Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 036 (Freedom from the Law)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
D - Uwezo Wa Mungu Hutuokoa Na Nguvu Ya Dhambi (Warumi 6:1 - 8:27)

2. Uhuru kutoka kwa sheria inarahisisha ukombozi wetu na dhambi (Warumi 6:15-23)


WARUMI 6:15-22
"15 Ni nini basi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sheria, bali chini ya neema? Hasha! 16 Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki? 17 Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake; 18 na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki. 19 Nasema kwa jinsi ya kibinadamu, kwa sababu ya udhaifu wa miili yenu. Kwa kuwa kama mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa. 20 Kwa maana mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki. 21 Ni faida gani basi mlivyopata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti. 22 Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa , na mwisho wake ni uzima wa milele.“

Maswali ya ujanja ya Wayahudi aliyasikia yakilia tena ndani ya kumbukumbu ya Paulo: Je, tutende dhambi, kwa sababu hatuwi chini ya sheria, bali tumeokolewa kwa neema ?

Paulo alikataa kata kata swali hilo la kishetani, maana lilitengenezwa si kwa Roho Mtakatifu, lakini kwa ajili ya mambo fulani tu. Paulo aliwashuhudia waumini kwamba, kwa mapenzi yao wenyewe walijitoa kabisa kwa kumtumikia Kristo kwa sababu ya upendo wake, na kwa sababu hiyo walipata kuwekwa huru na nguvu ya dhambi na madai ya sheria, wakibeba maisha ya haki ya Mungu ndani yao. Yeyote anayedai habari ya uhuru wa kibinadamu bila kumstahi Mungu atakuwa ni mwongo. Daktari Luther alikuwa akifananisha mtu na punda, alipotoa tamko kwamba, mtu mmoja peke yake hawezi kuishi bila bwana mkubwa, kwa sababu anahitaji fulani ampande na kuchukuliwa naye. - Wewe basi, umepandwa na mmojawapo, ni shetani au Mungu. Mungu anapopata kuwa Mungu wako, nawe unambeba kwa furaha, pia na kumtumikia kwa furaha na uangalifu, ndipa hali ya kukata tamaa, dhambi na nguvu ya mauti yanakoma ndani yako, Badala yake tumaini, amani na uhuru wa kweli ya rohoni yanaanza ndani yako. Kristo atakuwa amekuweka huru - si kwa ajili ya kupata wasiwasi au kujifurahisha tu, lakini kwa ajili ya kumtumikia Mungu, pia na kwa kutenda mema kwa wengine chini ya uongozi wa roho ya hali ya kujaliwa haki. Kwa njia ya utii kwa uongozi wa Roho Mtakatifu dhamiri yako itakuwa inatulia. Bila ushirikiano huo ndani ya Roho wa Kristo utadumu katika hali ya kukata tamaa na taabu.

Kristo mwenyewe alishuhudia kwamba, alibeba nira, iwapo yeye mwenyewe alikuwa huru na kuwa Mungu wa milele. Hata hivyo, kwa furaha alijitwisha nira ya Babaye, na akamtii hadi kufa, tena kifo cha msalabani. Upendo tukufu ulimfanya Yesu kuwa mtumwa wa kupeleka mbali dhambi za ulimwengu. Basi, kwa nini wewe hujakubali kumfuata yeye? Je, wewe unabeba dhambi za marafiki zako na kuteseka kwa sababu ya ulegevu wao? Basi, usikasirike kwa ajili ya swali hilo; lakini weka moyo wako kwenye shabaha ya wokovu wao na wapate kuwekwa huru kiroho. Upendo wa Mungu unakusukuma kwenye ukombozi wa watu wote.

Maisha pamoja na Kristo yanakuongoza kuwahudumia wengi, si kimawazo tu au kwa mhemuko kimoyo, lakini kwa mpango kamili, kwa kujitoa kabisa na kwa nguvu zako zote. Jinsi ulivyotumia zamani muda, fedha na vipawa vyako kwenye mambo ya kujifurahisha tu yasiyofaa, sasa basi tumia uwezo wako wote katika kumtumikia Kristo na wokovu wa watu wengine. Uwafariji wale wanaohuzunika, watembelee wagonjwa, wasaidie walio na njaa, jifunza na wale walio wadhaifu kimasomo, na uwape nuru wale wanaotafuta kujaliwa haki kwa njia ya injili.

Upendo wa Kristo unaoonekana maishani mwa waumini ndiyo tumaini lenye subira ndani ya dunia yetu isiyo na haki. Je, umepata kuwa mtumishi wa Mungu na mtumwa wa upendo wa Mwana wake? Kama ndiyo, basi dhambi haiwezi kuwa na nguvu tena juu yako, kwa vile umepita ndani ya kifo cha ungamo, hali umesulibiwa na Kristo, ndipo umejazwa na Roho Mtakatifu wa kwake na kuimarishwa ndani ya uzima wake wa milele. Basi, unayo tumaini kuu pamoja na wote hao wanaoishi ndani ya Kristo.

WARUMI 6:23
"23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.“

Mstari huu ni kama dhahabu, inajumlisha injili yote kamili, ukitueleza wazi matunda ya mwanadamu wa asili, na upande wa pili hilo jambo kuu linalopatikana kwake Kristo.

  1. Inatupasa kufa kwa sababu tunatenda dhambi. Kifo haikwepeki kwa sababu tunajaa makosa. Na kwa sababu watu wote ni wenye dhambi, wote watakufa. Hii ndiyo tokeo la maisha yetu.
  2. Lakini aaminiye ndani ya Kristo, atapokea zawadi ya Mungu. Zawadi hiyo si shaba au dhahabu, au kitu chochote cha thamani, wala haiwezi kupatikana katika vitu vya asili ya ulimwengu mzima. Badala yake inakuja moja kwa moja kutoka kwa moyo wa Mungu na kwa uhakika itatawala ndani ya mioyo yetu. Yeye anatoa maisha yake kwa wote wale waliosulibiwa pamoja na Mwana wake, ili nao wapate kushiriki utawala wake wa milele. Naye anafanya hivyo, kwa sababu ndiye Bwana wa Mabwana, naye anatawala pamoja na Baba yake na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja, milele na milele.

SALA: Tunakuabudu, Ee Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, kwa sababu umetuondoa kutoka katika uhusiano na dhambi na chuki, ulituweka huru na mapingu ya mauti, ulitubeba hadi kwenye mapana ya baraka ya Kristo, nawe ulitujaza na uhai wa Roho yako Mtakatifu, ili tusife kwa milele, bali tuishi nawe na ndani yako kutokana na neema yako kuu. Amina.

SWALI:

  1. Ipi ni utofauti kati ya mapingu ya dhambi na mauti, na upande wa pili upendo wa Kristo?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 15, 2022, at 12:38 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)