Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 011 (The Wrath of God against the Nations)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
A - Ulimwengu Wote Umekaa Chini Ya Utawala Wa Yule Mwovu, Na Mungu Atahukumu Wote Kwa Uadilifu (Haki) (Warumi 1:18 - 3:20)

1. Ghadhabu ya Mungu dhidi ya mataifa imewekwa wazi (Warumi 1:18-32)


WARUMI 1:22-23
"22 Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika ; 23 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo.“

Hakuna mtu mwenye hali ya kufa awezaye kuishi bila Mungu. Kama alimkataa Bwana wake moyoni mwake, basi atawageukia miungu mingine, maana mtu alivyo ameumbwa kwa ajili ya kuamini. Wote wanaokataa habari ya kuwepo kwake Mungu (atheist), kama ni mwenye kusoma au kutokusoma, wanao sanamu zao wenyewe, wanazozitegemea, wanazipenda na kutukuza, wanajitoa kwao na hata kujitoa kama dhabihu kwa ajili yake. Umati wa watu huwafanya viongozi kuwa miungu yao, wakitegemea kujaliwa mafanikio kwa sababu yao.

Kila mtu naye hukusanya pesa na kutafuta utajiri, ili aimarishe raha na starehe yake. Waliosoma sana wamejitumbukiza ndani ya vitabu vyao na filosofia zao tupu, wakidhani kwamba wanajua mengi, wakati na wao hawana kitu ila kuwa na wenye dhambi. Wana-siasa wanategemea sana kufaulu kwao kwa namna yoyote ile, hata gharama yake iwe ya juu mno. Wasomi wa chuo kikuu (students) wanategemea sana maendeleo katika mazingira yao, na wenye mashuhuli wanajitoa wenyewe kwenye roho ya mapinduzi. – Hofu hutawala juu ya hao wote, kwa sababu amani ya Mungu haimo ndani ya mioyo yao.

Madreva fulani wa mataxi waliweka ushanga wa blue kwenye kioo cha magari yao, ili iwalinde na macho maovu, ila hivyo wanakataa uwezo wa Mungu kuwalinda barabarani. Baadhi ya wasafiri huvaa hirizi, ambazo pia zinafikiriwa kuwapa ulinzi. Watu wengi huwakimbilia wauguzi na wenye kutabiri mambo ya mbeleni. Mara nyingine husimama kwenye msululu mrefu kungojea zamu yao kufanyiwa uhusiano na wafu, au pia kwa roho fulani. Watu hutenda dhambi kila siku zaidi ya mara milioni moja dhidi ya amri ya kwanza: „Mimi ndimi Bwana, Mun gu wako. Usiwe na miungu mingine mbele zangu“.

Ulimwengu umekuwa kipofu kwa ajili ya ukewli wa utukufu wa Mungu, na watu huenda kupotea baada ya madanganyo, wakitamani tumaini na amani kwa ajili ya mioyo yao mitupu. Wengu wao wanatawaliwa na hali ya kukata tamaa na ya kuona mambo yote kuwa mabaya.

Watu huvutwa sana kufuatia taarifa za habari kuhusu wata wanaosafiri angani, wabingwa wa mambo ya TV, pia na ya viongozi wakubwa wa siasa, lakini hawachukui muda kufahamu maagizo ya Mungu wala kuyafuata maishani mwao. Baya zaidi wanaangamizana wao kwa wao vitani, na wanajiharibu wenyewe kwa kumkataa Mwumbaji wao.

Ujipime mwenyewe! Unajipenda mwenyewe, au mtu fulani mwingine zaidi kuliko kumpenda Mwumbaji wako? Unategemea sana injini ya gari yako? Unajipendekeza mwenyewe sura yako nzuri? Unatafuta uombezi kutoka kwa watu? Yote ya kidunia unayoyapenda yanamfanya Mungu kwako kuwa mdogo. Basi, mpende Bwana wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, kusudi sanamu na miungu yako na hata kujipenda kwako yapate kufa, na utukufu na msaada wa Mungu yakuangazie.

SALA: Ee Baba, tunakushukuru kwa sababu ulituumba kwa mfano wako, na pia kutufunulia kiini chako ndani ya Mwana wako. Tunaomba ufunulie upendo wako kwa watu wote, ili hali ya kutokuamini ipotee kote ulimwenguni, na jina lako la Kibaba lipate kutakaswa. Utusamehe pale tulopokuwa na miungu mingine au sanamu., na uyafute kabisa toka mawazoni mwetu, ili Mwana wako apate kutawala peke yake ndani yetu daima.

SWALI:

  1. Kwa nini inampasa mtu aishiye bila Mungu ajitengenezee mungu wa kidunia kwa ajili yake mwenyewe?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 15, 2022, at 01:09 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)