Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 053 (Disparate views on Jesus)
This page in: -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
C - Safari ya mwisho ya Yesu kwenda Yerusalemu (Yohana 7:1 - 11:54) Neno Kuu: Kutenganisha giza na nuru
1. Maneno ya Yesu kwenye sikukuu ya Vibanda (Yohana 7:1 – 8:59)

b) Maoni tofauti tofauti juu ya Yesu kati ya watu na kwenye Baraza Kuu (Yohana 7:14-53)


YOHANA 7:45-49
„Basi wale watumishi wakawaendea wakuu wa makuhani na Mafarisayo. Nao wakawaambia, Mbona hamkumleta? Wale watumishi wakajibu, Hajanena kamwe mtu yeyote kama huyu anavyonena. Basi Mafarisayo wakawajibu, Je, Ninyi nanyi mmedanganyika? Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo? Lakini makutano hawa wasioifahamu torati wamelaaniwa.“

Wakati Yesu alipokuwa anafundisha hekaluni, Mafarisayo walikutana wakitazamia watumishi wao wamshike Yesu na kumleta kwao. Makuhani wakuu wanatajwa kama zaidi ya mmoja, iwapo kuhani mkuu huwa aongoza baraza kuu kwa maisha yote. Basi Warumi waliotawala mara kwa mara waliwaondoa katika nafasi yao. Kwa sababu hiyo kulikuwa na makuhani makuu kadhaa wakati wa Yesu walioondolewa na Warumi; lakini wote walikuwa wa ukoo wa kikuhani na kuendelea kuheshimiwa na Wayahudi. Kawaida walikuwa ni Masadukayo na kuelekea kutafakari huru kuhusu torati, na hivyo hawakupatana na namna ya kisheria ya Mafarisayo.

Hata hivyo Mafarisayo barazani waliketi sambamba na makuhani. Wao kama washika torati walikataa kutafakari namna ya kiyunani, na wakafanya sheria kuwa msingi wa imani yao na njia ya kufanya kazi katika chama chao. Walikuwa na mioyo migumu, wakimheshimu Mungu kwa ukali wa msimamo wao kwa ajili yao wenyewe na wengine pia.

Wote, Mafarisayo na Masadukayo walikasirika kwa kukosa kumshika Yesu. Wanafunzi wake hawakumpigania wala makutano hawakumlinda, lakini maneno yake yakawaingia moyoni wote, basi hawakujaribu kumshika, kwa sababu walitambua nguvu ya Mungu iliyotenda kazi ndani yake.

Kwa jambo hilo Mafarisayo walikuwa wamesisimuka na kuwakemea watumishi wa hekalu wakisema, “Ninyi nanyi mmejiunga na makundi ya huyu mdanganyi? Hata mmoja wa waheshimiwa washiriki wa baraza anamwamini. Hakuna mwumini mwaminifu ambaye angethubutu kumfuata huyu Mgalilaya.”

Kwa kweli wengi walianza kumpenda Yesu, ila walikuwa ni watu wa kawaida tu, waliodharauliwa, waovu au wenye tabia mbaya. Yeye aliwahi kukaa nao na kushiriki kula nao na hivyo kuwaheshimu kwa kuwepo kwake. Lakini waliojidai kuwa wacha Mungu walidharau hao watu na kuwahesabu kama walaaniwa. Waliwatazama kwa miwani ya kisheria. Ila kwa hali halisi hao wadharauliwa ndiyo waliomfuata Yesu. Wengine wao waliwahi kukiri makosa yao hata mbele ya Yohana Mbatizaji. Basi watawala waliwachukia umati huo, wakisahau kwamba walisema lugha moja nao na kufuata desturi za namna moja. Watu wote waliunda shirika la taifa moja mbali na matatizo au migawanyo iliyokuwapo kati ya madaraja mbalimbali.

YOHANA 7:50-52
“Akawaambia Nikodemo, ( naye ni yule aliyemwendea zamani, maana ni mmoja wao), Je, torati yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza, na kujua atendavyo? Wakajibu, wakamwambia, Je, wewe nawe umetoka Galilaya! Tafuta ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii.”

Mmoja wa wale waliokuwapo alisumbuka kwa uadui ndani ya baraza. Huyu alikuwa ni Nikodemo, aliyemjia Yesu sirini wakati wa usiku. Yesu alikuwa amemwonyesha wakati ule Haja ya kuzaliwa kwa upya. Hadi sasa alikuwa chini ya mvuto wa Yesu, akataka kupatanisha kwa niaba yake, bila kukiri wazi kwamba alimpendelea Yesu.Alitumia namna ya kisheria mbele ya baraza, iliyokataa kupitisha hukumu wakati mstakiwa hayupo.

Mahakimu hata hivyo walimcheka huyu mtu mwenye dhamiri. Hata kama baraza lingeketi kwa hukumu, ingekuwa jambo la maneno tu kijumla, kama wangemhukumu asiye na hatia kwa hatua za kudanganya. Wanashauri wakasikia kwamba ushahidi wa kukomesha ilikuwa kwamba, Yesu ni nabii wa uongo kwa vile alitoka Galilaya, mkoa uliodharauliwa na Wayahudi kwa ajili ya kuwa walegevu kuhusu kushika amri. Waliona hakuna Maandiko inayotaja kwamba Masihi mtazamiwa au nabii wa siku za mwisho atokee kule. Mafarisayo walihakikisha kwamba ni mwongo, hivyo wakamdhihaki Nikodemo, aliyetamani kumweleza Yesu mbele zao, ili kuwashawishi kwa uhodari wa maneno yake, jinsi yeye alivyomwaminisha Nikodemo mapema.

SWALI:

  1. Kwa nini makuhani na Mafarisayo waliwadharau watu wa kawaida?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 18, 2014, at 11:10 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)