Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 005 (The Baptist prepares the way of Christ)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
A - Neno la Mungu kufanyika mwili ndani ya Yesu (Yohana 1:1-18)

2. Mbatizaji anatengeneza njia ya Kristo (Yohana 1:6-13)


YOHANA 1:6-8
6 „ Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake aliitwa Johana. 7 Huyu alikuja kwa ushuhuda, ili ashuhudie ile nuru, watu wapate kuamini kwa yeye. 8 Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru.“

Mungu alimtuma Johana mbatizaji ndani ya ulimwengu wa giza, ili kuwaita watu waingie katika miali ya nuru tukufu. Kila mmoja anajua kwamba dhambi nyingi zinafanyika gizani. Lakini yeyote anayekiri makosa yake mbele za Mungu, kwa kuungama dhambi kwa moyo uliovunjika, atakuwa amekuja nuruni. Je, wewe umeamua nini kwako? Umekuja kwenye nuru ama unaendelea kujificha gizani?

Mbatizaji alieleza juu ya hali ya roho za watu.Kwa kufuatana na sheria za Mungu, wote ni wabaya. Wanahitaji kutubu na wafanye mabadiliko ya msingi maishani mwao, ili wasipate kuangamia siku ya Bwana. Wito wa Mbatizaji ilitikisa mati ya watu, wakimkimbilia yule aliyewaita watubu kule jangwani. Waliungama dhambi zao kwa uwazi wakitamani kubatizwa katika mto wa Jordani kama ishara ya kusafishwa kwa dhambi. Kuzamishwa majini ubinafsi wao kuliwafikisha kwenye maisha mapya kwa kupitia maji ya mto ule.

Mungu alimchagua Yohana Mbatizaji kwa kazi muhimu. Alimmulikia na kumtuma ili kuwavuta watu wote, ili wapate ufahamu, wabadilishe mawazo yao na wapate kujitajarisha kwa kuja kwake Kristo. Watu wa Agano la Kale walijua mengi kuhusu yule Mmoja atakayekuja kwa jina la Bwana. Nabii Isaya alisema juu yake: „Watu wale waliotembea katika giza wameona nuru kuu. Wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti, kwao nuru imewaangaza (Isaya 9:2). Pia alisema kwa Jina la Kristo: „Amka uangaze, kwa sababu nuru yako imekuja. Na utukufu wa Bwana umekuzukia.“ (Isaya 60:1) Mbatizaji alifundisha kwamba kuingia kwa nuru ndani ya giza, si kwa ajili ya watu wa Torati tu, lakini imefunguliwa kwa watu wote. Kwa hivyo ujumbe wa mbatizaji uliwamaanisha watu wote duniani, ili watu kutoka Asia Ndogo na maeneo yote yanayozunguka bahari ya kati walikuwa wanamfuata kwa miaka mingi, hata baada ya kifo chake.

Maelfu walimfuata Yohana ingawaje alishuhudia kwamba yeye siyo ile nuru, lakini ni mjumbe aliyetumwa mbele yake. Hakuwavuta watu kwake binafsi, bali aliwaelekeza kwake Kristo. Hii ndio dhihirisho ya wazi kwa wajumbe wa kweli wa Mungu hata siku hizi kwamba, hawafunganishi wafuasi wao kwa nafsi zao, bali wanawaelekeza kwa Kristo tu.

Lengo la huduma ya Yohana haikuwa ungamo na ubatizo, bali watu wawe na imani ndani ya Kristo. Alijua kwamba, watu kadhaa walitegemea kwamba, atajitangaza siku moja kuwa yeye ndiye Kristo anayekuja. Lakini hakuingia katika mtego huo, bali aliendelea kutengeneza njia ya Bwana. Alifahamu kwamba Kristo ajaye ndiye atakayewabatiza watu kwa Roho Mtakatifu. Yohana pia alijua kwamba, kutubu katika mawazo ya mwanadamu haitoshi hata kidogo, ingawa anabatizwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Lakini alijua kwamba, sote tunahitaji kubadilishwa upya katika utu wa ndani. Mungu hakumpa mamlaka ya kubadilisha mioyo ya watu, kama vile hakumpa nabii yeyote katika Agano la Kale uwezo huo. Jukumu hii inahifadhiwa kwa Nuru yenyewe ambayo inaumba, tena ni Neno liletalo uhai. Hii ndiyo inaweza kubadilisha mtu kwa mamlaka yake wakati wanapoamini katika Jina lake Yesu na kufungua maisha yao kwa nuru yake. Kwa njia hii Yohana aliwaongoza umati wa watu kumwamini Kristo. Alijua kwamba imani pekee itawawezesha kuingia ndani ya utawala wake mpya.

Apollo naye alikuwa mtu msomi mwenye uchangamfu, aliyefuata mafunzo ya Yohana Mbatizaji. Baadaye alimhubiri Kristo na kufanikiwa, lakini bila kutambua Nuru mpya ya Agano Jipya. Bali alipopata kukutana nayo, alijipeleka mwenyewe kwake Kristo. Nuru ikaingia ndani ya roho yake, akawa nuru katika Bwana na alama kubwa ya kung’aa gizani. Yeye aliwafundisha wengi na kuwaeelekeza kwenye nuru ya kweli. (Matendo 18: 24-28)

SALA: Ee Kristo Yesu, tunakuinua na kukushukuru kwa sababu wewe ndiwe nuru ya ulimwengu na tumaini ya waliovunjika moyo. Ulileta nuru ya ufahamu katika giza la mioyo yetu, ulifunua dhambi zetu na kutusamehe. Tunakushukuru kwa sababu ulitufanya tuwe watoto wa nuru na kutuweka huru kwa uzima wa milele. Tunakuomba miali ya nuru yako iwafikie na marafiki zetu na jamaa zetu, ili wao nao wakutambue na wapate msamaha wa kweli, na kwa imani nuru yako ipate kuingia na kwao.

SWALI:

  1. Ni yapi malengo makuu katika huduma ya Yohana Mbatizaji?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 24, 2013, at 07:51 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)