Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 119 (Jesus appears to the disciples)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 4 - Nuru Inashinda Giza (Yohana 18:1 - 21:25)
B - UFUFUO na KUTOKEA KWAKE KRISTO (YOHANA 20:1–21:25)

2. Yesu awatokea wanafunzi wake kwenye chumba cha orofani (Yohana 20:19-23)


Yohana 20:19
“Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu.”

Ndani ya chumba kilichofungwa milango wanafunzi waliketi pamoja, wakijadiliana matukio ya kuogofya yaliyotokea siku hiyo ya Jumapili. Walifahamu kutoka kwa Petro na Yohana kwamba kaburi ilikuwa tupu. Wale wanawake walithibitisha hayo pamoja na maneno waliyoyasema malaika, kwamba amefufuka. Zaidi ya hapo Mariamu Magdalene alitangaza kwamba amemwona. Habari hii iliwajia wafuasi wa Yesu kama mshtuo, kwamba aliyekufa yu hai, lakini hakufika kwao, kundi lililokuwa waaminifu. Lakini wao walikuwa wakisinzia Bwana alipofungwa; Petro alikuwa amemkana, na hakuna kati yao aliyesimama karibu na Bwana wakati wa kushtakiwa kwake; wala hakuna hata mmoja aliyekuwapo hapo penye msalaba, isipokuwa Yohana na wanawake; pia si wao waliomwondoa msalabani ili kumpaka mafuta. Walikuwa wakihofia Wayahudi, wakifikiri kwamba udhalimu utaanza mara baada ya sikukuu kumalizika. Kwa sababu hizo walifunga milango na kukutana bila tumaini katika chumba cha ndani.

Walisikia kana kwamba taarifa za wanawake zilikuwa ndoto za upuzi wakisemezana, “Sisi tulimfuata Yesu, na tulimtazamia kushinda kwa shangwe na kutufanya kuwa mawaziri wake. Hapo basi tu wenye kushindwa kabisa; watatufukuza katika upotevu.”

Wakati wa hali hii ya kukata tamaa, na ijapokuwa walipungua imani na kusikia uchungu, Yesu akasimama katikati yao. Hakuja kwa sababu ya tumaini lao, upendo na ufilisdi wao, awahurumie juu ya upotovu wao na kuony esha neema juu ya kutokuamini kwao, hapana.

Kutokea kwake Yesu kimyakimya kati yao ilikuwa ni mwujiza. Mfu atokee yu hai, aliyekataliwa yuko huru! Si kaburi ya mwambani wala mlango wa chuma zingeweza kuzuia kuwepo kwake kati ya wateule wake. Basi, alikuwapo hapo katikati yao chumbani akiwa na mwili kama wanadamu wengine, akionekana, kusikiwa na kuweza kuguswa. Ila wakati uu huu alikuwa roho, akiweza kupita katikati ya kuta na milango iliyofungwa. Hali yake mpya inatuonyesha na sisi jinsi tutakavyokuwa, ikiwa tunadumu ndani yake. Mwili wake wa ufufuo ndiyo tumaini letu pia.

Loo, ni faraja ya namna gani! Huyu aliyefufuka kutoka kwa wafu hakuwakemea wanafunzi wake kwa ajili ya mapungufu yao mengi, lakini aliwasalimia na salamu ya Ufufuo, akitamka maneno ya kwanza mbele ya kundi lote baada ya kufufuka, „Amani iwe kwenu!“ Salamu hiyo ndiyo ishara kwamba kwa njia ya msalaba wake aliupatanisha ulimwengu na Mungu. Amani ilianza kuenea toka mbinguni kuja duniani, na milenium mpya ikaanza, iliyotolewa na Kristo kwa ajili yetu, ili tumkubali au kumkataa. - Kila mtu peke yake awajibika kwa ajili ya wokovu wake. Kila mmoja anayeungama na kuamini ndani ya Yesu anashiriki katika baraka zake. Yeyote anayejiunga na daraja la Mfalme wa Amani, huhesabiwa haki kwa ajili ya dhabihu yake ya pekee, jinsi Paulo anavyoeleza akisema, “Basi tukiisha kuhesabiwa haki kwa imani, tunayo amani na Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo“ (Warumi 5:1).

Sala: Bwana Yesu Kristo, uliyefufuka kutoka kwa wafu, wewe Mfalme wa Amani, tunainama mbele zako kwa furaha na shukrani, maana hukuja kwetu kwa hukumu na kuadhibu, bali umekuja kumwaga neema yako na kutuokoa kutoka katika hali ya kukata tamaa na ya kutokuamini, ili kutujalia amani yako na kutuunganisha katika upatanisho na Mungu. Wokovu wako sio mshahara kwa ajili ya bidii zetu, bali ni zawadi ya neema. Wafundishe marafiki na maadui zetu, waweze kutambua makusudi yako ya rehema; ili wapate kukupokea, wala wasije wakafuliza katika uadui juu ya Mungu Mtakatifu.

Swali 123: Ipi ni maana ya maneno ya kwanza ambayoYesu aliyatamka mbele za wanafunzi wake baada ya kufufuka kwake?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on June 29, 2017, at 05:52 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)