Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 045 (Jesus offers people the choice)
This page in: -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
B - Yesu ni chakula cha (mkate wa) uzima (Yohana 6:1-71)

4. Yesu anawapa watu chaguo: “Kubali au kataa!” (Yohana 6:22-59)


YOHANA 6:51
51 „Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni, mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.“

Je, uliwahi kuona mkate unaotembea au kusema? Yesu alijiita mwenyewe Mkate wa Uzima, mkate mwenye uhai - hasemi habari ya mkate wa kawaida toka mbinguni, lakini chakula cha kiroho na tukufu. Yeye hamaanishi kwamba tumeze mwili wake halisi; sisi sio walaji wa watu.

Basi mapema Yesu alianza kuzungumzia kifo chake. Siyo utawa wake uliookoa binadamu, lakini kuingia kwake mwilini. Akawa mwanadamu, ili ajitoe hadi kufa kwa dhambi zetu. Wasikilizaji wake walichukizwa; alionekana kuwa mtu wa kawaida, atokaye katika familia isiyokuwa na sifa ya kipekee. Kama malaika angalitelemka toka mbinguni, wangailimpokea kwa kupiga makofi. Yesu aliwaeleza kwamba, si utukufu wake wala uwezo wa roho yake ungewaokoa, bali mwili na uhai wake ambazo zitatolewa kwa huruma zitaweza jambo hilo.

YOHANA 6:52-56
52 „Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao, wakisema, Awezaje mtu huyu kutupa sisi mwili wake ili tuule? 53 Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. 54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; Nami nitamfufua siku ya mwisho. 55 Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.“

Kati ya hao Wayahudi kulikuwa na waumini na wakataaji wa Yesu. Vikundi hivi viwili walihojiana kwa vikali. Maadui wa Yesu walichukizwa kwa wazo la kula mwili wake na kunywa damu yake. Yesu alihimiza mgawanyiko kati ya makundi hayo mawili, ili wale wanaomtegemea kweli wapate kuonekana. Alijaribu upendo wa kundi la kwanza, na kuonyesha wazi upofu wa wale wengine. Akakaza kusema, „Amin, amin,nawaambieni, msipokula mwili wangu na kuinywea kikombe changu, hamna uzima ndani yenu. Msiposhiriki katika kuwepo kwangu, mtaendelea kubakia katika hali ya kufa na dhambi daima.“ Maneno hayo yalilia masikioni mwao na kusikika kwao kama maneno ya kumtukana Mungu. Kana kwamba huyu mtu Yesu alithubutu kuwaambia: „Mniue na kunimeza, maana ndani yangu mimi ni mwujiza. Mwili wangu ni mkate, ulio uhai tukufu, unaotolewa kwenu.“ Damu yao ilichemka na wakawa na ghadhabu. Hata hivyo, wale waliomtegemea, waliitika kwa kuvutwa na Roho Mtakatifu, wakiamini hayo ya ajabu, wakiegemea kwake Yesu, na wapate njia ya kuonyesha maneno yake kuwa mema. Kama wangetafakari kidogo, wakati wa Pasaka, wangekumbuka jinsi Yohana Mbtizaji alivyomwita Yesu Mwana Kondoo wa Mungu. Wayahudi wote walikuwa wanashiriki Pasaka na kula nyama ya kondoo waliochinjwa kwa tukio hilo. Hii ilitendeka kwa kupisha mbali hasira ya Mungu, wakikubaliana na sadaka hizo. Yesu aliweka wazi kwamba, yeye ndiye Mwana Kondoo wa kweli wa Mungu abebaye dhambi za ulimwengu.

Siku hizi tunafahamu kwamba alama za Ushirika Mtakatifu zinakumbusha kwamba mwili wa Kristo humezwa nasi, na damu yake inatusafisha na dhambi zetu. Tunamshukuru kwa neema yake. Hao Wagalilaya wakati ule hawakuelewa siri hii, basi maneno yake yalipumbaza akili zao. Yesu alijaribu imani yao, lakini ukaidi wao mapema ukajionyesha katika hasira kali.

Sisi tunamwabudu Kristo katika furaha na shukrani, maana alitueleza Ushirika Mtaktifu katika alama (mkate na divai), na jinsi anavyokuja kwetu kwa njia ya Roho yake. Bila sadaka yake hatuwezi kumkaribia Mungu au kuendelea naye. Msamaha kamili wa dhambi zetu inatufanya tustahili kuja kwake ndani yetu. Imani ndani yake inatokeza mwujiza huo, na kutufanya washiriki katika ufufuo wake tukufu. Tunaabudu Mwana Kondoo kwa ajili ya kutuokoa. Jesu hakuridhika kutufia msalabani, bali anatamani kutujaza kwa kutawala ndani yetu kiroho, na hivyo kutufanya tuwe watakatifu na kuishi milele.

YOHANA 6:57-59
57 „Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; Kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi. 58 Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si kama mababa walivyokula, wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi milele. 59 Maneno hayo aliyasema katika sinagogi, alipokuwa akifundisha, huko Kapernaumu.”

Kristo anatueleza habari ya kuishi ndani ya Mungu mwenye enzi, aliye Baba hai. Yeye yupo tangu milele hadi milele Baba wa upendo wote. Kristo aishi ndani ya Baba, Wala haishi kwa ajili yake mwenyewe, bali kwa ajili ya Baba. Maana ya uhai wake si kwa kuridhisha uwezo wake, bali kwa utii kamili kwa Baba aliyemzaa tangu milele. Mwana humtumikia Baba, wakati Baba humpenda Mwana na kufanya kazi kikamilifu kwa njia ya Mwana.

Yesu alifunua siri ya umoja wake na Baba mbele ya wapingaji wake waliokasirika. Aliwapa mafunuoya juu sana akisema,”Jinsi niishivyo kwa ajili ya Baba na ndani yake, ndivyo natamani kuishi kwa ajili yenu na ndani yenu. Kwa kusudi mweze kuishi kwa ajili yangu na ndani yangu:” - Mpendwa ndugu, uko tayari kwa ajili ya kiungo hiki cha kimoyo na Kristo? Utamkubali na shabaha na nguvu zote za maisha yako, au utasema hapana? Unatamani kufia maisha ya ubinafsi, ili Bwana apate kuishi ndani yako?

Kristo hakuja na matengenezo ya kufaa, wala hatutumii afya ili kutusaidia. Hapangi maendeleo ya jamii au ya vijijini, hapana! Anabadilisha mioyo, ili watu wapate kuishi maisha ya kimungu siku zote. Alitolea kwa waumini wake sehemu ya utukufu wake. Hivyo anaumba mtu mpya asiyekufa, anayeishi, anayependa na anayetumika. Lengo lake ni Mungu.

Rudia sura ya sita, ukahesabu ni mara ngapi Yesu anapotamka maneno matatu: “Baba”, “Uhai” na “Ufufuo” pamoja na maneno yanayotokana na hayo. Kwa haraka utashika kiini cha injili ya Yohana. Mwumini wa Kristo huishi katika Roho ya Baba, akiendelea kusogea kwenye ufufuo wa utukufu.

SALA: Bwana Yesu Kristo, tunakushukuru kwa kuja kwako kwetu, na kutujalia uhai wa Baba pamoja na ukamilifu wa furaha. Uwe radhi kwa dhambi zetu na ututakase, ili tuweze kukutumikia kwa uvumilivu na upendo, tukufuate kwa unyeyekevu, na tusiishi kwa ajiili yetu tu.

SWALI:

  1. Kwa nini Yesu aliwaambia wasikilizaji wake kwamba, lazima wale mwili wake na kuinywa damu yake?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on October 07, 2013, at 11:53 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)