Previous Lesson -- Next Lesson
1. Ghadhabu ya Mungu dhidi ya mataifa imewekwa wazi (Warumi 1:18-32)
WARUMI 1:24-25
"24 Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. 25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina:“
Mstari wa 24 unatuonyesha daraja la kwanza la ufunuo wa ghadhabu ya Mungu. Hakimu mtakatifu anajitenga na wale wote wanaomfahamu, lakini bila kumheshimu, ili waangukie kwenye tamaa za mioyo yao. Wanapata kuwa vipofu kiroho, kwa sababu ya kutokutii kwao. Wao hawamwoni tena Mungu kuwa ni kiini cha walimwengu, lakini wanaanza kuzungukia nafsi zao wenyewe, maana hali ya kujiona wenyewe huanza ndani ya wote wasiompenda Mungu. Kutokana na hayo, mwelekeo wa maisha yao umebadilika, na mwisho wa maisha yao unapata kutawaliwa na roho wa umimi, badala yake Mungu. Wao wanaishi tu kwa ajili ya mafurahisho ya kinyama na tamaa, wakikana kwa kiapo kuwajibika kwao kwa Mungu na kukataa hata kuwepo kwake.
Na kama mapenzi ya mtu imetawaliwa na tamaa zake, ndipo dhambi haitokei tu kimawazoni, bali pia katika utendaji. Maana karibu dhambi zote zinatendeka nje ya mwili baada ya kuchafuliwa. Damiri yako inachukizwa dhidi aina zote za uchafu, maana kwa kutenda dhambi, unapotosha mfano wa Mungu ndani yako. Mwili wako uliumbwa uwe hekalu la Roho Mtakatifu, na dhambi zozote dhidi ya mwili wako ni kuiondolea heshima hiyo hekalu la Roho Mtakatifu, na hii inatendeka kwa njia ya kuileta mwili wako, ulioumbwa kwa sura ya Mungu, katika hali ya kutokuheshimiwa na kupata aibu.
Kuna hatua za kuingia katika hali ya uchafu. Mtu anapogeuka mbali na Mungu, anapoteza hali ya kawaida na kupata hali ya kioja, na anaanza kufikiria mambo kinyume cha sheria kuwa sawa na sheria, maana kupinda kweli za Mungu ndiyo kiingilio katika hali ya kutenda dhambi bila kukataliwa na dhamiri. Mtu aliyepotoshwa hivyo ni mwenye wasiwasi anayewaharibu na wengine na kufungwa katika tamaa zake mwenyewe. Ziwa la majaribu lilivyo kina gani, ya kuharibu mwili na roho, pia na ya laana kutokana na maisha bila Roho wa Mungu ! Dhambi inajionyesha tamu na na ya kufurahisha mwanzoni, lakini tunapoitenda, tunajisikia kuchukia, na tunatambua aibu kwa ajili yetu wenyewe. Kwa njia iyo hiyo wengi wetu wanageuka rangi ya uso kwa ajili ya fadhaa na haya, - machukizo yao yatakapofunuliwa kwenye siku ya mwisho ya hukumu.
Kiini cha dhambi sio kupotoka tu, bali ni ibada isiyo sawa. Kugeuka mbali na Mungu inaharibu msimamo wa nafsi ya mtu, maana mara anapoenda mbali na Bwana wake, anaishi bila kuwa na mwelekeo. Yeyote asiyetaka kumtambua Mungu ameshurutishwa kufanya sanamu kwa ajili yake, maana mtu hawezi kuishi bila mwelekeo. Kwa hiyo basi sanamu zote za watu sio za kweli, zinaharibika, na zimetengenezwa na mikono ya watu. Heri watu wangeweza kutofautisha kati ya maisha na hali ya milele! Maana ndipo wasingekuwa watumwa wa pesa, roho mbaya, vitabu, au hata watumwa wa watu.
Yupo Mmoja, anayestahili kupewa shukrani zetu na heshima. Yeye ndiye Mwenye Uwezo wote, na bila yeye hakuna kinachotendeka, mwenye kujua yote na hekima yote; naye ni mwenye rehema kwa viumbe vyake vyote. Sifa zake ziwe midomoni mwetu daima, maana ameinuliwa juu mno, naye hawezi kukosea jambo, na hakuna kabisa yasiyo ya haki na halali ndani yake. Upendo wake ni mpya kila asubuhi. Uaminifu wake ni juu mno. Yeye hafi milele wala hawezi kubadilika, naye anatutunza kwa uvumilivu usioshindika. Watu wangemgeukia tu Muumbaji wao, ili wapate kuwa na msingi kwa maisha yao, kipimo kwa ajili ya vitu wanavyovithamini, pia kuwa na shabaha kwa ajili ya tumaini lao!
Paulo alikamilisha tamko lake kwamba, Muumbaji hubarikiwa daima na neno hilo „Amina“, kana kwamba somo lake ni sala au ushuhuda. Neno hilo „Amina“ inamaanisha „Iwe hivyo“. Kweli, la kuaminiwa na kuhakikishiwa kabisa ni kwamba, Mungu hawezi kulinganishwa na lolote. Heri yetu Bwana akiruhusu uungu wake kuwa kusudi letu kuu mawazoni mwetu, mipango na shughuli zetu, ili maisha yetu na mawazo yetu yawe yenye afya na ya kukubalika vema. Ulimwengu bila Mungu ni kama jehanum ambayo haijaiva, maana wale waliokwisha kupotea katika tamaa za mioyo yao wanajiharibu wenyewe kwa njia za uchafu wao ya aibu.
SALA: Tunakuabudu wewe, Ee Mungu mtakatifu, maana wewe ndiwe wa milele, safi na mwenye haki. Ulituumba katika hali safi kabisa, nawe unatutunza katika rehema zako. Tunakupenda tukikuomba uvute mioyo yetu kwako, ili tuishi tu kwa ajili yako, tukuheshimu na kukushukuru wakati wowote. Utusamehe tulipogeuka kwenda mbali nawe, na utusafishe na machafu yetu. Utuweke huru na sanamu zetu, ili tusipende chochote humu duniani ila Wewe tu.
SWALI:
- Yapi ni matokeo ya kutokumwabudu Mungu ilivyo sawa?