Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 069 (The Son of God in the Father and the Father in him)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
C - Safari ya mwisho ya Yesu kwenda Yerusalemu (Yohana 7:1 - 11:54) Neno Kuu: Kutenganisha giza na nuru
3. Yesu, Mchungaji Mwema (Yohana 10:1-39)

e) Mwana wa Mungu ndani ya Baba, naye Baba ndani yake (Yohana 10:31-39)


YOHANA 10:31-36
“Basi Wayahudi wakaokota mawe tena ili wampige. Yesu akawajibu, Kazi njema ninyi nimewaonyesha, zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe? Wayahudi wakajibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu. Yesu akawajibu, Je, haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu? Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neon la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka); Je, Yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?”.

Wayahudi walimchukia Yesu kwa vile alisema: “Mimi na Baba tu Umoja”. Walichukua ushuhuda wake juu yake mwenyewe kuwa ni unajisi, wakawa na shabaha ya kumpiga kwa mawe jinsi sheria ilivyodai, vingine ghadhabu ya Yehova ingeangukia taifa lote. Basi wakakimbia uani na kurudi na mawe ili wamtupie.

Yesu alisimama kwa upole mbele zao na kuuliza, “Ubaya gani nimetenda kwenu? Nimewahudumia, nimeponya wagonjwa wenu, nimetoa pepo wabaya na kufungua macho ya vipofu wenu. Nimetakasa wenye ukoma na kuhubiri Injili kwa maskini. Kwa ipi ya kazi hizo mwataka kuniua? Mnatafuta kumwangamiza mfadhili wenu? Mimi sitafuti heshima au pesa kwa ajili ya huduma zangu, ambazo kwa unyenyekevu nilizitaja kuwa ni kazi za Baba yangu. Mimi nipo hapa kama mtumishi wenu.”

Wayahudi walilia, „Hatukupigi kwa mawe kwa ajili ya kazi zozote ulizozifanya, lakini kwa ajili ya unajisi wako. Umejiinua mwenyewe hadi usawa na Mungu, wakati unaposimama kati yetu kama mtu wa kufa. Tutamwaga damu yako na kuonyesha kwamba nawe u wa kufa. Unawezaje kujaribu kusema wewe u Mungu, umoja na Mwenye Utukufu? Lazima umepatwa na mapepo, unastahili kuangamizwa hapohapo.

Katika tumaini kuu Yesu aliwajibu, „Hamkusoma ndani ya torati yenu kwamba Mungu alizoea kusema binafsi na wateule wake akitamka, „Ninyi ni miungu, ninyi wote ni wana wa Mwenye Ukuu“ (Zaburi 82:6), wakati ninyi wenyewe mnaenda kuharibika na kuanguka katika dhambi moja hadi nyingine. Bila shaka wote ni wenye dhambi, wakizunguka katika upotovu. Hata hivyo Mungu aliwaita „miungu na wana“ kwa ajili ya jina lake tukufu. Hapendezwi kabisa na upotovu wenu, bali nanyi mgepata kuishi milele. Mgerudi kwa Mungu wenu na kuwa takatifu jinsi yeye alivyo.“

„Basi, kwa nini mnataka kunipiga kwa mawe? Mungu mwenyewe awaita „miungu na watoto“. Mimi sikutenda kosa lolote kama ninyi. Mimi ni mtakatifu katika neno na tendo; ninayo haki ya kuishi milele, kama Mwana pekee wa Mungu. Someni yaliyoandikwa katika torati yenu, ndipo mtapata kunifahamu, lakini hamwamini hata Maandiko yenu, na hivyo hamtambui uungu wangu.”

“Mimi sikujituma mwenyewe, bali Baba Mtakatifu ndiye aliyenituma. Mimi ndimi Mwana wake; yeye ni Baba yangu. Utukufu wake unadumu na ndani yangu. Hivyo mimi ni Mungu toka kwa Mungu, nuru toka kwa nuru, kutokana na yeye wala si kuumbwa, wa asili moja na Baba.”

Yesu aliwashinda Wayahudi kwa maneno kutoka kwa Maandiko yao, na hivyo kubomoa hoja zao. Lakini macho yao yaliendelea kuwa ovu kwa chuki, hata hivyo walishusha mikono yao, kwa vile Yesu alithibitisha kutoka kwa Kitabu chao uwezekano wa Uwana tukufu katika Agano la Kale kwa jumla, na kwa yale yaliyomhusu yeye mwenyewe.

YOHANA 10:37-39
“Kama sitendi kazi za Baba yangu, msiniamini; lakini nikizitenda, ijapokuwa hamniamini mimi, ziaminini zile kazi; mpate kujua na kufahamu ya kuwa Baba yu ndani yangu, nami ni ndani ya Baba. Wakatafuta tena kumkamata; lakini akatoka mikononi mwao.”

“Maana yake”, akaeleza Yesu, “Ni lazima kuniamini mimi, kwa vile natenda yale atendayo Mungu, ambazo ni kazi za rehema. Mamlaka haingekuwa mikononi mwangu, ikiwa nisingetenda kufuatana na huruma zake. Tangu upendo wake kuingia mwilini ndani yangu, ninayo madaraka ya kutimiza kazi zake Mungu, maana kweli ni kazi za Baba.”

“Inawezekana ufahamu wenu uilikosa kutambua uungu ndani ya ubinadamu. Hata hivyo, mgepima kazi zangu; nani aweza kufufua wafu kwa neno lake, au kufungua macho ya vipofu, au kutuliza dhoruba ya bahari, au kulisha watu 5000 wenye njaa kwa mikate 5 na samaki 2? Kweli mnatamani Roho Mtakatifu afungue akili zenu na kusikiliza sauti yangu, ili mtambue kwamba Mungu mwenyewe yu ndani yangu? Mkipata kujaliwa Roho Mtakatifu, mtadumu ndani ya ufahamu huu wa msingi, na kuelewa kwamba ukamilifu wa uungu umo ndani yangu kimwili.”

Hapo na mbele ya umati wa watu waliosindika, Yesu alitamka maneno hayo ya nguvu, kwamba yeye ni ndani ya Baba; na jinsi tawi la mzabibu lazima adumu ndani ya shina na kupokea nguvu toka kwa mizizi, ndivyo Kristo naye atokana na Baba na kudumu ndani yake. Hao wawili hawawezi kutengana, wakiwa katika mapatano na umoja kamili. Hivyo twaweza kusema: Mwana amefichwa ndani ya baba, ili amfunue Baba na kumheshimu yeye tu. Kwa hiyo sala inayojulikana sana inaanza hivyo: “Baba yetu, uliye mbinguni, jina lako litukuzwe.”

Yeyote atakayechimba chini katika ushuhuda wa Yesu kuhusu uungu wake - katika sala na kumtukuza - atatambua kwamba ni thibitisho dhahiri kabisa dhidi ya kuelewa kijuujuu tu habari ya Utatu Utakatifu. Sio miungu mitatu mbalimbali, bali umoja kamili ndani ya Utatu Utakatifu; hivyo twashuhudia kwa furaha kwamba Mungu ni mmoja.

Wayahudi walipomsikia Yesu akirudia ushuhuda wake juu ya umoja kamili pamoja na Baba, waliachilia kwa kumpiga mawe. Hata hivyo walitamani kumfunga na kumpeleka mbele ya baraza kuu, na hapo waweze kuchunguza na kufunua maoni yake. Basi Yesu aliponyoka mbali nao. - Kuhusu kondoo zake Yesu alisema, “hakuna awezaye kuwapokonya mkononi mwa Baba yangu.”

SALA: Baba na Mwana Kondoo wa Mungu, tunaona umoja kamili ndani ya upendo wako. Ufahamu wetu unashindwa kutambua uungu ndani ya ubinadamu wako. Lakini Roho wako alitumulikia, ili kutambua ule upendo kuu pamoja na matendo yako ya kuokoa. Ulitufanya tuwe watoto wako. Utusaidie kuadhimisha jina lako ndani ya nia zetu, mawazo na matendo yetu. Ututakase tuwe kama wewe ulivyo mtakatifu.

SWALI:

  1. Jinsi gani Yesu alitangaza uungu wake?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 18, 2014, at 11:34 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)