Previous Lesson -- Next Lesson
3. Neema ya Kristo ulishinda kifo, dhambi, pia na sheria (au Torati) (Warumi 5:12-21)
WARUMI 5:12-14
12 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hiyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi; 13 maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria; 14 walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja.”
Paulo anatuwekea wazi na sisi ile siri ya kifo, akituonyesha kwamba, dhambi zetu ndiyo sababu kwa ajili ya uharibifu wetu. Wazazi wetu wa kwanza walianza uasi wao dhidi ya Mungu, nao wakavuna adhabu, ambayo ni kifo, na hivyo wakavuta viumbe vyote ndani ya ubovu wao, maana wote tu wa mbegu ile ile. Tangu wakati ule mauti inatawala juu ya viumbe vyote, hata juu ya wana-sheria na wacha Mungu wa Agano la Kale, maana dhambi imetokea waziwazi, na adhabu ya kifo imekuwa kama sheria tangu hapo sheria ilipotolewa.
Sisi sote tutakufa, kwa sababu tu wenye dhambi. Ulimwengu wetu wa kibinadamu hauna uzima wa milele. Sote tunaelekea hatua kwa hatua kuelekea kifoni, kwa sababu tunabeba mbegu za kifo ndani yetu. Hata hivyo, Mungu atujalia muda wa kuungama, ili labda tumkubali Mwokozi, tupate kukaribishwa kwenye maisha mapya kwa njia ya imani yetu ya Kikristo.
WARUMI 5:15-17
"15 Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi. 16 Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyefanya dhambi si kadiri ya kile kipawa; kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu; bali karama ya neema ilikuja kwa ajili ya makosa mengi, ikaleta kuhesabiwa haki. 17 Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema , na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.“
Paulo anatuelezea na sisi ile siri ya dhambi na kifo kwa nja ya yule wa kwanza, Adamu, na habari ya haki na uzima kwa njia ya Adamu wa pili, ambaye amwita Baba yetu wa kwanza: „ni mfano wa Kristo, aliyekuwa wa kuja“.
Paulo hakusema kwamba, jinsi dhambi na mauti zilivyoenea kwa watu wengi kwa njia ya Adamu, hivyo neema ya Mungu na zawadi ya uzima wa milele zilienea kwa wengi kwa njia ya mtu huyu Yesu, hapana; Maana Kristo ni mkubwa kuliko Adamu, na pia tofauti sana. Bwana wetu hutujalia si kidogo tu, bali uneemefu wa neema na vipawa vya mbinguni. Neema yake hujaa tele ndani ya wengi. Haileti hali ya kifo na ya kupooza kama mauti, bali inatoa maisha yaliyofufuka, yenye matunda, ya kukua na yenye nguvu.
Maamuzi ya Mungu dhidi ya dhambi ilianza na mtu wa kwanza, na kupitisha kwa kujiendea tu hukumu kwa watu wote. Si hivyo kwa kuwekwa haki, ambayo haikuanza na mtenda dhambi mmoja, bali kwa watenda dhambi wote, maana Yesu aliwahesabia haki wote mara moja. Yule amwaminiye yeye huhesabiwa haki. Wakati mauti ilipopata kuwa mfalme wa kufisha juu ya binadamu kutokana na dhambi ya wazazi wetu wa kwanza, Yesu kwa ajili ya neema yake kuu, alifungua chemchemi ya faraja na mema, na kutokana na hayo uzima wa milele unatiririka kwa waumini wote. Hata hivyo, uzima kutoka kwa Mungu haikutawala kwa lazima juu ya mioyo ya waumini, jinsi mauti ilivyofanya (kwa lazima), ila wale waliotakata watatawala milele na Kristo, Mwokozi na Bwana wao. Kwa kweli, ukuu wa Kristo hauwezi kufananishwa kwa vyovyote na Adamu, maana neema na uzima wa Mungu ni tofauti sana na mauti na lawama.
WARUMI 5:18-21
"18 Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima. 19 Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki. 20 Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi; 21 ili kwamba, kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema na itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.“
Paulo anarudi kwenye linganisho lake la kufaa kati ya Adamu na Kristo. Hata hivyo, katika fungo hilo la andiko halinganishi watu kwanza, lakini kazi zao na matokeo yake. Kutokana na kutokutii mara moja hali ya kuhukumiwa ilitawala juu ya watu wote, walakini kutokana na tendo moja la haki kule kuhesabiwa haki na kweli ya uzima wa milele zilitolewa kwa wanadamu wote. Loo, jinsi toleo la mbinguni lilivyo kuu! Ndiyo, kwa kutokutii kwake yule mtu wa kwanza, sisi sote tulifanywa kuwa wafungwa wa dhambi; lakini kutokana na utii wa kwanza, sisi tuliwekwa huru na kufanywa kuwa wenye haki.
Mwishowe katika linganisho hilo kati ya Adamu na dhambi yake, na Kristo ndani ya haki yake kamili, Paulo anaingiza na tatizo la sheria. Maana sheria haikuhesabiwa kuwa na msaada kwa ajili ya ukombozi wa ulimwngu, kwa sababu iliingia katka historia ya wokovu ili kuonyesha habari ya kuvunja sheria kwa ushahidi na kumchochea mtu akamilishe utii wake. Hata sheria iliongeza ugumu wa mioyo ya watu na wingi mno wa dhambi zake. - Sasa basi, Kristo alitupeleka karibu sana kwenye asili ya neema yote, naye anatutolea ukamilifu wa nguvu na kuhesabiwa haki siku zote na kuendelea, ili mito ya neema zimwagike kwenye majangwa yote ya dunia. Paulo anafurahi sana na kulia kwa sauti ya shangwe, „Kama dhambi kwa njia ya mauti, ilitawala juu ya wanadamu wote katika enzi za hapo nyuma, utawala ule mbaya sasa umekwisha, maana neema imepewa taji kama malkia juu ya wakati wetu, hali imewekewa msingi kwenye haki ya Mungu iliyothibitishwa na msalaba wa Yesu.
Sasa kila mtu anayo sababu ya kuwa na shukrani, faraja na sifa, maana kifo na ufufuo wa Kristo zilifungua wakati mpya ki-historia kwa ajili yetu, ambamo ndani yake nguvu ya dhambi na mauti zimeshindwa. Sisi tunaona maendeleo ya neema kutokana na matunda yake pamoja na uzima wa milele, pia na ukamilifu wa enzi ya Mungu unatenda kazi katika injili ndani ya wote wanaoamini ndani yake Kristo.
SALA: Tunakuabudu Bwana Yesu, kwa sababu wewe ni Mshindi juu ya dhambi, mauti na Shetani. Wewe umetubeba kwenye wakati wa neema, na ulitufanya kuwa washiriki katika mambo yote mema ya maisha yako. Uimarishe imani yetu, na utie nuru ndani ya ufahamu wetu, ,ili tusigeukie tena kwenye nguvu zile za zamani zilizoshindwa sasa. Utuimarishe ndani ya neema yako, na utokeze ndani yetu matunda ya Roho yako, ili iwe thibitisho kwamba, neema yako kweli inatawala, na ya kwamba, inayo nguvu kuliko mauti. Tunakushukuru kwa sababu umetubariki na ukamilifu wako, na pia unatutunza kwa uaminifu wako kamili.
SWALI:
- Paulo anataka kutuonyesha nini kwa njia ya linganisho lake la Adamu na Yesu?