Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 070 (Jesus across the Jordan)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
C - Safari ya mwisho ya Yesu kwenda Yerusalemu (Yohana 7:1 - 11:54) Neno Kuu: Kutenganisha giza na nuru
4. Kumfufua Lazaro na matokeo yake (Yohana 10:40 - 11:54)

a) Yesu akiwa ng’ambo ya Yordani (Yohana 10:40 - 11:16)


YOHANA 10:40-42
“Akaenda zake tena ng’ambo ya Yordani, mpaka mahali pale alipokuwapo Yohana akibatiza hapo kwanza, akakaa huko. Na watu wengi wakamwendea wakasema, Yohana kweli hakufanya ishara yoyote, lakini yote aliyosema Yohana katika habari zake huyu yalikuwa kweli. Nao wengi wakamwamini huko.”

Mgongano kati ya Yesu na Mafarisayo ulianza kuenea; walichochea viongozi wa watu baada ya yeye kumponya kilema penye bwawa la Bethzatha (sura ya 5). Mwisho wa kutembelea kwake mara ya tatu Yerusalemu, mgongano huo ulikuzwa kufikia kileleni. “Nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza” (Yoh. 1:5). Wakati wowote Yesu alihatarishwa hadi kuuawa. Hata hivyo akaendelea kimwili tena na tena kuingia hekaluni, akiwaongoza wanafunzi wake waimarike katika ufahamu na tumaini ndani yake, wakati maadui zake wakasogea penye kina cha chini cha chuki.

Kufuatana na sikukuu ya kumbukumbu ya kuweka wakfu hekalu, Yesu aliondoka Yerusalemu akaenda mkoa wa ng’ambo ya Yordani, ambapo Kuhani Mkuu hakuwa na mamlaka. Mapema Yohana Mbatizaji alikuwa amehubiri hapo, ambapo ni nje ya utawala wa kiyahudi, lakini chini ya mmoja wa wafalme wa Herode. Mbatizaji alikuwa amejulikana sana pale; ushuhuda wake juu ya Yesu ukawa wazi.

Wale watu walitangulia kuamini, kwa sababu Mbatizaji aliendelea kufundisha katika imani yao ya awali. Sasa mwalimu wao alikuwa amekwisha kukatwa kichwa. Yesu alipofika, wakamkimbilia, wakifahamu unyenyekevu wake, enzi yake nguvu. Yesu aliwaonyesha mifano na ishara zake, akihubiri kwa uaminifu habari ya Mungu na wanadamu. Basi wengi walifungua mioyo yao kwa Injili, wakiendelea kushikamana na imani kutokana na kazi ya unabii ya Mbatizaji, ingawa Mbatizaji hakutenda miujiza, ili kuthibitisha huduma yake. Lakini mara Yesu alipowafikia, wakamtumaini kuwa ndiye Bwana na Mwokozi

YOHANA 11:1-3
“Basi mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake. Ndiye Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu kwa nywele zake, ambaye Lazaro, nduguye alikuwa hawezi. Basi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake wakisema, Bwana, yeye umpendaye hawezi.”

Wakati Yesu alipokuwa akihubiri kule katika mkoa wa Yordani, mtu aliyeitwa Lazaro akawa mgonjwa. Alikuwa mwenyeji wa kijiji juu ya mlima wa mizeituni. Mara nyingi Yesu aliwahi kuwa mgeni katika nyumba yake. Mazungumzo ya Kristo na Martha, dada yake wa Lazaro, yanajulikana sana. Mwinjilisti Yohana hakuandika mambo hayo, kwa vile yajulikana kwa maandishi ya injili zingine. Hata hivyo anaeleza habari ya Mariamu aliyemimina chupa cha marhamu kwenye miguu ya Yesu. Mwinjilisti anamtaja huyu mwanamke wa pekee, aliyekuwa na njaa ya maneno ya Bwana. Baada ya yeye kumpaka miguu yake na mafuta yale, aliendelea kuifuta na nywele zake (Yohana 12:1-8). Alionyesha wazi unyenyekevu wake, imani na upendo kwake Mwana wa Mungu.

Habari za ugonjwa wa Lazaro zikampa Yesu huzuni. Basi, imani ya dada zake ilimvuta aende kuungana nao. Hawakumwomba Yesu aje haraka kumponya rafiki yake, lakini wakatuma habari hivi hivi kuhusu hali yake, wakitumaini kwamba, Yesu ataweza kumponya hata kutoka mbali. Walisikia uhakika kwamba shauku yake kwa ajili ya Lazaro itamsukuma atende kitu. - “Lazaro” maana yake “Mungu amesaidia”. Hivyo jina lake likawa usemi kwa ajili ya mwujiza ya mwisho unaotajwa na Yohana.

YOHANA 11:4-10
“Naye Yesu aliposikia alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo. Naye Yesu alimpenda Martha na umbu lake na Lazaro. Basi aliposikia ya kwamba hawezi, alikaa bado siku mbili pale pale alipokuwapo. Kisha, baada ya hayo, akawaambia wanafunzi wake, Twende Uyahudi tena. Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, Juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena? Yesu akajibu, Je, saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sabamu aiona nuru ya ulimwengu huu. Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake.”

Habari ilipomfikia Yesu, akawa anatambua shindano lake na nguvu ya kifo ikamjia. Alikuwa ametabiri kwamba huyu mgonjwa hatakuwa mateka ya kifo, bali ndani yake utukufu wa Mungu utang’aa. Yesu alielewa kwa uongozi wa Roho Mtakatifu la kufanya kabla ya rafiki yake kukata roho; enzi yake itajionyesha kwa kumfufua mtu aliyekufa kule karibu na malango ya Yerusalemu. Na hivyo hata wenyeji wa Yerusalemu wasije wakawa na udhuru wa kutokuamini.

Utukufu wa Mungu na kutukuzwa kwake Kristo ni jambo moja. Utukufu ulikuzwa, kwa sababu kwa tendo lake kifo na ushindi zilikabiliana. Ubinadamu kwa jumla unaumia vibaya ndani yake unapokabili kifo. Watu hutambua, kifo kinapeleka moja kwa moja kwa kuzimika kwa uhai. Yesu alifahamu mapenzi ya Babaye na hakushituka kwa kifo na matukio yake, lakini alielewa sababu ya kifo. Katika enzi yake aliweza kupanda uhai ndani ya dunia gonjwa.

Basi Yesu hakwenda moja kwa moja Bethania; alichelewesha kwa siku mbili. Aliruhusu kifo kummeza rafiki yake. Wanafunzi wake walitishwa kwa kusikia kwamba anataka kurudi Uyahudi; walishuhudia matokeo yale ya kumpiga kwa mawe. Wanafunzi hawakumhurumia Lazaro, wala hawakuhitaji kushuhudia utukufu wa Mungu, bali kuwa na hofu tu kwa ajili ya maisha yao.

Hapo ndipo Yesu alitumia kielelezo kwamba, mtu husafiri salama wakati wa mchana, bali usiku aweza kuanguka kwa vizuizi na genge. Kwa vile saa ya kusulibishwa ulikuwa bado, saa za nuru ya mchana zilikuwa bado ziliendelea. Iliwapasa kwenda Yesusalemu pole pole, wakiwa salama mkononi mwake Mungu.

Yeyote asiyeweza kutegemea majaliwa ya Mungu, atasumbuka gizani, sawa na maadui wa Yesu, maana nuru ya imani haijawafikia bado. Hivyo basi Yesu aliwataka wanafunzi wake kumtegemea yeye kabisa pamoja na uongozi wake. Kama sivyo, mashaka yatawavuta hadi gizani. Hii ndiyo faraja letu hata katika saa ya giza kabisa, kwamba hakuna lolote litakalotupata pasipo mapenzi ya Bwana. Ndani yake ndiyo tumaini letu.

SALA: Bwana Yesu, Asante sana kwamba wewe ndiwe Bwana wa maisha; ndani ya nuru yako twaona njia wazi. Unatuongoza katika njia iliyonyoka, hata wakati adui zetu wanatamani kutuharibu. Utusaidie tusichelewe, bali kuwa tayari hata kwa maumivu hata kufa kwa ajili yako. Twapenda tunzo lako maishani mwetu lipate kutukuzwa kwa imani yetu.

SWALI:

  1. Kwa nini Yesu alisema habari ya utukufu wa Mungu, iwapo Lazaro alikufa?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 18, 2014, at 11:35 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)