Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 010 (The fullness of God in Christ)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
A - Neno la Mungu kufanyika mwili ndani ya Yesu (Yohana 1:1-18)

3. Ukamilifu wa Mungu ulitokea katika kuzaliwa kwa Kristo mwilini (Yohana 1:14-18)


YOHANA 1:17-18
17 „Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa. Neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Kristo Yesu. 18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote. Mungu Mwana wa pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.“

Tofauti ya Agano la Kale na Agano Jipya inaweza kujumlishwa kuwa tofauti kati ya kujaliwa haki kwa sheria au kujaliwa haki kwa neema. Mungu alimpa Musa amri kumi. Tena sheria ya sadaka ya damu na sheria ambazo zinaagiza taratibu safi kwa watu kuishi pamoja. Aliyeshika maagizo hayo aliona raha maishani. Lakini aliyekaidi moja ya hayo maagizo, alistahili kifo. Kwa njia hiyo sheria ilipata kuwa hukumu ya kifo, kwa sababu hakuna mwanadamu asiye na makosa. Hata wenye maisha bora ya utawa wakawa wanavunjika katika toba na majuto, wakitambua ukweli wa kutokuweza kutimiza maagizo yote ya sheria. Watu wa juujuu basi, walijihesabu kuwa wema, kana kwamba maisha yao yalimpendeza Mungu. Hali hii iliwapeleka katika maisha ya kujipendeza wenyewe na kujishughulisha sana taratibu za sheria. Walisahau upendo na kuringa kwa kujihesabu wenye haki ndani ya kazi zao za ubinafsi. Kweli kabisa, sheria yenyewe ni takatifu, kwa sababu inaonyesha utakatifu wa Mungu. Lakini mbele ya sheria kila mwanadamu anaonekana kuwa mwovu. Kwa njia hii sheria inatupeleka katika huzuni na kifo.

Katika mazingira haya ambayo inayonuka harufu ya kifo mwinjilisti Yohana anamtaja Yesu Kristo kwa mara ya kwanza katika injili yake, kwamba yeye ni Mkombozi kutoka kwa ghadhabu ya Mungu. Mwanaume Yesu kutoka Nazareti ndiye Masihi aliyewekwa wakfu kwa ukamilifu wa Roho Mtakatifu. Yeye ni mfalme wa wafalme, tena ni Neno la Mungu na Kuhani Mkuu. Yeye ndiye jumla ya yote yale yanayohitajika kwa tumaini na wokovu wetu.

Kristo hakuja kwetu akiwa na taratibu ya sheria mpya, lakini alitukomboa kutoka kwa laana ya sheria. Akiwa na upendo usio na kipimo, yeye alitimiza madai yote ya sheria kwa niaba yetu. Alitwishwa dhambi zetu na hukumu za ulimwengu wote begani mwake pale msalabani, na hivyo kutupatanisha na Mungu. Kuanzia hapo, Mungu si adui yetu tena, kwa sababu ya dhambi zetu, lakini tumepata amani na Mungu kupitia kwa Yesu Kristo, Bwana wetu. Huyu Mwana wa Adamu Yesu alipaa juu mbinguni kwa baba yake na kutumwagia Roho Mtakatifu wake kwetu. Alitia mioyoni mwetu sheria zake, kwa kujaza utu wetu wa ndani na tabia na mawazo safi, ya kweli na ya heshima. Hatuishi tena chini ya sheria, badala yake yeye anakaa ndani yetu. Kwa njia hiyo Mungu alitupatia uwezo wa kutimiza madai ya sheria ya upendo wake.

Katika kuja kwake Kristo duniani, utawala wa neema umeanza, nasi tunaishi ndani yake. Mungu hadai kwetu tena sadaka za wanyama, huduma au matoleo ya kuimarisha haki yetu wenyewe, lakini alituma Mwana wa pekee atujalie haki tukufu wa ajabu.Yule anayeamini ndani yake ametakasika kabisa. Kwa sababu ya haya tunampenda na kumshukuru na kumtolea sadaka iliyo hai kwa mwenendo wetu, kwa sababu yeye ametutakasa.

Kristo hakutuacha kama yatima, lakini anaendelea kukaa kati yetu na kumwagia vipawa vyake ndani yetu.Hatustahili msamaha wa dhambi zetu au ushirika wa Roho wa Mungu. Wala hatustahili kipawa chochote kingine au baraka toka kwake. Kila kitu ni neema tu kutoka kwake. Kwa kweli, hatustahili lingine ila hasira ya Mungu na kupotea milele. Lakini kwa hali yetu ya kufungwa kwetu na Kristo kwa imani, tumefanyika wana wa Mungu ambaye kwake ameweka neema yake kuu. Umepata kutambua tofauti kati ya kuwa mtumwa wa dhambi au mtoto wa neema?

Neema hii si jambo la kujisikia tu moyoni. Zaidi ya hii ni kuongozwa na upendo ulio na msingi ndani ya haki adilifu. Mungu hawezi kumsamehe yeyote yule anayetaka hivi hivi, kwa sababu makosa ya mwenye dhambi inadai kifo papo hapo. Ila, kusulubishwa kwa Kristo badala yetu imetimiza madai yote ya haki ya sheria. Hivyo neema ikaonekana kuwa haki kwa ajili yetu, na rehema ya Mungu kuwa ni ukweli usioweza kutikiswa. Neema ndani ya Kristo ndiyo msingi wa haki kwa maisha yetu na Mungu.

Unauliza: Mungu huyu ni nani, aliye huru kabisa kufanya aonavyo, na hata hivyo hutenda nje ya unyofu wa haki yake? Tunakujibu: Dini nyingi zimejaribu kwa bidii sana kumwelewa Mungu hadi kuchoka. Lakini yote inafanana na ngazi iliyosimamishwa hapa ardhini ambayo haifiki mbinguni. Ila Kristo ni kama ngazi tukufu ambayo inashuka toka mbinguni na kufikia ardhini.Kukutana kwetu na Mungu kupitia kwa Kristo kama ngazi, haimwachi hata mmoja wetu akate tamaa.

Hakuna mtu aliyemwona mwumbaji wa milele, kwa sababu dhambi zetu zimetutenga na yule aliye Mtakatifu. Maelezo yote kumhusu Mungu sio zaidi ya mawazo ya kuhisi na ya mashaka tu. Lakini Kristo ni Mwana wake, akiishi na Mungu tangu milele. Hii ni tamko moja kuhusu Utatu tukufu. Kwa hiyo ni dhahiri kwamba, Mwana ajua yote ya Baba. Mafunuo yote kabla ya hapo ni ya upungufu. Lakini Kristo ndiye Neno la Mungu kamili, tena ni jumla ya ukweli wote.

Ni nini kiini cha ujumbe wa Kristo?

Alitufunza kumwelekea Mungu namna hii kwa sala: „Baba yetu uliye mbinguni“. Kwa namna ya tamko hilo kumwomba Mungu anatutangazia kwamba, kiini cha Mungu ndiyo Ubaba wake. Mungu sio mkatili, mpiganaji au mwenye kuharibu. Wala yeye sio mtepetevu wala mwenye kubadilika-kubadilika. Anatutunza sote kama vile baba anavyomjali mtoto wake. Ikiwa huyu mtoto anaanguka matopeni, anamwinua, anamwosha wala hamwachi apotee katika dunia ya maovu. Kwa sababu tumepata kujua Mungu kuwa ndiye Baba yetu, mashumbufu yanayoletwa na mahangaiko na dhambi zetu yamefutwa. Kwa kurudi kwa Baba yetu tulipata kuoshwa na kukaribishwa kwake. Tukae na Mungu milele. Mapinduzi ya dini ambayo yamechipuka duniani kwetu katika jina „Baba“ ndiyo wazo kuu mpya ya kikristo aliyeleta Kristo mwenyewe. Jina hilo la ubaba linajumlisha mafundisho na kazi zote za Kristo.

Kabla ya kuzaliwa kwake mwilini Kristo alikaa pamoja na Baba. Picha hii ya kupendeza inadhihirisha uhusiano wa upendo ulioko kati ya Kristo na Mungu. Baada ya kufa na kufufuka kwake Mwana alirudi kwa Baba. Hakukaa tu upande wa kulia kwa mkono wa Mungu, lakini pia amekaa kwenye kifua cha Baba. Hii ina maana kwamba, kuwa mmoja naye, yeye ni yeye. Kwa hiyo yote asemayo Kristo kuhusu Mungu ni kweli tupu. Katika Kristo tunamwona Mungu alivyo. Kama vile Mwana alivyo ndivyo Baba alivyo, na vile Baba alivyo ndivyo na Mwana alivyo.

SALA: Baba yetu uliye mbinguni tunakuinua na kukushukuru, kwa sababu ulimtuma Kristo kwetu, Mwana mpendwa wako. Tunainama chini mbele zako kwa vile ulituweka huru kutokana na ndoto za sheria, na kutupanda ndani ya haki yako tukufu. Tunakushukuru kwa kila kipawa cha kiroho na kukutukuza kwa sababu ya uhuru uliotupatia kwa njia ya jina lako la ubaba.

SWALI:

  1. Ni fikira gani mpya aliyoleta Kristo kwetu duniani ?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 24, 2013, at 07:52 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)