ni mungu kamili anayejitegemea, bali alitangaza wazi kwamba umoja wake wa lazima na Baba unatenda kazi. Na pia hatendi lolote kwa uamuzi wake mwenyewe tu. Baba hufanya kazi ndani yake. Kiasi cha ubinadamu wake inajionyesha kwa kukubali kwake kwamba anayo jina la “Mtume wa Mungu”. Lakini hata hivyo katika matamshi yake alijifunua kuwa “Bwana wa historia”.

Baba yetu wa mbinguni siye mwepesi, lakini mwenye uwazi, jinsi anavyoonyeshwa na Roho Mtakatifu. Kwa mambo ambayo Yohana ametusimulia kuhusu maana hizo za juu sana, Yesu anashiriki ukweli wa kuogofya katika umoja wa Utatu. Ndipo anaendelea kusema, “Baba yangu alikuwa pamoja nami tangu milele, naye yu nami hata sasa, wala hajaniacha peke yangu hata kwa dakika moja. Na kwa kugeuza matamshi, Mwana hajamwacha Baba wa mbinguni hata kidogo, wala hajamwasi wakati wowote lakini yeye ni wa kumtii na kwa kumpendeza daima. Alishuka toka mbinguni akawa mwanadamu kutokana na mapenzi ya Baba yake”. Loo, ni tamko la kupendeza zana, “Wakati wowote natenda yanayompendeza Baba.” Hakuna ila Mwana tu awezaye kutamka kama hayo, akiishi wakati wowote kwa kukubaliana na Baba yake, katika ukamilifu wa Roho. Yesu alitimiza sheria kikamilifu. Na zaidi ya hapo, yeye ndani yake alikuwa ni sheria au amri kamili ya Agano Jipya (UPENDO). Hata hivyoWayahudi walimwita mkufuru, anayevunja sheria na kuwapotosha watu, wakati yeye pekee ni mwenye kutimiza sheria kikamilifu.

Ndugu, wewe unasikia sauti ya Roho kwa matangazo ya Kristo kuhusu nafsi yake? Unasikia enzi na uvumilivu wake, uhuru wake na kujinyenyekeza kwake kwa Baba? Kwa njia hii alitamani kukuvuta na wewe ndani ya ushirikiano wa upendo wake kwa kujikabidhi kwake kwa uhuru pamoja. Atakuongoza katika raha na huduma kwa kuwepo kwake. Atakuwa mwalimu wako, nawe hutatenda lolote mbali na kutaka kwake, ukitenda yote kwa shabaha ya kumpendeza. Je, utapenda uwe na hali hiyo?

SALA: Bwana Yesu, nasikia haya kwa ukaidi wangu, ujanja na hila zangu. Naomba nisamehe makosa yangu yote. Unitakase, ili nijitoe kabisa kwa uongozi wa Roho Mtakatifu wako. Naomba uwe kiongozi na mwalimu wangu; fungua moyo na akili zangu kwa upendo wako wa daima.

SWALI:

  1. Jinsi gani Yesu alitangaza uthabiti wake ndani ya Utatu Utakatifu?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 18, 2014, at 11:13 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)