Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 088 (The Holy Trinity descends on believers)
This page in: -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 3 - Nuru yang’aa ndani ya shirika la Mitume (Yohana 11:55 - 17:26)
C - Hotuba ya kuaga kwenye chumba cha orofani (Yohana 14:1-31)

2. Utatu utakatifu huwashukia waumini kwa njia ya Mfariji (Yohana 14:12-25)


YOHANA 14:21
“Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.”

Mto wa baraka na neema unafurika kutoka kwake Yesu Kristo ndani ya Kanisa lake wakati wowote. Hata kama waumini wote wangejazwa na mafuriko hayo, bado bahari kuu ya neema ingebakia. Mbele ya adui zake ilimpasa Yesu kuhakikisha tamko lake kwamba yeye ndiye Masihi na Mwana wa Mungu. Lakini kwa wanafunzi wake alifunua utajiri wa umoja wake na Baba katika saa hizo za mwisho tu. Basi mioyo yetu ifunguliwe kwa upana, ili ukamilifu wa uungu wa Kristo uweze kutujaa.

Yesu alitueleza kwamba, upendo wa wanafunzi wake kwake haukuwa ni msukumo tu kutokana na hisani yao, lakini upendo huo ulikuwa umejengwa juu ya utii kwa maagizo yake na maisha ya utendaji wa utii huo. Mtu wa kawaida hatambui agizo hilo kutokana na upendo wa Kristo. Bwana hutufungulia hazina za mbinguni, ndipo anatutuma nje tuwahudumie watu waliopotea, na pia kuwajenga kiroho ndugu zetu; anatujalia uwezo wa kutambua mipango yake aliyo nayo kwa ajili yetu. Maagizo yake siyo ya kutukandamiza au kutushinda, kwa vile furaha ya Roho inatusukuma, na Roho wa kweli inatugusa kuungama kila tendo baya au iliyo na hatia tuliyoifanya. Huyu Roho anatutia nguvu, ili tuzishike amri zake, kwa sababu alitupenda na kutuokoa kwa kila hali, na hivyo tunampenda mno na kutembea naye ndani ya Roho yake.

Je, unampenda Yesu? Usijibu haraka ukisema “Ndiyo” kwa kuchekelea. Wala usiitike “Hapana” kwa uzito. Kama umezaliwa kwa upya, Roho Mtakatifu ndani yako atasema, “Ndiyo nakupenda, Bwana Yesu, kwa sababu ya ukuu na unyenyekevu yako, pia kwa sababu ya dhabihu uliyotoa na uvumilivu uliyo nayo; umeumba ndani yangu uwezo wa kupenda, asante sana.”

Maongezi kama hayo na Roho Mtakatifu ndani yetu sio tumaini la juu juu au wazo tu, lakini yamewekwa juu ya uamuzi wa utendaji katika upendo. Bwana huumba upendo ndani ya wapendwa wake na kuwaweka imara ndani yake mwenyewe kwa neema.

Mungu huwapenda wampendao Yesu. Baba alikabidhi uwezo wote na rehema ndani ya Mwana wake kwa ajili ya kuokoa binadamu. Yeye ampokeaye Yesu, ampokea Mungu; na yeyote amkataaye Mwana, basi amemkataa Mungu. - Je, unatambua kwamba, Mungu akuita, “Mpendwa wangu”, kwa sababu Roho wa Kristo amekubadilisha na kukufanya uwe mtu wa kuweza kupendwa? Wewe huwezi kuwa mwema kwa kutaka mwenyewe, lakini upendo wa Mungu unakufanya uwe kiumbe kipya. Kristo atenda kazi ndani yako akikuombea kwa Baba, naye atakutunza hata milele. Yeye atajifunua kwako kwa uhakika wa kiroho. Kiasi chochote utakachokua katika ufahamu wa Mwokozi wako, ufahamu peke yake bado utadumu kuwa dhaifu, maana ufahamu wa kweli unamaanisha kukua katika hayo: utii, upendo, kujitoa na kujikinahi.

YOHANA 14:22-25
“Yuda (siye Iskariote), akamwambia Bwana, imekuwaje ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu? Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda , atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake na kufanya makao kwake. Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka. Hayo ndiyo niliyowaambia wakati nilipokuwa nikikaa kwenu.”

Yesu alikuwa na mwanafunzi mwingine aliyeitwa pia Yuda, sio Iskariote. Yeye alitambua kwamba Yesu alisogea kwa mambo mengine katika maongezi yake baada ya msaliti wake kuondoka. Alihisi kwamba tukio fulani la ajabu litakokea.

Yesu hakumjibu moja kwa moja, lakini akatangaza shabaha kuu ya Kanisa pamoja na haja ya kufia mambo ya dunia. Yesu aliwaonyesha hatua za kuwaongoza kwa ufahamu wa kweli wa Mungu. Hilo ndilo jambo hasa kwamba, kumfahamu Yesu na kumkubali, ndilo linalotokeza uwazi kwake na maisha mapya; na pamoja na nguvu za Roho Mtakatifu kushika amri zake; hayo ndiyo njia ya kutambua upendo wa Mungu. Ndipo, Yesu alitamka maneno ya kugusa sana, “Sisi tunakuja kwa mwumini wa namna hii, na kwake tutafanya makao yetu.” Hapo hasemi juu ya Kanisa kwa jumla, bali kwa mwumini mmoja mmoja. Utatu utakatifu hutembelea mwumini, ndipo kukaa ndani yake! Tamko hilo lagusa sana moyo wa mtu, kana kwamba anakumbatiwa na Roho Mtakatifu, Mwana na Baba pamoja. Kwa kuingia katika hatua za kuokolewa, mtu hutambua kwamba, Mungu anamzunguka kabisa, akimlinda binafsi na mabaya yote. Kila mmoja amtegemeaye Kristo namna hii, atatambua ukweli wa siri hiyo.

SALA: Ee Utatu utakatifu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, nakuabudu, nakushukuru na kukutukuza. Umenitembelea na kukaa ndani yangu mimi mwenye dhambi. Nisamehe dhambi zangu. Asante sana kwa nguvu za upendo ulizonijalia, na kwa Roho ya upendo ndani ya moyo wangu. Unitunze ndani ya jina lako.

SWALI:

  1. Jinsi gani upendo wetu kwa Kristo unaweza kukua; na jinsi gani Utatu Utakatifu unweza kutushukia?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 12, 2015, at 04:46 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)