Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 006 (The Baptist prepares the way of Christ)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
A - Neno la Mungu kufanyika mwili ndani ya Yesu (Yohana 1:1-18)

2. Mbatizaji anatengeneza njia ya Kristo (Yohana 1:6-13)


YOHANA 1:9-10
9 „Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu. 10 Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.“

Kristo ndiye nuru ya ukweli ulimwenguni. Roho Mtakatifu aliwajulisha manabii kuja kwake mamia ya miaka kabla ya tukio hilo. Vitabu vya Agano la Kale yanajaa maneno ya kukariri unabii kuhusu kuja kwake Kristo ulimwenguni. Hivyo nabii Isaya akasema „Tazama, giza kuu itafunika dunia na dhiki itawaangukia watu, bali Bwana atakuzukia wewe, na utukufu wake utaonekana juu yako“ (Isaya 60:2). Katika kifungu chetu cha Yohana 1, neno „dunia“ imerudiwa mara nne. Kwake mwinjilisti Yohana neno hili lina maana karibu sawa na maana ya „giza“, kwa hiyo ameandika, „dunia yote imewekwa chini ya mamlaka ya yule muovu“. (1.Yohana 5:19b)

Hapo mwanzo dunia haikuwa na uovu, maana Mungu aliiumba safi na kamili. Urembo wake na uzuri wake ulijaza ulimwengu. „Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana“. (Mwanzo 1:31) Mungu alimwumba na mwanadamu kwa mfano wake na utukufu wake, wakapewa wazazi wa wanadamu wote ambao wanadhihirisha nuru ya Mwumbaji kama kioo.

Lakini kwa sababu ya majivuno, wote wakawa wabaya na waasi. Waliacha ushirikiano na Mungu katika mioyo yao, kwa sababu walijifungua kwa roho ya giza. Wakajiweka mbali na Mungu na hilo wakawafanya kuwa waovu zaidi. Ndivyo Daudi alivyokiri katika Zaburi 14:1 “Mjinga anasema moyoni: Hakuna Mungu, - wameharibu matendo yao na kufanya chukizo, hakuna mmoja atendaye mema hata mmoja“.

Mwinjilisti Yohana alishuhudia ukeli kwamba Kristo alikuja katika ulimwengu huu mbaya kama vile jua linavyopaa kila kukicha na kuondoa giza mbele zake. Nuru ya Kristo haikuingia katika dunia kama vile mwangaza wa radi inapopiga. Lakini aliingia polepole akiwangazia watu wote. Kwa hivyo hakuingia kama hakimu au mtimizaji wa hukumu. Bali alikuja kuwa mwokozi na mfariji. Watu wote wanahitaji kuangaziwa na Kristo. Pasipo mwangaza wake watadumu gizani. Kristo ndiye mwangazaji wa kweli, wala hakuna mwingine. Yeyote anayekubali kumulikiwa hivyo kupitia injili, atabadilishwa tabia yake na kuwa mwema na atawaangaza na watu wengine.

Je, unaelewa maana ya msemo huu: „Mwumbaji aliingia duniani“? Mwenyewe, au Mmilikaji aliingia mahali pake na mfalme aliwakaribia watu wake aliyewaumba. Ni nani atakayeinuka na kuandaa kuja kwake? Ni nani atakayejifunza ukweli kuhusu kuja kwake, katiba yake, na malengo yake? Ni nani yule atakayeacha dunia na malengo ya bure, atakayekaribia na kumkaribisha Mungu ajaye ? Ni nani atakayetambua wakati wenyewe wa saa na dakika ya ajabu Mungu atakapokuja kwa upesi katika utukufu wake?

Hivyo, Bwana alionekana katikati ya wenye dhambi. Alikuja bila kutambulikana kwa sababu ya udogo, upole na ukimya aliyoivaa. Hakutaka kuangazia dunia kwa mambo ya ukuu wake, nguvu na utukufu wake, lakini alidhihirisha unyenyekevu, upendo na ukweli. Tangu wakati wa uumbaji kiburi ndio chanzo cha kuanguka kwa mwanadamu. Basi, Mwenyezi alijionyesha mwenye kunyenyekea. Hata shetani alitaka kuonyesha nguvu zake, kuwa mtukufu na mwerevu kama Mungu. Lakini Kristo alitokea kama mtoto mdhaifu, amelala mahali pa aibu horini. Kwa hivyo, kwa unyenyekevu wake, upole wake na utiifu alishinda. Alishuka kabisa, kwenye usawa na mtu wa chini kabisa, ili kuweza kumwinua mtu yeyote na pia kuwaokoa wote.

Sikilizeni, enyi watu wote! Baada ya habari hii njema, tunasoma neno la kuogofya na kuvunja moyo, kwamba dunia haijui nuru wala kuifahamu .Haikutambua ya kwamba Mwana wa Mungu amekaribia na amekuwa kati yao. Watu wamedumu katika hali ya upofu na ujinga, hata ingawa wamesoma sana na kuwa na ujuzi wa mambo mengi, pamoja nao wenye elimu ya juu ya kidunia. Hawakutambua kwamba Mungu mwenyewe amesimama mbele zao. Hawakumjua Mwumba na hawakumkubali Mwokozi wao, naye ndiye atakayewahukumu.

Kutokana na ukweli huu chungu, tunaelezwa msimamo muhimu wa ufalme wa Mungu. Ni kwamba, hatuwezi kumwelewa Mungu peke yetu kwa akili zetu na uwezo wa kibinanadamu. Hekima zote kuhusu upendo wa Kristo ni neema tupu na zawadi kutoka kwa Mungu. Kwa sababu ni Roho Mtakatifu anayetuita kupitia kwa injili. Yeye anatuangazia kwa vipawa vyake na kututunza katika imani ya kweli. Kwa hiyo ni lazima kutubu wala si kutegemea akili zetu au makusudio ya roho zetu. Sisi sote twahitaji kujiweka wazi tukielekea kwenye nuru ya kweli, kama vile maua yanavyojifungua kuelekea mwangaza wa jua. Kwa njia hii, imani ndani ya Kristo inatutengenezea hekima ya kweli. Mwanzo wa imani hii haitoki ndani yetu, lakini ni kazi ya Roho wa Mungu ndani ya wote wanaokubali kumtii.

SALA: Tunakushukuru, ewe Bwana Kristo, kwamba ulikuja katika dunia hii. Hukuja kwa kuhukumu au kulipiza kisasi, lakini ili kuangaza watu wote na kwa wokovu wao. Lakini sisi tmekuwa vipofu na wajinga. Utusamehe makosa yetu na utupe moyo wa utii. Tufungulie macho yetu, ili tuweze kukuona, na utufungue roho zetu kwa mwangaza wa nuru yako ya upole, ili tuweze kuishi kwa nguvu ya Roho wako Mtakatifu.

SWALI:

  1. Kuna ushirikiano gani kati ya nuru ya Kristo na ulimwengu wa giza?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 24, 2013, at 07:51 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)