Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 046 (Sifting out of the disciples)
This page in: -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
B - Yesu ni chakula cha (mkate wa) uzima (Yohana 6:1-71)

5. Kupepetwa kwa wanafunzi (Yohana 6:59-71)


YOHANA 6:59-60
59 “Maneno haya aliyasema katika sinagogi, alipokuwa akifundisha huko Kapernaumu. 60 Basi watu wengi miongoni mwa wanafunzi wake waliposikia, walisema, Neno hili ni gumu, ni nani awezaye kulisikia ?”

Mazungumzo haya kuhusu mkate wa Mungu na kulishwa mwili wa Yesu yalitolewa mahali mbalimbali. Alirudia maneno fulani na kusisitiza maana yake hatua kwa hatua. Ila Yohana alijumlisha majadiliano hayo katika mkusanyo moja. Tunamwona Yesu kwenye sinagogi ya Kapernaumu, akifundisha wasikilizaji wake kwa kuzunguka, kwamba yeye ni bora kuliko Musa, na kwamba wamwaminio wote washiriki katika mwili na damu yake.

Mafunuo ya namna hii yalipita ufahamu hata wa wafuasi wake waaminifu. Walianza kuuliza na kuonyesha mashaka. Walikuwa wameelewa kumtii Mungu na kumtumikia, bali walichanganyikiwa na upuzi wa mwili na damu kuliwa na kunywewa. Kwenye kilele cha bumbuazi wao, Bwana kwa huruma zake akafunua akili za wafuasi wake waaminifu, ili waweze kuelewa mfano wa Mkate wa Uzima.

YOHANA 6:61-63
61 “Naye Yesu akafahamu nafsini mwake ya kuwa wanafunzi wake wanalinung’unikia neno hilo, akawaambia, Je, Neno hili linawakwaza? 62 Itakuwaje basi, mmwonapo Mwana wa Adamu akipaa huko alikokuwako kwanza? 63 Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.”

Yesu alitambua mawazo ya wanafunzi wake, wala hakukaripia kuuliza-uliza kwao. Kunung’unika kwao haikuwa kwa sababu ya ukaidi fulani, kama kwa wale ambao hawakumwamini, bali ilikuwa tu kwa kutokuelewa kwao kwa habari ya mifano ya siri za Kristo. Lakini kabla ya Yesu kuwapatia ufahamu, anawaondolea kwanza fumbo la mfano huo, maelezo kamili ya mpango wa kuokoa ulimwengu,

Yeye hatawafia hivi hivi tu, ili wale mwili wake kiroho, lakini naye atapaa kwa Baba, ambako kutoka kule alishuka. Ndiye yeye aliyetoka mbinguni, bali hatabaki ulimwenguni petu. Waliwahi kumwona akitembea juu ya maji ya ziwa, wakatambua kwamba yeye anapita uwezo wa binadamu. Atapaa kwa Babaye, ili apate kumimina Roho yake juu ya wafuasi wake. Hii ndiyo kusudi la kifo chake na shabaha ya kuja kwake ulimwenguni. Hivyo, zawadi yake kwao haikuwa kipande cha nyama yake, bali anakuja ndani ya mioyo ya wafuasi wake. Sio mwili wake hasa, bali Roho Mtakatifu wake anakuja kuingia ndani yetu.

Yesu aliwaonyesha kwamba, mwili au nyama haina faida. Tangu asili tuliumbwa wazima na kamili, lakini mawazo yetu na kuishi kwetu yalibadilika kuwa ya kuasi. Ndani ya miili yetu hatupati namna ya kuishi kweli, ila kwa kutenda mabaya tu. Hata mwili wake Yesu ulielekea madhaifu ya kibinadamu, hata akatamka: “Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu” Math. 26:41

Mungu asifiwe, Yesu alikuwa na Roho Mtakatifu nafsini mwake kila wakati. Kuwepo kwa Roho huyu ndani yake ilikuwa ndiyo siri ya maisha yake. Alitamani kutujalia na sisi ushirikiano huo wa Roho na mwili kwa njia ya kifo chake, kufufuka na kupaa kwake, na kutawala kwa Roho wake Mtakatifu ndani ya miili yetu midhaifu. Mapema alikuwa amemsisitizia Nekodemo kwamba, maji na Roho itatuwezesha kuingia katika Ufalme wa Mungu, kwa kurejea ubatizo wa Yohana na kubatizwa na Roho wakati wa Pentekoste. Katika maelezo yake kuhusu mkate wa uzima, Kristo aliwaelezea wanafunzi wake kwamba, atawajia na kuwa ndani yao wanaposhiuriki Ushirika Utakatifu: Kwa hali ya kwamba, alama hizi za mkate na divai hazisaidii kitu, isipokuwa Roho Mtakatifu ametujia kwanza. Ni Roho Mtakatifu tu anayehuisha - mwili hauna thamani . Roho wa Kristo tu ndiye anayetuhakikishia kuwepo kwake Bwana ndani yetu waumini.

Jinsi gani Roho Mtakatifu anatujia? Ndiyo swali la ufunguo kwa wote wanaojitayarisha kushiriki mwili na damu yake, ili kuishi na umoja kamili na Kristo. Yesu anajibu kwa urahisi swali hilo: „Sikiliza maneno yangu, fungua moyo wako kwa utajiri wa injili“. Kristo mwenyewe ni Neno la Mungu; yeye askilizaye maneno yake na kumtegemea, atajazwa na Roho Mtakatifu. Ujaze shauku yako na nguvu ya Mungu kwa kujifunza kimoyo maneno mengi ya Maandiko. Tegemea kabisa ahadi zote za Mungu, kamata kabisa yote aliyoyathibitisha, na utakuwa na nguvu zaidi ya wavumbaji na maajabu yao. Maana kwa neno la Kristo linalookoa Mwumbaji wa ulimwengu wote atakujia, akikujalia uhai wake na enzi yake.

YOHANA 6:64-65
64 „Lakini kuna wengine miongoni mwenu wasioamini. Kwa maana Yesu alijua tangu mwanzo ni nani wasioamini, naye ni nani atakayemsaliti. 65 Akasema, Kwa sababu hiyo nimewaambia ya kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.”

Wengi waliomfuata Yesu walishindwa kuelewa jambo hilo kuu, wakamwacha. Mazungumzo kuhusu kula mwili wake na kunywa damu yake ilikuwa ni kiini cha huduma yake kule Galilaya, pia ilikuwa ni sababu ya wafuasi wengi kuachana naye. Basi hesabu ya watoro ilikuwa dogo kuliko ilivyotazamiwa kwa maoni ya kibinadamu, yaani walioshindwa kumtegemea Yesu bila hoja. Walishindwa kushika ukweli wa uungu wake, wala hawakuthubutu kufanya agano naye kutokana na msingi wa utoaji wake.

Yesu aliwaeleza wanafunzi wake kwamba, baadhi yao watakuwa kinyume cha Roho yake, kwa kumfungia nje. Bwana alimwona kila mmoja wao hadi ndani ya maoni ya moyo wake. Alifahamu kabisa udanganyifu wa Yuda Iskariote, aliyejiunga na kundi la wanafunzi wake tangu mwanzo. Yuda hakuwa tayari kujifungua kabisa kwa Roho wa upendo wa Yesu. Yesu alielewa hayo wakati alipoongea habari ya mwili wake kuteseka, kwamba mmoja wa hao waliokuwepo atamsaliti, ili atwishwe hatua gumu hii ya kuuawa.

Kwa kujumlisha, Yesu akarudia siri hii kwamba, hakuna awezaye kumwamini mbali na kusaidiwa na Roho wa Mungu ndani yake. Hakuna awezaye kumwita Yesu “Bwana” isipokuwa kwa msaada wa Roho. Imani yetu sio kibali chetu tu, bali ni umoja wa binafsi naye Yesu, inayofanyika na Roho. - Fungua moyo wako kwa mvuto wa Roho huyu wa kibaba, wala usikatae ukweli wowote wa Yesu. Ndipo utajaliwa kuja kwake juu yako na kubaki nawe daima. Yeye ndiye Mkate wa Usima uliotayarishwa kwa ajili yako.

SWALI:

  1. Jinsi gani huyu Roho mtoa Uzima alikuwa ameunganika na nafsi ya Yesu?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on October 07, 2013, at 11:54 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)