Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 035 (The Believer Considers Himself Dead to Sin)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
D - Uwezo Wa Mungu Hutuokoa Na Nguvu Ya Dhambi (Warumi 6:1 - 8:27)

1. Mwumini hujifikiria mwenyewe kwamba, amefia dhambi (Warumi 6:1-14)


WARUMI 6:12-14
"12 Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake; 13 wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na vyungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki. 14 Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.“

Yule aliyewekwa huru na nguvu ya dhambi na kuimarishwa katika ushirikiano na Kristo, huyu atachukia dhambi, na ataikirihi, na kabisa hataki kuitenda tena. Ndiyo, tamaa zaweza kuwa kali sana, lakini upendo kwake Kristo inayo nguvu zaidi. Yeye asimamaye imara ndani ya injili na kuendelea kwa kudumu katika sala zake, ataona na kupokea nguvu kuzishinda tamaa zote za mwili wake na za rohoni. Maana hajitumikii mwenyewe, au kufuata mafundisho fulani ya ovyo, lakini kwa kukubali kabisa atajizuia na matendo yoyote yasiofaa. Hatasikiliza tena wito wa tamaa hata kidogo, kwa sababu anaendelea katika ushirikiano na Yesu mshindi, ambaye nguvu zake zinazo uwezo kuliko maelekeo ya kifo yote ya mwilini wako. Roho Mtakatifu ataimarisha ndani yako elimu iliyo na hekima kuliko filosofia zote za humu duniani.

Jizuie na matendo yoyote ya ovyo, vitabu, maonyesho ya TV, pia na urafiki usiofaa. Mambo hayo yasikutenganishe na ushirikiano wako na Kristo. Usiamini nguvu ya dhambi zako, lakini umtegemee Kristo na enzi ya wokovu wake.

Umepata kuwa mali ya Mungu. Unapumua Roho yake na umetambua mwenyewe kweli za milele. Hivyo basi, utawezaje tena kutafakari habari ya mapito yako pasipo Mungu? Ujipeleke kabisa kwa Bwana wako kama askari kwa vita takatifu, nawe umkabidhi yeye muda wako, nguvu zako, pia na fedha zako. Sadaka yako kama hii si jambo la lazima, lakini ni pendeleo, ukishukuru, na ukifurahia. Umwulize Bwana wako ni wapi anapokutaka umtumikie, maana mavuno kweli ni tele, ila wafanya kazi ni wachache. Kwa hiyo umwombe Bwana wa mavuno atume wafanya kazi ndani ya mavuno yake. Hata hivyo, usimtumikie Bwana wako kwa haraka haraka na ukaidi, lakini ujinyoshe kwa uongozi wake. Anakusudia kuwainua, kwa njia yako wewe, watu waliokufa dhambini, ili nao wapate kuishi ndani ya maisha yake ya milele. Basi umkabidhi mwili wako, pia na mali yako yote, ziwe silaha za haki kwa ajili ya Mungu.

Daima usisahau kushukuru, maana ulikuwa umekufa ndani ya dhambi, lakini sasa unayo uzima ndani ya Kristo. Leta na vipawa vyako virudi kwa Mungu, ili avitumie kama vyombo kwa ajili ya kuwaokoa wengine. Huyu Mtakatifu anakustahilisha kwake Kristo, naye anakutuma duniani, ili utukuze nguvu ya haki yake hata ndani ya unyonge wako. Usisite-site! Mtume Paulo mwenyewe alijiita mtumishi mfungwa wa Kristo. Hivyo, lini wewe utamfuata kweli, ukitoa maisha yako kwa huduma za Mungu kwa muda wote?

Hao wote wanaotumika, kama vile Paulo, wakiwa ndani ya ushirikiano wa upendo wa Mungu, watatambua nguvu za Roho Mtakatifu kila siku, nao wanatambua mapinduzi ya kwanza yalitendeka ndani ya mioyo yao. Dhambi haikai tena kwa kucheka kwenye kiti cha enzi cha moyo wako, bali Kristo mwenyewe amekuwa mwenye kutawala moyo wako; na kwa kukaa kwake ndani yetu wakati mpya umeanza maishani mwetu. Sasa kutimiza amri zake Mungu haiwi tena wajibu usiowezekana, bali tunatamani kuzitii kwa furaha, huku tukisukumwa na upole wa nguvu ya Roho yake. Kila Mkristo anayo vipawa vya nguvu za neema. Kifo na uchafu hazimtawali tena. Yule wa pekee atawalaye kwenye akili na mioyo yetu ni Kristo pamoja na neema yake kuu.

SALA: Ee Bwana Yesu Kristo, tunakutukuza kila asubuhi na kila jioni, kwa sababu umejifungamanisha na miili yetu ya mauti, ili kutufanya tuwe washiriki katika uzima wa milele. Wewe unatawala ndani ya mioyo na akili zetu: Utufundishe namna ya kuishi kwa hekima, ili tuweze kukusifu wewe na Baba yako wa mbinguni kwa utu wetu wote, nguvu na fedha, pia na tupate kuhesabiwa pamoja na waaminio wote walio watumwa wa upendo wako.

SWALI:

  1. Jinsi gani tutaweza kujileta wenyewe na viungo vya miili yetu vipate kuwa silaha za haki kwa Mungu?

Nami najizoeza katika neno hili niwe na dhamiri isiyo na hatia
mbele za Mungu na mbele za watu siku zote.

(Matendo ya mitume 24:16)

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 15, 2022, at 12:32 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)