Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 035 (God works with His Son)
This page in: -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish? -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
A - Safari ya pili kwenda Yerusalemu (Yohana 5:1-47) -- Neno Kuu: Kutokea kwa uadui kati ya Yesu na Wayahudi

2. Mungu afanya kazi na Mwana wake (Yohana 5:17-20)


YOHANA 5: 17-18
17 “Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi. 18 Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo, alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu.”

Kabla ya ule uponyaji pale Bethzatha, kule kumpinga Yesu bado ilikuwa kiasi kidogo. Lakini baada ya hapo upinzani ulizidi. Maadui zake walipanga kumwua. Kwa hiyo mwujiza huo ulikuwa ni sababu ya kubadili uhusiano na Yesu. Kuanzia hapo Yesu alikuwa amedhulumiwa na kuwekwa kwenye orodha ya watafutwa. Lakini ni nini hasa jambo la kumgeukia hivyo?

Mgongano ulitukia kati ya maandamano ya upendo wa Yesu na mamlaka ya sheria zao katika ukali wake. Watu wa Agano la Kale walikuwa wakiishi kama hali ya gerezani. Hukumu nyingi zilitolewa kwa kuwahusisha watu kwa kutokushika sheria kikamilifu kabisa; maana kuhesabiwa haki waliamini inatokana na matendo safi. Wacha Mungu waliangalia sana wasivuke maagizo madogo madogo ya kila wakati na hivyo kujipatia kibali tukufu. Kushika sheria ikapata umuhimu na kuendeleza hali ya kujipenda na kuishi bila upendo kwa wengine. Kwa sababu hili taifa waliishi na agano na Mungu na kuhesabiwa kuwa ni jambo zima la ushirikiano, wale wasimamizi walijaribu kumsukuma kila mtu kushikamana na maagizo yao mengi yasiohesabika. Jambo lililokuzwa juu ya mengine yote ilikuwa ni kukataza kazi siku ya Sabato. Kwa vile Mungu alipumzika siku ya saba baada ya kazi yake ya uumbaji, basi watu walikataliwa kutenda kazi yoyote siku hiyo ya kuabudu, hata kwa tisho la hukumu ya kufa.

Hivyo sabato ikafanywa kuwa alama ya mapatano kati ya Wayahudi na Mungu wao. Ikawa ni dalili ya kuwepo wake kati yao, kana kwamba hakuna dhambi yoyote iliyotendeka nao kinyume cha Mungu iliyoweza kudhuru shwari hili.

Jesu alikuwa na jibu rahisi kwa Mafarisayo waliokataa kuvunja kwake kwa sabato, kulichoamua kama Mungu yuko nao au siyo. Tunasoma neno la „kazi“ na yanayotokana nayo - kama vile kufanya kazi - mara saba katika maelezo ya Yesu kwa Mafarisayo. Jibu lake kwa shauku yao ya uhalali ilikuwa kushuhudia jinsi Mungu afanyavyo kazi katika upendo wake kwa watu. Jinsi gani Mungu angeweza kupumzika hadi sasa baada ya kazi ya uumbaji wake, lakini sasa hutenda kazi bila kupumzika? - Tangu dhambi kuingia duniani na kifo kudhuru viumbe vyote, na ulimwengu mzima kuvunjika kuacha asili yake, tangu hapo Mungu ameshughulika kwa bidii kuwaokoa wanaotanga-tanga na kuwarudisha waasi ndani ya ushirikiano wake. Utakatifu wetu ndiyo shabaha yake, na tuweze kutambua usafi wa upendo wake kwetu.

Uponyaji kwenye Sabato ndiyo picha ya kazi ya Mungu hasa. Yesu alihubiri neema na kutenda matendo ya upendo, hata kama kazi hii ilionekana kuwa kinyume cha sheria. Upendo ndiyo ukamilisho wa sheria. Uponyaji kwenye Sabato ilikuwa ni kushambulia utawa wao wa kinyume na bila upendo.

Basi Wayahudi walilia: “Yesu anavunja Sabato! Tusaidieni! Nguzo za agano letu zinakatika-katika. Huyu adui wa sheria anatia unajisi, akajifanya mwenyewe kuwa mtoa sheria mpya, ni hatari kwa taifa letu.“

Hakuna aliyeshughulika kuona upendo wa Yesu kwa wasiojiweza, wala hawakutambua ushindi wake hapo duniani. Walibaki katika upofu wao na ushupavu wa kidini. - Ndugu, usishangae kama hata siku hizi watu wanashindwa kumtambua Yesu kuwa ndiye Mwokozi, ni kwa sababu ya ushupavu wa namna hii.

Wayahudi nao walikuwa wamechemka dhidi ya Yesu kwa sababu ya maneno ya kumtukana Mungu, waliyoyafikiri kusikia kwake kwamba Mungu ndiye Baba yake. Kwao hili lilisikika chafu. Hivyo wakalia: „Mungu ni mmoja; hana mwana! Namna gani Yesu aweza kumwita Mungu kuwa baba yake?“

Msimamo huo unadhihirisha kutokutambua kwao; hawakuishi ndani ya mafunuo ya kiroho, wala hawakujishughulisha ndani ya maandiko. Maana mle imo utabiri wa wazi kuhusu ubaba wa Mungu. Mungu aliwaita watu wa agano lake „Mwanangu“ (Kut.4:22 na Hosea11:1). Na huku taifa la Waisraeli kumwita Mungu “Baba” (Kumb.32:6, Zab.103:13, Isa.63:16, Yer.3:4,19 na 31:9). Mungu naye alimwita Mfalme aliyeamini “Mwanangu” (2.Samw.7:14). Ila hakuna mtu binafsi wa taifa la agano aliyeweza kuruhusiwa kumwita Mungu “Baba”. Hii ilikuwa haiwezekani kwa mawazo ya kiyahudi na hivyo kuhesabiwa kuwa ni majivuno ya kupita kiasi. Wayahudi walifahamu ahadi ya kwamba Yesu, aliye Masihi, atakuwa wa asili tukufu, atakayeleta uzima wa milele. Hivyo chuki yao kwa Yesu ilionyesha wazi kutokuamini kwao kwamba yeye ndiye Masihi.

Yesu aliitikia woga wa Wayahudi kwa maneno yake kwa kuwaeleza wazi kwamba, anatenda kazi ile ile ya Baba yake, tena kwa hekima na upendo. Yesu akahakikisha kwamba, aliweza kutenda mambo yote na kuwa sawa na Mungu. Itikio la Wayahudi kwa mawazo kama hayo ilikuwa ya kufarakisha na ya ukorofi. Yeyote anayejiinua mahali pa Mungu, lazima aondolewe. Wayahudi walimchukia Yesu kama mtia unajisi na mwenye kustahili kufa.

YOHANA 5:19-20
19 “Basi Yesu akajibu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile. 20 Kwa kuwa Baba ampenda Mwana, naye humwonyesha yote ayatendayo mwenyewe; hata na kazi kubwa zaidi kuliko hizi atamwonyesha, ili ninyi mpate kustaajabu.”

Yesu aliwajibu Wayahudi akijaa upendo, akakabiliana na chuki zao kwa kuwaelekeza kwa kazi ya upendo wa Mungu. Ndiyo, Mwana hufanya kazi jinsi Baba afanyavyo kazi. Yesu hafanyi kazi peke yake. Umoja wake na Baba ilikuwa karibu sana, jinsi mtoto anavyomwangalia kwa karibu baba yake, akitazama mikono yake aone yanavyotendeka, na hivyo kutenda sawasawa kabisa atendavyo baba. Hivyo Yesu alijinyenyekeza na kurudisha utukufu kwa Baba. Alimheshimu sana Babaye. - Tutambue kwamba sisi tu watumwa tusiofaa, lakini tunaoitwa kutukuza jina la Baba yetu, alivyofanya Yesu.

Kwa kujikana na katika unyenyekevu Jesu alipokea mamlaka ya kutenda kazi za Babaye. Sifa zake, majina yake na kazi za Baba ni zake vilevile. Yeye ndiye Mungu kweli na wa milele, mwenye enzi, wa kupenda, mwenye utukufu. Umoja wake na Baba ni kamili.

Mungu Baba ampenda Kristo kwa sababu ya kujikana mwenyewe, asiyeficha lolote kwake. Anashiriki haki zake, mipango na kazi zake na Mwana. Kwa kutamka hayo tunaona thibitisho lililo wazi kabisa kuhusu umoja wa Utatu - umoja wa upendo na wa utendaji. Kwa vile Baba, Mwana na Roho Mtakatifu wanashirikiana katika mambo yote, ingetupasa kutulia kabisa kwa ufahamu kwamba Utatu Utakatifu unatenda kazi bila kukoma - kwa makusudi ya kukomesha vita zote, chuki na ushupavu duniani humu. Tuone jinsi ilivyo kubwa mno utofauti kati ya umoja wa upendo kazini, na upande wa pili kule kutokutenda kitu kwa msimamo wa kisheria.

SALA: Baba wa mbinguni, twakushukuru kwa kumtuma Mwana wako kwetu. Kwa kazi zake ulituonyesha unayoyatenda wewe na pia wewe ulivyo. Utuweke huru na matendo yote ya kisheria na tuchague matendo ya upendo. Tuwe tunaungama ushupavu wetu na tunakusihi kwa ajili ya wale walio vipovu kiroho, ili wapate kutambua uhuru wa upendo wako na wajikabidhi kwako katika utii na unyenyekevu.

SWALI:

  1. Jinsi gani na kwa nini Mungu hufanya kazi na Mwana wake?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 31, 2013, at 10:06 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)