Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 070 (Practical Result of the Knowledge that Christ is coming again)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek? -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish? -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 3 - HAKI YA MUNGU HUJIONYESHA MAISHANI MWA WAFUASI WA KRISTOS (Warumi 12:1 - 15:13)

7. Matokeo halisi kutokana na ufahamu kwamba, Kristo atarudi tena (Warumi 13:11-14)


WARUMI 13:11-14
"11 Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini. 12 Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na tuzivae silaha za nuru. 13 Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu. 14 Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake.“

Mtume anataja ndani ya waraka wake kwamba, kanisa kule Rumi lilishiriki katika kutazamia kurudi kwake Kristo karibuni sana. Waumini walitambua ishara za siku za mwisho, na ule ukaribu wa nguvu ya roho ya yule Mpinga Kristo ndani ya Makaisari wa kirumi. Walitazamia kutokea kwake Mwana wa Mungu kwa utukufu, na kipeo cha furaha kwa kuinuliwa juu kwenye nchi yao ya mbinguni.

Mtume aliwataka wafuasi wa Kristo wasiendelee katika kutokuangalia kwao kiroho, bali watambue hali ya kujibidiisha kwao kiroho, kisha watambue wokovu wao kamili, ulioanza kwao wakati Roho Mtakatifu alipoanza kuwatawala kama dhamana ya ukombozi wao. Ndiyo, yeye hutukumbusha habari ya kurudi kwake Kristo hivi karibuni, atakaye kutuvisha na nguvu yake, utukufu na upole. Usiku wa ulimwengu kweli unakaribia kwisha, na kule kupambazuka kunatujulisha habari ya siku mpya, ambayo nuru yake hakika itang‘aa. Pamoja na hayo, Paulo anatambua kwamba, maisha yetu hata hivyo ni matayarisho kwa ajili ya kutokea kwa wakati wa ahera, ambao utaonekana katika ushirikiano wa Baba na Mwana na katika enzi ya Roho Mtakatifu.

Ndipo basi, kama matokeo ya ufahamu huo, mtume anasema: „basi tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru. Ondoeni dhambi kutoka katika maisha yenu. Mjipambe na sifa za Kristo katika nguvu ya Roho yake“. Ufufuo huo unamaanisha kujikinga na giza maishani mwetu, na pia ndani ya makanisa yetu. Injili na matunda ya Roho Mtakatifu lazima yajionyeshe ndani ya maisha yetu, pia na ndani ya masumbufu.

Paulo alifahamu makusudi ya kweli ya watu wale waliokosa kumfahamu Mungu, walioendeshwa na nia zao za kimwili na tamaa zake kama wanyama. Walikuwa wanakula na kunywa na kuzaa; na pamoja na hayo walizama ndani ya chuki, uchoyo na uchafu. Upendo bila Mungu ni ovu, upotovu na ngumu; ndipo ambapo kila mmoja anajichukulia ya kwake, na bila haya anatumia udhaifu wa wengine kwa ajili ya faida yake ya binafsi.

Mtume alipata kuona mwenyewe masababisho ya watu wa giza; lakini wakati uo huo alipata kuona maisha mapya ndani ya Kristo, akawataka waumini wa Rumi wasiridhike tu na imani yao ndani ya Kristo, bali wamvae kabisa kiroho. Kumvaa Yesu kunatokeza hali ya kutimiza tabia zake, kutembea ndani ya kiini chake, kutii maagizo yake na kumruhusu Roho yake ashike mamlaka ya utawala na uongozi wa maisha, ili matunda ya Roho hiyo yapate kuonekana ndani yao.

Basi na tukuulize swali, Ndugu mpendwa: Je, wewe umo ndani ya Kristo, au bado unaendelea na uchoyo, ukiishi kwa ajili yako tu, wala si kwa ajili ya Bwana wako? Yesu amekuweka huru na kiburi chako, namna yako ya kujitegemea tu mwenyewe, kuamini mali yako pamoja na kujihusisha na tamaa. Mvutano kati ya Roho Mtakatifu na mwili wetu pamoja na mawazo machafu ndiyo kiini cha matayarisho yetu kwa ajili ya kurudi kwake Kristo.

Kwa sababu hiyo, mtume anawakaribisha Wakristo wajivishe na silaha za kiroho; sio kwa kupigana na maadui, bali kwa kushinda majaribu na tamaa za mwili, ndipo kujazwa na upendo na utakatifu wa Kristo.

SALA: Ee Baba wa mbinguni, twakuadhimisha kwa sababu Mwana wako Yesu alitujalia mbele yetu mfano wa maisha mema na kufaa. Utusaidie kwa nguvu ya Roho wako Mtakatifu tupate kumvaa Kristo, na tufaulu kuwa waumini waaminifu, tukiwa tumejitayarisha kwa ajili ya kurudi kwake Mwokozi wetu mpendwa, aliye Bwana wa mabwana.

SWALI:

  1. Maadili ni yapi, ambayo ufahamu wa kurudi kwake Kristo hivi karibuni, kunatusukuma kuyavaa maishani mwetu?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 17, 2022, at 12:12 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)