Previous Lesson -- Next Lesson
b) Maoni tofauti tofauti juu ya Yesu kati ya watu na kwenye Baraza Kuu (Yohana 7:14-53)
YOHANA 7:31-32
“Na watu wengi katika mkutano wakamwamini; wakasema, Atakapokuja Kristo, je! Atafanya ishara nyingi zaidi kuliko hizi alizozifanya huyu? Mafarisayo wakawasikia mkutano wakinung’unika hivi juu yake; basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakatuma watumishi ili wamkamate.”
Ijapokuwa kulikuwa na hali ya kushtusha hapo Yerusalemu, wengi walianza kuamini enzi iliyotenda kazi ndani ya Yesu. Wakasema, “Labda ndiye Masihi; maana alitenda ishara nyingi za nguvu.” Hata wenye hali nafuu wakasukumwa kutafakari na wakaanza kumtegemea Yesu. Twaona hapa kwamba Yesu alikuwa na wafuasi wake hata kwenye mji mkuu.”
Mafarisayo walipotambua kutokana na wapelelezi wao kwamba, mwamko fulani ulianza kati ya watu, na mwendo waYesu ulianza kushika mizizi hapo Yerusalemu, wakajisikia kuchokozwa, wakatafuta namna ya kushirikiana na lile kundi ambalo walikuwa kinyume chao, ambao ni makuhani na Masadukayo. Walifanya hivyo, ili wachochee wale wenye madaraka hekaluni, ili wamrufuku Yesu. Makuhani wakuu wakakubali jambo hilo wakajinyenyekeza kushirikiana na Mafarisayo kwa ajili ya kumfunga Yesu.
Malaika wa Bwana walikuwa wanamzunguka huyu mwalimu mtukufu ndani ya ua la hekalu, wakawazuia watumishi wasiweze kutimiza agizo waliopewa na wakubwa wao. Yesu aliwaona hao watumishi wakimkaribia, lakini hakutoroka, bali alifunua utukufu wake, ambao mwinjilisti alitusimulia kama utabiri juu ya mpango wa Mungu wa kuleta wokovu.
YOHANA 7:33-36
“Basi Yesu akasema, Bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; kisha naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka. Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja. Basi Wayahudi wakasemezana, Huyu atakwenda wapi hata sisi tusimwone? Ati! Atakwenda kwa utawanyiko wa Wayunani, na kuwafundisha Wayunani? Ni neno gani hilo alilolisema, Mtanitafuta wala hamtaniona; nami nilipo ninyi hamwezi kuja?”
Yesu aliwatangazia maadui yake kwamba atabaki kwa kifupi na wafuasi wake. Alikuwa ameeshajua kwamba atakufa kama Mwana-Kondoo wa Mungu. Wakati huo nao alifahamu siku ya kufufuka kwake, kupaa na kurudi kwake kwa Baba. Yesu alitamani kurudi kwa Baba yake, aliyekuwa amemtuma kutuokoa. Kwa sababu ya upendo wake kwetu alivumilia ulimwenguni mbali na kwake mbinguni.
Yesu aliona mapema jinsi wafuasi wake watakavyoshangaa kwa ufufuo na kupaa kwake. Kwamba watarudi kwa huzuni, kwa sababu bado hawakuwa na miili ya kiroho ambayo ingepaa naye mbinguni. Pia alielewa kwamba, adui zake watatafuta mwili wake “uliopotea”, utakaotoweka kutoka kwenye kaburi uliowekewa muhuri. - Ole wao wasiompenda Mwokozi! Hawataweza kushiriki katika utukufu wake wala kuingia mbinguni. Dhambi zao zitawatenganisha na Mungu. Kutokuamini kwao kutawazuia nje ya nafasi ya neema.
Wayahudi walishindwa kuelewa maneno ya Yesu, kwa sababu walitafakari kwa namna ya kibinadamu kwamba, alikusudia kutoroka kwa masinagogi ya Wayahudi yaliyoko Uyunani (au Ugriki), kwenye miji inayozungukia Bahari ya Kati. Kusudi lake ingekuwa kujipatia wafuasi kutoka kwa wale wasioelewa sana maandiko ya kiebrania. Wengine wakachokoza wakisema: „Labda anatamani kuwa msemi maarufu na kutangaza maoni yake kwa wanafilosofia wa kiyunani na kuwaongoza kwake Mungu aliye hai.
Mwinjilisti Yohana alipoandika maongezi ya Yesu na matukio hayo, alikuwa ameishi kule Efeso kati ya Wayunani. Habari njema hiyo ya wokovu ilikuwa imeesha kuwafikia Wayahudi waliotawanyike kule. Wayunani wengi wakamwamini Kristo. Mwinjilisti aliona katika maneno ya Yesu na katika manung’uniko ya Wayahudi kuna tangazo kwamba Yesu ndiye mwalimu mkuu hata kati ya Wayunani. Maana hakuwatolea filosofia tupu inayompeleka mtu kwenye tabia ya kuona mambo yote ni mabaya. Yeye ndiye mwenye kutoa uhai wa kweli; kutoka kwake kunachipuka enzi isiyoweza kushindwa.
SWALI:
- Yesu alitabiri nini kuhusu wakati wake ujao?