Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 037 (Deliverance to the Service of Christ)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
D - Uwezo Wa Mungu Hutuokoa Na Nguvu Ya Dhambi (Warumi 6:1 - 8:27)

3. Kufunguliwa na Sheria inatuweka huru kwa ajili ya huduma ya Kristo (Warumi 7:1-6)


WARUMI 7:1-6
"1 Ndugu zangu, hamjui (maana nasema na hao waijuao sheria) ya kuwa torati humtawala mtu wakati anapokuwa yu hai? 2 Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sheria ya mume. 3 Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine. 4 Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda. 5 Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, zilizokuwako kwa sababu ya torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata mkaizalia mauti mazao. 6 Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko.“

Paulo alitamani sana kwamba, ndugu zake wa asili ya kiyahudi walioamini na kuishi Rumi, wangekubali mafundisho yake kwa heshima kwa ajili ya mauti yao ya kimoyo, na ufufuo wao ndani ya Kristo kama waumini wa kweli. Hata hivyo, Paulo naye alifahamu kwamba, ilimpasa kutoa jibu la wazi kabisa kuhusu msimamo wao kwa habari ya sheria, maana waliona ndani yake maongozi ya Mungu, tena linalozidi mafunuo yote mengine, pia na ukamilifu wa mapenzi matukufu yalivyotolewa kwake Musa. Paulo aliwaambia: Ninyi, ambao mnaifahamu na kuipenda Sheria, mmefungwa nayo jinsi watu wawili wa ndoa wanavyofungwa kwa kifungo cha kuoleana. Na jinsi kifungo hiki cha ndoa inavyofunguliwa kwa kifo cha mmojawapo kati ya hao wawili, ndivyo na ninyi mmefunguliwa na sheria, maana mlikufa ndani ya kifo chake Kristo. Mwili wake uliozikwa unahesabiwa kuwa yenu, ili mauti isiwe na nguvu juu yenu.

Hivyo basi, Kristo naye alifufuka kutoka kwa wafu, basi sasa na ninyi mlio huru, mchagueni huyu Mtawala wa uzima na mfanye maagano mapya naye huyu Mwana wa Mungu. Agano la Kale ilikuwa ni agano la mauti wa kungojea hukumu ya mwisha kutokana na sheria. Sasa ninyi baada ya kuingia katika ushirikiano na Mtawala wa uzima, matunda ya Roho yake yanatokea tele ndani yenu: upendo, furaha, amani, uvumilivu wa muda mrefu, rehema, wema, uaminifu, upole, kujitawala, pamoja na sifa zote za Yesu mwenyewe: shukrani, ukweli, usafi na uradhi wote.

Mungu hutazamia matunda ya Mwana wake ndani ya maisha yako, kwa sababu Kristo alikufa, akafufuka, naye alimwaga Roho yake ndani ya watu, ili wengi waweze kuleta ukamilifu wa matunda yake maishani mwao. Jinsi mtunza wa shamba la mizabibu afanyavyo kazi kwa bidii, ili azalishe matunda, ndivyo na Mungu anayo haki kuyapata ndani yako.

Kabla ya kristo, binadamu alikuwa anahesabiwa kuwa mtumwa wa sheria, hadi tamaa zote zikachipuka ndani ya mwili wake, kwa sababu makatazo ya sheria yalituchokoza kutenda mabaya. Sheria ilituongoza kuleta zaidi yale matunda ya mauti. Kwanza sheria inatuvuta kuvuka mipaka yake, ndipo inatuhukumu bila huruma.

Hata hivyo, ndani ya Kristo tulifia madai yote ya sheria, kwa vila Kristo alitimiliza kabisa sheria kwa njia ya kifo chake. Na kwa sababu tumefia utu wetu wa zamani kwa njia ya imani yetu ndani ya Msulibiwa, tunajihesabu kuwa utu wetu wa kale umekufa na kufunguliwa na maandishi ya zamani ya ufunuo wa sheria.

Wakati uo huo Mwana wa Mungu ametuita ndani ya agano lingine jipya, ambalo limewekewa msingi wa mafunuo bora, ili tusijikwae kwenye herufi ya sheria , bali tumtumikie Mungu katika nguvu ya Roho yake. Maisha yetu haikuzungushwa tena na makatazo yanayotisha, lakini tumefufuliwa kwa njia ya karibisho la upendo kwa ajili ya maisha ya furaha ndani ya nguvu ya amani tukufu. Roho wa agano hilo jipya haliwezi kuzeeka, wala kufifia, maana ndiye Mungu mwenyewe na ukamilifu wake usio na mwisho. Yeye anayo uwezo bila mipaka upande wa hekima, wema, uaminifu na tumaini. - Wewe, kwa sababu hiyo basi, ujikabidhi kikamilifu kwenye mwongozo wa Roho wa Mungu ndani ya Injili, ili upate kupokea utajiri wa kiroho na nguvu tukufu, tena upate kukua ndani ya unyenyekevu na upole wa Kristo, kwa vile utu wako wa kale umekufa na Yeye anaishi ndani yako.

SALA: Ee Mungu Mtakatifu, asante sana kwa sababu ulituita kutoka kwa utumwa wa sheria, kwa njia ya kifo chake Kristo, aliyetimiza upendo na ukweli maishani mwake na katika msalaba wake. Tunakutukuza kwa sababu unatuvuta ndani ya agano jipya ulilofanya nasi, nawe unatutawala na Roho yako ya kutufariji ndani ya mioyo yetu, ili tuletena matunda yake kwa njia ya nguvu ya neema yako.

SWALI:

  1. Kwa nini waumini wote wameondolewa na madai ya agano la zamani?

Bali twaamini kwamba
tutaokoka,
kwa neema ya Bwana Yesu
vile vile kama wao.

(Matendo ya Mitume 15:11)

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 15, 2022, at 12:47 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)