Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 033 (Healing of the paralytic)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
A - Safari ya pili kwenda Yerusalemu (Yohana 5:1-47) -- Neno Kuu: Kutokea kwa uadui kati ya Yesu na Wayahudi

1. Kumponya aliyepooza kwenye birika la Bethzatha (Yohana 5:1-16)


YOHANA 5:1-9
1 “Baada ya hayo palikuwa na sikukuu ya wayahudi; naye Yesu akawea kwenda Yerusalemu. 2 Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania: Bethzatha, nayo in matao matano. 3 Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, wakingoja maji yachemke. 4 Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata. 5 Na hapo palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane. 6 Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima? 7 Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu kunitia birikani, maji yanapotibuliwa, ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu. 8 Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende. 9 Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda. Nayo ilikuwa Sabato siku hiyo.”

Inahisiwa Yesu alikaa miezi tisa Galilaya. Ndipo akapanda kwenda Yerusalemu wakati wa sikukuu ya hekalu. Alifahamu kwamba, vita ya imani itakuwa dhahiri penye mji mkuu. Ingawa aliwakabili wanasheria na wacha Mungu, alishika sheria kwa uaminifu. Mara tatu kwa mwaka alikwea kwenda hekaluni Yerusalemu, wakati ilipowezekana.

Katikati ya jiji kulikuwa na birika, ambalo maji yake - kufuatana na tafsiri zingine za kiyunani - yalikuwa mara kwa mara yakitibuliwa na malaika. Herode alikuwa amejenga malango kuzungukia birika pamoja na nguzo. Mabaki ya jengo hilo yalichimbuliwa siku hizi tu. Jengo lenyewe liliitwa “Nyumba ya huruma”, maana watu wengi walikuwa wakitembelea pale kwa ajili ya kutafuta kupona, wakingoja maji yapate kutibuliwa. Walifikiri kwamba, mtu wa kwanza atakayejitupa majini baada ya kutibuliwa ndiye atakayepona.

Yesu naye alitembelea birika hilo palipojaa wagonjwa wengi. Akamwona mtu aliyepoozwa tangu miaka thelathini na nane, mwenye uchungu na maumivu. Pamoja na hayo alikuwa na chuki kwa wengine. Kwenye jumba hilo la huruma kila mmoja alijishughulikia mwenyewe tu. Hakuna wa kumhurumia yeye. Hata hivyo hajatupa tumaini, akingojea nafasi, ingawa haba sana, ili naye apokee rehema tukufu. Mara huruma mwenye mwili alisimama mbele yake, naye Yesu alianzia tiba lake kwa kumvuta mtu huyu badala ya kuangalia yale maji, amtazame yeye. Ndipo akachokoza mawazo ya yule mpoozwa atamani kupona. Yesu alimpatia nafasi ya kutamka uchungu wake akilia: “Hakuna anayenijali! Mara ngapi nalijaribu nipate kupona, lakini tegemeo langu limefifia. Hakuna aulizaye habari zangu. Labda wewe utasubiri hapo pangu ili maji yatibuliwe, ukanisaidia kunitia majini?”

Hakuna anayenijali! Je, hii ndiyo hali yako, ndugu yangu? Wengine wanakukatalia? Twakuambia kwamba, Yesu asimama mbele yako. Anakuulizia na amekupata. Hayo yalikuwa ni mambo aliyoyasikia yule aliyepoozwa. Mtazamo wake wenye maswali ulikutana na macho ya Kristo; na huruma yake ilikuza ndani ya huyu mtu tumaini juu ya huyu Bwana wa upendo.

Yesu alipoona hamu kubwa ya huyu mtu mwenye bahati mbaya, kwamba anatamani sana kuponywa, pamoja na tumaini lake, kwamba Yesu anayo uwezo wa kumfungua , akaagiza: “Inuka, jitwishe godoro lako na uende!”. Hili lilikuwa agizo tukufu, likifanya jambo lisilowezekana litendeke. Huyu mpoozwa aliamini neno la Kristo, akitegemea nguvu iliyomiminwa toka kwake.Alisikia mwamko uliomiminika ndani ya mifupa yake na nguvu iliyohuisha mwili wake. Akapokea nguvu hata akapona.

Mara moja akaruka kwa furaha, akasimama kabisa akiinua godoro lake juu ya kichwa chake na kuibeba kwa shangwe. Imani yake iliheshimu neno la nguvu la Kristo, na hivyo kumpatia mara moja kuwa mzima.

SALA: Bwana Yesu, tunakushukuru kwamba, hukumpita huyu mtu ambaye hakujiweza, lakini ulimwangalia kwa huruma zako. Hakuwa na mtu yeyote ila wewe tu mwenye huruma. Tusaidie tushikamane na wewe mwenye enzi, wala tusitegemee msaada wa mwanadamu. Utugeuze tufanane na mfano wa upendo wako, tuweze kuwahurumia wengine, tukishiriki baraka zako nao.

SWALI:

  1. Jinsi gani Yesu alimponya yule mwenye kupooza kwenye birika la Bethzatha?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 31, 2013, at 09:57 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)