Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 004 (The word before incarnation)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
A - Neno la Mungu kufanyika mwili ndani ya Yesu (Yohana 1:1-18)

1. Asili na kazi ya Neno kabla ya kufanyika mwili (Yohana 1:1-5)


YOHANA 1:5
5 “Nayo nuru inaangaza gizani lakini giza halikuiweza.”

Chochote ambacho kinakaa na Mungu kimejaa nuru na hakina lawama. Kinakaa wazi na kuwa na umaridadi. Katika maeneo ya utawala wake hakuna cha giza. Kila jambo ni wazi, wima, kweli na takatifu. Uchafu hauna nafasi katika uwanja wa ukaribu naye. Roho Mtakatifu ni usafi kabisa na nuru ya Bwana haiangazi kwa ukali, bali katika upole. Inatufariji na kutuponya.

Miali ya nuru ya Kristo haiko kwa ajili ya mbinguni.Inachomoza gizani na kuleta ukombozi. Ni neema ya ajabu kwamba, hata siku hizi Kristo anaangaza katikati ya giza yoyote. Hawezi kuwadharau au kusahau waliopotea, bali anawaweka huru na kuwaangazia maisha yao.

Tunatakiwa kutambua uwepo wa ulimwengu wa giza unaotenda kazi dhidi ya ulimwengu wa nuru. Hatujui kwa undani jinsi gani giza ilivyopata kutokea. Mwinjilisti Yohana hakutueleza siri hii. Alitutaka tujue habari ya nuru, wala hakutaka tuchungulie sana ndani ya giza. Wanadamu wote na viumbe walianguka ndani ya giza na ulimwengu wote ukatiwa chini ya ushawishi wa mwovu. Labda unaweza ukajiuliza: Ikiwa Kristo aliumba ulimwengu kwa ushirikiano kamili na Mungu na kuwa kitu kizuri na chema, ni vipi giza liliweza kuingia ndani yake? Mungu alimwumba mwanadamu kwa mfano wake, na vipi sasa mbona tulipata kupungukiwa na utukufu wake siku hizi?

Yohana hakumtaja shetani kwa jina, na kwamba shetani alimwasi Mungu na kutaka kuzimisha nuru yake.Yeye kila wakati alikuwa akimpinga Kristo. Kwa sababu hivyo alipoteza nuru aliopewa. Shetani alijawa na kiburi na kutafuta ukubwa bila idhini ya Mungu. Alkusudia kujiinua juu ya Mungu na kumweza. Ndio hapo alipotupwa na Mungu na kufanyika mkuu wa giza.

Na sasa ndugu, lengo la maisha yako ni nini? Unatafuta ukubwa, kujulikana na unyakuzi wa mali bila Mungu? Na kama ndiyo hivyo kwako, wewe basi ni wa lile kundi ambalo linakaa gizani kama yule mwovu mwenyewe. Kwa vile hakukaa peke yake, alifaulu kuwavuta mamilioni ya watu katika giza yake. Angalia nyuso za watu wanaopita barabarani.Unasoma nuru au giza katika macho yao? Roho zao zinadhihirisha furaha ya Mungu ama huzuni ya shetani ?

Yule muovu anamchukia Mungu kwa sababu nuru yake takatifu inamhukumu. Hataki ile nuru ifunue ukali wake. Kila wakati anajificha na kujifunika, na hivyo anajaribu kumshinda Kristo pamoja nao wanaofuata nuru yake. Huyu mdanganyifu hawezi kuvumilia nuru ya Mungu, lakini anaichukia. Anafunika uso wake kwa kusudi, na hivyo hawezi kutambua hiyo nuru. Linalotisha ni kwamba mamilioni ya watu hawaoni jua lake Kristo likiangaza ndani ya usiku wa dhambi zao. Tunaelewa jua na uwezo wake. Haihitaji kuelezwa. Jua liko kila kukicha na inang’aa, inaangaza wazi, linamulika kotekote. Hata mtoto mdogo anafahamu kwamba jua ndio chanzo cha uhai.

Lakini wingi wa watu hawatambui utukufu wa Kristo na nguvu zake inayozidi sana nguvu ya jua, kwa sababu hawataki kuitambua. Mafundisho ya udanganyifu ndio yanafunika macho yao kama blanketi zito na hivyo kukataa ujumbe wa kweli kuhusu uungu tukufu ya Kristo. Ukweli ni kwamba, hawataki kugunduliwa makosa yao, dhambi zao. Hawakubali kuelekea kwenye nuru na badala yake kuona bora kuendelea gizani. Wanafunika macho yao kwa kutokutambua hali zao na hivyo kukataa kutubu dhambi zao. Hali hii inawafanya kuringa na kuwa wenye kiburi. Wanaendelea wakiwa vipofu kuhusu rehema ya nuru ya Kristo. Kwao giza inashindana na Nuru, lakini Nuru inaweza kuishinda kwa upendo. Kwa hivyo wewe ni nani? Unaishi nuruni itokayo kwa Bwana au gizani itokayo kwa yule mwovu ?

SALA: „Ee Bwana, wewe ndiwe nuru ya ulimwengu. Tunakufuata kwa imani na katika upendo wako. Hatuendi gizani, bali tumepokea nuru ya uhai wako. Tunakushukuru kwa sababu hukutuacha katika upweke wetu, tukiogopa giza ya hasira ya Mungu. Asante kutuita tuingie ndani ya nuru yako ya kung’aa. Tunakusihi Mungu, uwamulikie mamillioni ya watu wanaotuzunguka ambao bado hawakutambui, iwapo nuru yako inamulikia kote. Tuonee huruma na kutuangaza kwa nuru yako, ewe Mmulikaji!“

SWALI:

  1. Kuna utofauti gani kati ya nuru na giza katika maana ya kiroho ya maneno haya?

„Watu ambao walitembea gizani wameona nuru ya ajabu; wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti nuru imewaangaza.“
(Isaya 9:2 )

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 24, 2013, at 07:51 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)