Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 080 (A Warning against the Deceivers)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek? -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish? -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
Maongezo kwa SEHEMU ya 3 - Maelezo ya pekee juu ya msimamo wa Paulo kwa viongozi wa kanisa la Rumi (Warumi 15:14 – 16:27)

6. Onyo dhidi ya wadanganyi (Warumi 16:17-20)


WARUMI 16:17-20
"17 Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao. 18 Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu. 19 Maana utii wenu umewafikia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wasio na hatia katika mambo mabaya. 20 Naye Mungu wa amani atamponda Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi."

Paulo bila shaka alipata kutambua, wakati alipofunga barua yake kwamba, watu washupavu wa kundi la wana-sheria wa Musa walianza kuwaita Wakristo katika mikutano ya kanisa kule Rumi washike sheria za Musa na mapokeo waliyorithiwa kutokana na mwenendo wa Kiyahudi. Sheria hizo zilijumlisha jambo la kujizuia na vyakula kadhaa, kufunga kwa siku fulani au miezi, kushika Sabato badala ya Jumapili, na kuzishika mistari fulani ya kiyahudi kabla ya zile za Kikristo.

Mapema Paulo alitambua hali ya kweli ya jaribu hilo, ambalo ibilisi alizua katikati ya makanisa yale ya kinyumbani, na hatari ya kugeukia mafundisho ya uongo yaliyojenga juu ya matendo mema, na kushika sheria, bila ya kukumbatia neema ya Mungu kipekee. Msalaba wa Kristo, kufuatana na mafundisho hayo ya uongo, haitoshi kwa ajili ya kupokea wokovu, bali ingetupasa kutegemea kwenye bidii yetu sisi wenyewe, pia kwa kushika sheria za Musa, na kuzifuata bila kukosa.

Paulo aliona shambulio la ibilisi dhidi ya haki ya Kristo, ambaye amewasamehe watenda dhambi wote makosa yao, kufuatana na tamko lake hilo: „Yeye atakayeamini na kubatizwa ataokolewa; lakini asiyeamini basi atahukumiwa“. Aliwaeleza wale waliotafuta kupinda neema ile ya bure katika Kristo kwamba, ndiyo wale walioleta magawanyo na ya kushambulia, kinyume cha fundisho la kweli, ambao kwa ajili yao nabii Daudi alisema: „Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, hakuna atendaye mema, la! Hata mmoja.“ (Zaburi 14:3).

Paulo alieleza hali hii ya ufilisi wa ubinadamu katika waraka wake kwa Warumi, akikazia njia ya Kristo kuwa ndiyo njia ya pekee kwa wokovu wetu (Warumi 3:9-24). Baada ya maelezo hayo, wadanganyi wa kiyahudi wakaja na kufanya bidii kubomoa yale ambayo Paulo aliyaleta, tena kabla ya kufika kwa waraka huu kwa kanisa la Rumi. Kwa hiyi, Paulo alionya kanisa la Rumi juu ya hao wadanganyi waongo.

Basi kabla ya hapo, katika mkutano wa kwanza wa mitume kule Yerusalemu, na baada ya mahojiano makali na wale waliokuwa washupavu kuhusu sheria kati ya waumini, Paulo alisema wazi: „Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu kwa kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua. Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao“ (Matendo ya Mitume 15:10-11).

Wakati Petro, kiongozi wa mitume, alipojaribu kumzuia Yesu asielekee kwenye mateso na kusulibiwa, Yesu alimwambia: „Nenda nyuma yangu, Shetani! U kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu“ (Mathayo 16:23).

Juhudi zote za wanadamu za kufuta msalaba wa Kristo, ndipo kusimamisha wokovu wao juu ya jitihada zao wenyewe, zilishindwa kabisa. Hayo ni madanganyo ya kishetani tu kwa asili yao. Kwa namna iyo hiyo, bidii za kufufua shabaha ya utu wema (Humanism) inajionyesha vizuri kabisa, lakini hata hayo ni ya kiasili, dhidi ya neema ya Mungu. Yeyote atafutaye kufikia hali ya Paradiso kwa njia ya kushika sheria, kukataa ukweli wa kihistoria ya usulibisho, pia na ukombozi wa Kristo chenye thamani mno, basi amekumbwa na kudanganywa na shetani.

Katika waraka wake Paulo aliwaelekea waumini wa Rumi waliochanganyikiwa akiwaambia: „Mwe waangalifu kwa wale wadanganyi, mkajiepushe nao, wala msiwaruhusu kusema katika vikundi vyenu vya manyumbani, maana hamkuelewa yale ambayo Yesu alimaanisha alipotamka „Ilisemwa kwa wale wa zamani….. Lakini mimi sasa nawaambia….. Wale wadanganyao wanaishi katika zamani za kale, wala hawajasogea ndani ya wakati wa sasa, wakati wa neema. Basi, mshikamane na Msulibiwa aliyefufuka, nanyi mtaishi milele“.

Paulo akaongeza kwenye onyo lake, akiwasifu na kuwapa heshima hao waumini wa Rumi, akiwaambia: „Nafurahi kwa sababu ya imani yenu ya kweli na upendo wenu wa kiroho, kwa sababu mmejifunza utii, chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, nanyi mliifanyia kazi katika maisha yenu ya kila siku; na ukweli huu wa kiroho umepata kujulikana katika makanisa yote ya Uyunani. Kwa sababu hiyo, tafuteni hekima kutoka kwake Yesu aliye hai kwamba, mweze kutofautisha mema na mabaya. Fanyeni yale yaliyo safi na mwache upumbavu wa mabaya. Mtakieni Bwana aliye hai kila wakati, awajalie uongozji unaojengwa kwenye injili, ili yeye awaongoze kwenye imani ya kweli, pia na mkaishi kwa amani na Mungu“.

Baada ya mnaneno hayo ya kutia moyo, Paulo akiwa katika uchungu wake takatifu, akawaahidi kwa tamko lake la pekee, ambalo hatulikuti penginepo ndani ya Biblia: „Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi“ (Warumi 16:20). Tamko hilo dhahiri linamaanisha kwamba, Mungu wa amani, ambaye kutoka katika ukamilifu wa amani ndani yake, atamwaga amani yake ndani ya mioyo yao. Huyu Mungu, ambaye hawezi kukubali machafuko, atamshinda shetani wakati Kristo atakaporudi kutoka mbinguni. Paulo alilithibitishia kanisa la Rumi kwamba, lilipata kuwa mwili wa kiroho wa Kristo, na kwa sababu hiyo litatambua kimatendo, jinsi Mwenyezi atakavyomwangamiza yule mwovu kabisa chini ya miguu yao, maana wamo ndani ya Kristo na Kristo ndani yao. Hamwezi kumshinda yule mwovu kwa nguvu zenu, bali Mungu atamtupa chini ya miguu ya Mwana wake mpendwa, maana ndani yake mnashiriki onyesho la utukufu wake wa kung‘aa waziwazi. (taz. Zaburi 110:1)

Paulo aliangalia yote kwa hali halisi. Alimwomba Bwana Yesu awalinde waumini wa Rumi na majaribu ya shetani, pia na kuwaimarisha ndani ya neema yake, maana neema ndiyo ufunguo kwa ridhaa ya Baba, ya Mwana na ya Roho Mtakatifu.

SALA: Ee Bwana Yesu, ulitufundisha kuomba: „Usitutie majaribuni, bali utuokoe na yule mwovu“. Tufunulie macho ya mioyo yetu, ili tuone jinsi unavyotawala juu ya yule mwovu, na utulinde na kila namna ya jaribu la kutuokoa sisi wenyewe, maana wewe tu kipekee ni Mwokozi wetu. Amina.

SWALI:

  1. Ni wapi ambapo shetani anapokaza majaribu yake kwa uangalifu?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 17, 2022, at 01:11 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)