Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 050 (Disparate views on Jesus)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
C - Safari ya mwisho ya Yesu kwenda Yerusalemu (Yohana 7:1 - 11:54) Neno Kuu: Kutenganisha giza na nuru
1. Maneno ya Yesu kwenye sikukuu ya Vibanda (Yohana 7:1 – 8:59)

b) Maoni tofauti tofauti juu ya Yesu kati ya watu na kwenye Baraza Kuu (Yohana 7:14-53)


YOHANA 7:21-24
“Yesu akajibu akawaambia, Mimi nalitenda kazi moja, nanyi nyote mnanistaajabia. Musa aliwapa tohara; lakini si kwamba yatoka kwa Musa, bali kwa mababa; nanyi siku ya sabato humtahiri mtu. Basi ikiwa mtu hupashwa tohara siku ya sabato, ili torati ya Musa isije ikavunjika, mbona mnanikasirikia mimi kwa sababu nalimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato? Basi msihukumu hukumu ya macho tu, bali ifanyeni hukumu iliyo haki.”

Yesu hakujibu moja kwa moja kwa hisia ya Wayahudi kwamba anayo roho mbaya, bali aliwaonyesha makutano waliokuwepo kwamba, tamko lililotajwa juu yake kwamba auawe ilikuwa ni upuzi wala si haki. Aliwakumbusha kwamba hukumu ya viongozi juu yake ilisababishwa na uponyaji wake kwa kilema pale Bethesha kwa siku ya sabato. Siku ile Yesu alimwagiza ainue godoro lake na aende nyumbani hali akiwa mzima. Huu ilikuwa ni mwujiza mkubwa, na ishara hiyo ilistahili kuondolewa kwake ile hukumu dhidi yake.

Ndipo Yesu alihakikisha kwamba hao mafundi wa sheria wenyewe hawakutimiza sheria kikamilifu. Sheria hii inayo hitilafu zake: Kutahiriwa ndiyo alama ya agano na Mungu, wakati Sabato inasema habari ya ushirikianao na mengineyo ya huyu Aliye Mtakatifu. Iliwapasa watu kuwatahiri watoto wao siku ya nane baada ya kuzaliwa, na siku hiyo pengine itaangukia kwenye Sabato. Je, kutahiri si kazi?

Kwa vile ugonjwa unahisiwa kuwa ni tukio la dhambi, kuponywa ilimaanisha wokovu kwa mwili, utu wa ndani na roho. Basi Yesu aliwahimiza watu watumie akili zao, ili watofautishe ile huduma ya huruma mbali na kutahiriwa siku ya Sabato - waone ipi ni ya thamani zaidi? Hivyo alitumia uwezo wa akili ili waamshwe kutambua kiwango cha upendo wake na enzi na wokovu. Ila jaribu lake ilikuwa bure; masikio yao yalikuwa siwi na roho zao zikawa gumu - uamuzi wa haki na kukata shauri kwema haikuwezekana kwao.

YOHANA 7:25-27
“Basi baadhi ya watu wa Yerusalemu wakasema, Je! Huyu siye wanayemtafuta ili wamwue? Na kumbe! Anena waziwazi, wala hawamwambii neno! Yamkini hao wakuu wanajua hakika ya kuwa huyu ndiye Kristo? Lakini huyu twamjua atokako; lakini Kristo atakapokuja hakuna ajuaye atokako.”

Wenyeji wa Yerusalemu wakafika karibu na hekalu na kukuta mkutano mkubwa. Walipomtambua Yesu akiwa katikati yao na wote wakimsikiliza, wakaghadhabika, maana bado alikuwa anatembea kwa huru, kinyume cha agizo la kumfunga. Na jambo hilo lilieleweka wazi kwa wote.

Wenyeji wa mji mkuu wakadhihaki Baraza Kuu kwamba ni dhaifu katika jambo hilo. Warumi walikuwa wameondoa uwezekano kwa viongozi wa Wayahudi wa kumhukumu mtu afe. Watu walicheka kwa dhihaka wakisema, “Mwenye kutafutwa anatembea kwa huru mjini, na kuhubiri uani mwa hekalu bila hofo. Viongozi hawana nguvu ya kumlaani. Hata makuhani walishindwa kumweza kwa hoja zao au kwa mijadala naye.”

Wengine wakaitika hivi: “Ninyi hamwelewi, pengine baadhi ya viongozi wanaamini kwamba yeye ndiye Masihi.” Hii ilikuwa ni jambo lao la kuweka wazi kwamba hawakutaka Yesu afungwe. Basi, maoni ya watu yaligawanyika katika vikundi mbalimbali.

Maoni aina ya tatu: Ikiwa kuja kwa Masihi inasadikiwa, angeng’aa kitukufu katika hali ya siri, wala si mtu wa kawaida tu. Huyu mtu mwenye umri mdogo alikuwa ni seremala toka vijijini kule milimani. Masihi wa kweli atakuja kutelemka moja kwa moja toka mbinguni, wala si kutembea hivi kati ya watu wa kawaida.

YOHANA 7:28-30
“Basi Yesu akapaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, Mimi mnanijua na huko nitokako mnakojua? Wala sikuja kwa nafsi yangu; ila yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi. Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma. Basi wakatafuta kumkamata; lakini hakuna mtu aliyenyosha mkono wake ili kumshika, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado”

Yesu alikuwa anasikiliza maoni hayo kuhusu asili yake ya kidunia. Akasema kwa sauti nzito, “Mnanijua kweli? Au ni wapi nitokako? Ninyi ni wa kijuujuu tu katika maamuzi yenu, wala hamjibidiisha kunifahamu kwa undani. Mnisikilize, chimbeni chini ndani ya roho yangu. Ndipo mtakapofahamu mimi ni nani na nilikotoka.”

Yesu hakujituma mwenyewe, bali Mungu alikuwa nyuma yake, ambaye kutoka kwake. Baba yake ndiye yeye aliyemtuma. Yesu alikuwa na namna ya Baba yake na daima alikuwa kitu kimoja naye. Akaongeza kusema, “Hakuna kati yenu amjuaye Mungu, ingawa mnafikiri yupo nanyi hapa hekaluni. Makuhani yenu ni vipofu; hawamwoni Mungu, wala hawasikii sauti yake kwa kweli. Basi mwajidanganya wenyewe.”

Ndipo akasema, “Mimi namfahamu.” Kiini cha Injili ndiyo hii, kwamba Yesu amfahamu Mungu na kutueleza jina la Baba yake na upendo wake. Huyu Mnazareti alikuwa bila dhambi, akiishi daima katika ushirikiano na Baba yake. Kinyume chake wengine wote wakajitenga wenyewe na huyu Mtakatifu kutokana na dhambi zao.

Baadhi ya wasikilizaji walipotambua umuhimu wa maneno yake, kwamba Yesu aliwahukumu wazi wazi, wakalia, “Alikufuru dhidi ya Hekalu na kutueleza kwamba tu wakafiri”. Walikasirika wakalia kwa kelele, wakijaribu kumkamata. Lakini hakuna kati yao aliyeweza kumwelekea Mwana wa Mungu, kana kwamba malaika walikuwa wanamzunguka. Saa iliyopangwa kwa ajili ya ushuhuda wake wa mwisho ilikuwa ni bado. Baba yake alikuwa amepanga saa ya kuamua, ambapo Kristo aokoe binadamu.

SALA: Bwana Yesu, tunakuabudu, kwa vile unamfahamu Mungu na kufunulia kwetu habari ya Baba. Ufunuo wako umetufanya sisi tuwa watoto wa Mungu. Tunakutukuza na kukuza jina lako pamoja na wote waliozaliwa mara ya pili. Tunakusihi umfunue Baba na kwa watu waaminifu wanaotuzunguka, ili wapate kurejea kutoka kwa ushupavu na uzembe wao.

SWALI:

  1. Kwa nini Yesu ni mtu wa pekee ambaye amfahamu Mungu kwa kweli?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 18, 2014, at 11:07 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)