Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 026 (The Baptist testifies to Jesus)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
C - Kristo kutembelea mara ya kwanza mji wa Yerusalemu (Yohana 2:13 - 4:54) -- Neno Kuu: Kuabudu kwa kweli ni nini?

3. Mbatizaji anamshuhudia Yesu kama Bwana Arusi (Yohana 3:22–36)


YOHANA 3:22-30
22 “Baada ya hayo Yesu na wanafunzi wake walikwenda mpaka nchi ya Uyahudi; akashinda huko pamoja nao, akabatiza. 23 Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa. 24 Maana Yohana alikuwa hajatiwa gerezani. 25 Basi yalitokea mashindano ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi mmoja juu ya utakaso. 26 Wakamwendea Yohana, wakamwambia, Rabi, yeye aliyekuwa pamoja nawe ng’ambo ya Yordani, yeye uliyemshuhudia, tazama, huyo anabatiza na watu wote wanamwendea. 27 Yohana akajibu akasema, Hawezi mtu kupokea neno lolote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni. 28 Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nalisema, Mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake. 29 Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi. 30 Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.”

Baada ya sikukuu ya Pasaka Yesu alitoka Yerusalemu na kuanza kubatiza.Wanafunzi wake walifahamu haja ya unyenyekevu kabla ya hatua ya kuzaliwa mara ya pili, na kwamba bila ya ungamo ya dhambi, wokovu hauwezikani. Ubatizo kwa ajili ya ungamo ya dhambi ilionyesha unyenyekevu, na kwa njia hii mwenye kutubu alionyesha hamu yake ya kuingia katika agano mpya na Mungu.

Mbatizaji alikuwa amebadilisha mahali pa huduma yake alipohamia Ainoni, chanzo cha bonde la Yordani kaskazini. Watu wakamwendea Yohana na kumwaga mioyo yao kwake; basi akawabatiza, na hivyo kuwatayarisha wakutane na Yesu.

Yesu hakurudi Galilaya moja kwa moja baada ya Pasaka, lakini alianza kuwabatiza wenye kutubu penginepo nchini. Akiwa na madaraka zaidi, watu wengi zaidi walimwendea yeye kuliko Yohana. Matokeo yake yakawa majadiliano kati ya hivi vikundi viwili. Hoja ilikuwa hii: Yupi kati ya hao viongozi wawili ni bora kwa ajili ya shabaha ya kuoshwa dhambi ? Nani kati yao yu karibu zaidi na Mungu? Hii ilikuwa ni swali muhimu sana, kwa sababu walifikiri sana wakitoa maisha yao kwa Mwalimu wa chaguo lao la mwisho. Eti wewe ndugu, umetafakari sana namna ya kujitoa kwa Mungu ?

Mbatizaji alijizuia jaribu kubwa sana. Hakuonea wivu mafanikio makubwa ya Yesu, lakini alitambua kwamba huduma yake ilikuwa na mpaka. Kwa unyenyekevu alikiri : “Mtu wa kawaida hawezi kufaulu kazi njema namna hii peke yake. Kama Mungu amemjalia tu nguvu hii, baraka na matunda ya kiroho, ndipo ataweza.” Kinyume cha hayo, sisi huwa tunajisifu wenyewe, uwezo wetu wa kiroho, sala na maneno ya kuvutia. - Wewe, ukiwa umepokea kipawa cha kiroho, basi ni toka kwa Mungu. Bado u mtumwa, bila kustahili lolote hata kama unafanya yote yanayotakiwa na Mungu. Mbatizaji aliendelea kuwa mnyenyekevu, wala hakudai uwezo wowote zaidi ya nguvu zake za kawaida, bali alimtukuza Mungu peke yake.

Tena Mbatizaji alishuhudia kwa wanafunzi wake kwamba, yeye siye Masihi. Angaliweza kutazamia mapokezi ya kumtukuza, kama angalienda Yerusalemu, lakini hayo hayakutokea. Yesu basi akaendelea kubatiza. Hivyo Mbatizaji alichanganyikiwa, hata hivyo akadumu kuwa mtiifu. Alikuwa ni mtangulizi wa Kristo tu akiandalia mapito yake. Yohana naye akaendelea kuwa mwaminifu kwa mafunuo aliyoyapata. Akashuhudia kwamba Yesu ndiye Bwana Arusi, aliyewatunza waliotubu na kusafishwa na maji ya ubatizo kuwa kama Bibi Arusi yake. - Siku hizi Roho Mtakatifu anaumba umoja huu wa kiroho, jinsi Paulo alivyoweza kutamka: “Sisi tu viungo vya mwili wa Kristo naye ndiye kichwa chetu; sisi tu mmoja na yeye.” Kristo siye mhukumu wetu tena, bali Mwokozi wetu, na kwa mfano mzuri yeye ni Bwana Arusi wetu. Picha ya furaha ya arusi inatuonyesha tumaini letu lenye furaha ndani ya Kristo.

Basi Mbatizaji akasimama kwa umbali, akifurahia hali ya kukua kwa kundi la wafuasi wa Kristo, yaani Kanisa. Lakini alisimama karibu na Yesu, kuliko kujichanganya na wafuasi wake mwenyewe. Alikubali kwamba yu rafiki mwaminifu kwake. Na huku akiendelea peke yake kubaki jangwani, Yesu moja kwa moja akaingia Mji Mkuu, alipofanya ishara zake na kuhubiri hotuba zake. Mbatizaji alitambua maendeleo ya Ufalme wa Mungu akafurahia sana. Sauti na ukuu wa Bwana Arusi zilimpendeza. Habari za kufaulu kwa Kristo kwake ilikuwa kama muziki ya mbinguni. Hivyo rehema laini ya Kristo ililainisha taabu za Mbatizaji wakati wa siku za mwisho wa huduma yake. Alishangilia kama mshiriki katika sikukuu ya arusi.

Hapo Yohana akawa tayari hata kufa, tofauti na nia ya kukuza kundi la wafuasi wake. Aliona bora kupungua na kupotea, ili Kristo na Kanisa lake lipate nafasi ya kukua.

Ndugu msomaji, ni nani anayeongoza mikutano yako? Je, kuna mvutano kati yenu kwa ajili ya uongozi ? Na wewe, unatoa nafasi kwa wengine? Kuwa wa mwisho, ili Kristo apate nafasi ya kukua na kutawala ndani yako? Ungana na Yohana na kusema: “Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua”.

SWALI:

  1. Kwa maana gani Kristo anafananishwa na Bwana Arusi?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 08, 2013, at 11:41 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)