Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 052 (Disparate views on Jesus)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
C - Safari ya mwisho ya Yesu kwenda Yerusalemu (Yohana 7:1 - 11:54) Neno Kuu: Kutenganisha giza na nuru
1. Maneno ya Yesu kwenye sikukuu ya Vibanda (Yohana 7:1 – 8:59)

b) Maoni tofauti tofauti juu ya Yesu kati ya watu na kwenye Baraza Kuu (Yohana 7:14-53)


YOHANA 7:37-38
„Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu alisimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.“

Wakati wa sikukuu Yesu alihubiri tena kwa makutano ndani ya ua la hekalu. Watu walikuwa wakimngojea kuhani mkuu kumwaga maji kwenye madhabahu. Makuhani walitokea kwa mfuatano wakifurahia ili wamwage yale maji mbele ya Mungu kama sadaka ya shukrani, alama ya baraka waliotazamia kutoka kwa Mwumbaji wao kwa ajili ya mwaka ujao. Asili ya mapokeo hayo ni maneno ya Isaya aliposema: „Watachota maji kwa furaha kutoka kwa chemchemi za wokovu.“

Yesu alitambua roho zao zenye kiu, ambao mbali na mambo yote ya mapokeo yao hawakufahamu wokovu. Yesu aliinua sauti yake kuelekea kwa makutano yenye matazamio makubwa, akisema, „Njooni kwangu mkanywe maji ya uhai bure - yeyote asikiaye kiu na aje kwangu, mimi ndimi chemchemi ya uzima.“

Wale wasiotamani uzima huu tukufu, hawatamjia Mwokozi kamwe. Ila kwa wale watakaokimbilia kwake, Yesu awaambia, „Yeyote aniaminiye mimi na kujifunga nami binafsi, yeye atakuwa kama chemchemi ya baraka kwa wengi. Maandiko yanakushurutisha kuwa na imani ndani yangu, tena Mungu anakuagiza uje kwangu ukapate uhai na furaha.“ Yeyote amjiaye Yesu kwa ujasiri na akinywa kutoka kwa maneno yake na kujazwa na Roho yake atakuwa amebadilishwa kikamilifu. Mwenye kiu atabadilika kuwa kisima; mwovu naye mwenye kujifikiria tu, pia atabadilika kuwa mtumishi mwaminifu.

Je, umewahi kupata kuona bahati njema ya utunzi wa Yesu? Yeye anatamani upate kuwa kama kisima chenye maji masafi. Bila shaka hata moyo wako unaweza kutoa mawazo mabaya, lakini Yesu anaweza kusafisha moyo wako na maneno ya mdomo wako. Na hivyo upate kuwa chemchemi ya baraka kwa ajili ya wengi.

Shabaha ya Yesu sio kusafisha mawazo na roho yako tu, bali na mwili wako pia, ili upate kuwa sadaka iliyo hai inayokubalika mbele za Mungu, ukiwatumikia waliopotea. Yeye Yesu anakusudia utakaso wako kikamilifu, ili kwamba usiendelee kuishi kwa ajili yako binafsi tu, bali utumie nguvu zako kwa huru kuwahudumia wengine. Yeyote atakayejitoa kwake Yesu bila masharti, basi atabadilika kuwa baraka kwa ajili ya watu wengi.

YOHANA 7:39
„Na neno hilo alilisema kwa habari ya Roho, ambaye wale wamwaminiyo watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.“

Yeyote amwaminiye Yesu atapokea zawadi ya Roho Mtakatifu. Mshuko wa Roho maishani mwa mtu ni mwujiza hata katika kizazi chetu. Hadi leo tunaishi katika muda wa mgao wa Roho Mtakatifu. Yeye si kama malaika au tukio la njozi, lakini yeye ni Mungu mwenyewe, akijaa utakatifu na upendo. Roho anafananishwa na mwali wa moto au upepo mwenye enzi. Tena hapo hapo yeye ni mfariji mpole. Kila Mkristo wa kweli anakuwa hekalu la huyu Roho Mtakatifu.

Huyu Roho tukufu hakumwagwa kijumla kote ulimwenguni siku za maisha ya Kristo duniani, kwa sababu madhambi yalitenganisha binadamu na Bwana wao. Milima ya udhalimu ikawa kama kizuizi kwa Roho asiwafikie wanadamu. Lakini baada ya Yesu kushughulikia dhambi zetu kwa kutufia, ndipo kupaa mbinguni na kuketi mkono wa kulia kwa Mungu, hapo akamtuma Roho wa upendo wake katika ushirikiano na Baba, ndipo kuimwagia juu ya waumini wake kote walipokuwapo. Mungu ni Roho awezaye kuwapo wakati wowote na mahali popote. Hivyo anaweza kutawala ndani ya mwumini, aliyekwisha kukubali msamaha wa dhambi zake kwa njia ya damu ya Yesu. - Ndugu je, umepokea Roho wa Mungu tayari? Nguvu ya Kristo imekuja maishani mwako? Njoo kwake Yesu aliye asili ya mwamko na baraka. Yeye anakuhakikishia, „Yeyote anijiaye hatakuwa na njaa, na yeyote aniaminiye hataona kiu daima. Basi aaminiye hivyo, jinsi maandiko yanavyosema, kutoka kwa mwili wake yatamwagwa mito ya maji ya uzima kwa ajili ya wengine.“

YOHANA 7:40-44
„Basi wengine katika mkutano walipoyasikia maneno hayo, walisema, Hakika huyu ndiye nabii yule. Wengine walisema, Huyu ndiye Kristo. Wengine wakasema, Je, Kristo atatoka Galilaya? Andiko halikusema ya kwamba Kristo atoka katika uzao wa Daudi, na kutoka Bethelehemu, mji ule alioukaa Daudi? Basi kukaingia matengano katika mkutano kwa ajili yake. Baadhi yao wakataka kumkamata, lakini hakuna mtu aliyenyosha mikono yake ili kumshika.“

Baadhi ya wasikilizaji wakasikia enzi ya ukweli ndani ya maneno ya Yesu, nao wakajitoa kwa enzi hiyo. Wakakiri waziwazi kwamba yeye ni nabii, akifahamu mapenzi ya Mungu, na akitambua na siri za mioyo ya watu. Yeye ndiye yule nabii aliyetajwa na kuahidiwa kwa Musa, atakayewaongoza watu wa Agano la Kale kutoka ushindi hadi ushindi kwa ushirikiano na Mungu. Kwa njia hii wachache wao walijaribu kukiri kwamba, huyu Mnazareti kweli ndiye Masihi aliyeahidiwa.

Hata hivyo, akili za Waandishi ilikataa wakisema: „Hapana! Huyu atoka Nazareti, bali Masihi lazima atokee mji wa Daudi na kutoka kwa ukoo wake.“ Kukariri maandiko hivyo ilikuwa ni sawa kabisa. Basi kwa nini Yesu hakuwaeleza kwamba alizaliwa Bethelehemu? Kuna sababu zake: Kwanza familia ya mfalme Herode wasingekubali mfalme mpya atokee nje ya ukoo wao wa kifalme. Wao walikuwa tayari kuchinja makumi elfu, ili wafaulu kuendelea kutawala. Pili, Yesu hakutamani kupata wafuasi kwa njia ya thibitisho la kihistoria. Alipendelea kujenga tumaini lao kwa njia ya upendo na wao kutambua mamlaka yake wenyewe. Hivyo aliwavuta kwake wale walioamini bila kuona.

Kinyume cha mgongano uliokuwa kati ya makutano wakajigawa katika makundi. Baadhi walimkiri kuwa ni Masihi, wengine walikataa kabisa. Watumishi wa hekalu walisimamia shabaha yao ya kumfunga Yesu. Lakini mamlaka ya huru ya maneno yake iliwaogofya, wakashindwa kumkaribia.

SALA: Bwana Yesu, tunakuabudu kwa ajili ya upendo wako na mamlaka yako. Wewe ndiwe asili ya uhai. Umejifunga nasi kwa imani. Umemwaga Roho yako ndani yetu. Utukufu wako umekuwa na ya kwetu kwa imani - sisi tulio na dhambi. Maana umetusafisha na damu yako, ili tuweze kuishi daima, Amina.''

SWALI:

  1. Kwa nini Yesu anayo haki ya kusema, „Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe!“?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 18, 2014, at 11:09 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)