Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 089 (Christ's farewell peace)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 3 - Nuru yang’aa ndani ya shirika la Mitume (Yohana 11:55 - 17:26)
C - Hotuba ya kuaga kwenye chumba cha orofani (Yohana 14:1-31)

3. Amani ya Kristo ya kuaga (Yohana 14:26-31)


YOHANA 14:26
“Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.”

Nani anathubutu kudai kwamba anafahamu maana ya maneno yote ya Kristo? Au nani aweza kuyakariri matamshi yake yote na kuyatimiza? Wanafunzi waliohangaika wakati wa Meza ya Bwana walitafakari juu ya madhara ya msaliti na ni nini atakaloweza kutenda sasa. Walishindwa kukumbuka mengi katika yale ambayo Yesu alisema kwenye hotuba yake ya kuwaaga, isipokuwa Yohana tu.

Yesu alikuwa ametulizwa na usahaulifu wa wanafunzi, akielewa kwamba, Roho wa kweli atawajalia kuwamulikia na kuwafanya kuwa wapya, jinsi alivyowafundisha. Huyu Roho aendeleza kazi ya Yesu kwa maana na shabaha yake ile ile. Tena anawalinda wadhaifu. Yesu hakuchagua waelekevu, au wasomi wa filosofia na wenye kipawa cha kusema; bali alichagua wavuvi, watoza ushuru na baadhi ya wahalifu, ili atie aibu kwa ufahamu wa kidunia na wenye kuendelea sana katika masomo. Baba kwa rehema zake alimtuma Roho yake kwa wasioelewa, awafanye kuwa watoto wake, akiwajalia kipawa cha kuelewa unyenyekevu ni nini, wakijikinahi wenyewe na kuishi katika unyofu wa moyo.

Yesu hakubainisha kitabu katika namna ya shairi, wala hakuandikisha injili yake kwa fulani, ambaye labda atapoteza karatasi kadhaa au kusahau kiini chake. Kwa mategemeo makuu alifahamu kwamba Roho atawafunulia ukweli wa kuwa fundisha wanafunzi wake, kuwamulika, kuongoza na kuwakumbusha yote aliyowaambia. Injili ndiyo kazi mojawapo kuu ya Roho hadi leo hii. Alikabidhi mpango wa wokovu kwa lugha ya kibinadamu na ndani ya kumbukumbu ya wanafunzi; Roho aliwakumbusha na kuwafundisha kwa kuwaimarisha ndani ya matamshi ya Yesu, ili huyu Roho apate kumtukuza Mwana kwa njia ya ushuhuda wa Mitume. Hatuna kitabu kingine cha kutushuhudia maandiko ya mitume ya Kristo, ambao kwa unyenyekevu wanauwekea wazi ulimwengu ufahamu na imani walioipokea. Hakuna maneno ya kuongezea yaliyowekwa mdomoni mwa Yesu. Mahubiri yao hayakuwa baridi au taarifa kavu tu, yaliyopata hali ya kutokufaa kwa muda, lakini Roho alihuisha uhai wa maelezo hayo na kutilia nguvu hasa, siku zote hadi leo. Tunaposoma Injili, inaonekana kana kwamba tunasoma habari ya mambo yaliyotukia katika siku zetu. Tunaposikiliza maneno ya Kristo, ni kana kwamba yeye mwenyewe anagusa masikio yetu kwa sauti yake. Mtu anayedai kwamba wanafunzi waliingilia au kuharibu maana ya injili ya kwanza, basi hamtambui Roho wa kweli, kwa vile ndani ya Roho Mtakatifu hakuna udanganyifu; yeye mwenyewe ni kweli na upendo.

YOHANA 14:27
„Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapayo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.“

Yesu aliwatolea wanafunzi wake amani; alipomaliza hotuba yake ya kuwaaga, kwamba anawapa amani inayopita salamu zozote za kibinadamu. Alikuwa akiondoka, lakini aliwarithisha amani yake, akitulia juu ya mikutano yao. Alisema kuhusu amani ya uwongo kama vile magazeti yanavyofanya. Majaribio yalikuwa yanakuja kwa uhakika. Kwa vile watu wanaishi mbali na Mungu, ghadhabu yake itaangukia makosa yote ya watu. Yesu anasema habari ya amani tofauti: Amani ndani ya dhamiri zao inayopatikana na masamaha ya dhambi, ambayo inatokana na upatanisho na Mungu; nayo inakuwa dhahiri katika amani ndani ya Kanisa. Amani ya Kristo ndiyo Roho Mtakatifu mwenyewe, ambaye ni nguvu isiyokoma, ikitujia kutoka kwa Mungu na kurudi kwake pia.

Kusema uongo, chuki na ujeuri, kuua, wivu, uchoyo na machafu zimeenea sana duniani. Lakini Yesu atuagiza tusiruhusu mawimbi hayo ya kishetani kutuzamisha. Huyu Mwovu ndiye mtawala wa dunia hii. Lakini ndani ya Yesu hao wapendwa wake, kote tunazungukwa na amani, inayotukataza tusianguke ndani ya giza na kukata tamaa. Pia inatuweka huru na moyo wa usumbufu na hofu ya kifo. Mwumini katika Kristo anaishi ndani ya Mungu na Mungu ndani yake. - Je, hayo ni kweli na kwako? Yesu alilala usingizi ndani ya mashua wakati wa mawimbi ya dhoruba ziwani. Wote wengine ndani ya chombo walikata tamaa, wakati maji yalipojaza chombo. Ndipo Yesu akainuka na kukemea tufani, kukawa shwari. Akawaambia wanafunzi wake, „Enyi wenye imani haba, mbona mmeshikwa na hofu?“

YOHANA 14: 28-31
„Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi. Na sasa nimewaambia kabla halijatokea, kusudi litakapotokea mpate kuamini. Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu. Lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru, ndivyo nifanyavyo. Ondokeni twendeni zetu.“

Wanafunzi walikuwa wakihangaika wakati Bwana wao aliporudia taarifa kwamba ataondoka kwao. Hatua ya kuachana nao ikakaribia. Tena Yesu alithibitisha kuondka kwake, lakini pia alikaza jambo la kurudi kwake. Akasema, „Furahini, nawaacha, kwa sababu naenda kwa Baba. Furahini kwa sababu ya kwenda kwangu kwenye makao yangu ya awali. Sitawatwisha mazito kama mateso ya msalaba. Nitawaweka huru na hofu ya kaburi. Ujumbe wangu kwenu ni habari ya umoja na Baba. Mkinipenda, mgefurahia kurudi kwangu mbinguni. Namhesabu Baba yangu kuwa mkubwa kuliko mimi. Nampenda sana kwa moyo, pia na upendo wangu kwenu hautakoma kabisa. Nitakuja kwenu ndani ya Roho yake.”

Yesu alichora picha kubwa ya Baba, ili wao watambue enzi yake na kushikamana naye, pamoja na kuwa tayari kuachana na Bwana wao, aliyekuwa sasa karibu na kufa. Yesu aliwataka wakumbuke kwamba hata kifo sio ishara ya kwamba Mungu ni adui yake. Amani kati ya Baba na Mwana iliendelea kudumu, hivyo Baba atamvuta kwake ng’ambo ya hiyo kifo.

Mazungumzo zaidi ya hapo hayakuhitajika; Yesu alifufuka, ili akamilishe amri ya Baba, ambayo ndiyo ukombozi wa ulimwengu msalabani. Na ndipo Roho aje juu ya wanafunzi wake. Ukombozi huo utoshe kwa wanadamu wote kabisa. Alipenda sana kwamba kila mtu angetambua upendo huo wa Mungu usio na mwisho.

Baada ya hapo Yesu na wafuasi wake wakaondoka kwenye chumba cha orofani alipoweka ile Agano Jipya; wakaenda nje kwenye giza la usiku, wakivuka bonde la Kidroni. Walitembea hadi mlima wa Mizeituni na kuelekea kwenye bustani ya Gethsemane, ambapo msaliti alijificha.

SALA: Tunakushukuru Bwana, kwa ajili ya amani yako. Umetusafisha mioyo yetu na kututuliza. Utusamehe mahangaiko yetu, hofu na kukata tamaa kwetu katika ghafula za chuki, mapambano na rushwa. Asante sana kwa Roho yako ya kutuongoza kwa amani. Twaomba atukumbushe saa za majaribu habari ya maneno yako yenye nguvu, ili tusianguke katika mitego ya dhambi na kutokuamini au kwenda kukata tamaa; bali tukuangalie wewe tukiomba kwa tumaini, subira na furaha. Asante kwamba njia yetu inaongozwa kurudi kwa Baba. Tunakuinamia, ewe Mwana Kondoo wa Mungu, kwa sababu unatutayarishia makao ya mbinguni.

SWALI:

  1. Amani ya Mungu ni nini?

NAMBA - 5

Mpendwa msomaji, ututumie majibu sahihi ya maswali 12 katika hizo 14. Ndipo sisi tutakutumia tena masomo mengine yanayofuata.

  1. Kwa nini Yesu alikubali kupakwa mafuta na Mariamu?
  2. Kuingia kwake Yesu Yerusalemu namna hii ilikuwa na maana gani?
  3. Kwa vipi Kifo cha Kristo kinaelezwa kuwa ni kutukuzwa kwa ukweli?
  4. Sisi kupata kuwa wana wa nuru inamaanisha nini?
  5. Lipi ni agizo la Mungu ndani ya Kristo kwa wanadamu wote?
  6. Bwana Yesu kutawadha miguu ya wanafunzi wake ilikuwa na maana gani?
  7. Tunajifunza nini kutokana na mfano wa Kristo?
  8. Nini ni maana za utukufu iliyoonyeshwa na Yesu wakati Yuda alipotoka kwake?
  9. Kwa nini upendo ni dalili la pekee linalowatofautisha Wakristo?
  10. Uhusiano wa Kristo na Mungu Baba ni wa namna gani?
  11. Utaje kanuni ya lazima kwa kujibiwa sala zako?
  12. Zipi ni sifa, ambazo Yesu anazitaja juu ya Roho Mtakatifu?
  13. Jinsi gani upendo wetu kwa Kristo unaweza kukua, na jinsi gani Utatu Utakatifu unaweza kutushukia?
  14. Amani ya Mungu ni nini?

Tafadhali usisahau kuandika jina lako na anwani ya Posta kamili waziwazi kwenye karatasi hii ya QUIZ, sio kwenye bahasha tu. Halafu uitume kwa anwani hii:

Waters of Life
P.O.Box 600 513
70305 STUTTGART
GERMANY

Internet: www.waters-of-life.net
Internet: www.waters-of-life.org
e-mail: info@waters-of-life.net

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 12, 2015, at 04:46 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)