Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 104 (Jesus intercedes for the church's unity)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 3 - Nuru yang’aa ndani ya shirika la Mitume (Yohana 11:55 - 17:26)
E - Maombezi ya Yesu (Yohana 17:1-26)

4. Yesu anaombea umoja wa kanisa (Yohana 17:20-26)


YOHANA 17:20-21
„Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.“

Kristo aliwawekea wanafunzi wake msingi ndani ya upendo wa Mungu na ndani ya nguvu ya Roho, akimwuliza Babaye, awakinge na yule Mwovu, na kuwatakasa kwa njia ya Injili kabla hajakabidhiwa asulibiwe. Baada ya kupata uhakika kwamba sala kwa ajili ya mitume wake na Kanisa itakuwa inajibiwa, alitazama mbele kwa siku zitakazokuja, akaona majeshi ya waumini wakitokana na ujumbe wa Mitume wake. Sura ya Mshindi aliyesulibiwa na hivyo kumshinda Shetani na dhambi iliwavuta ndani ya kanisa hao wote. Kwa njia ya tumaini lao ndani ya Kristo aliye hai, yule Roho alishuka ndani ya mioyo yao, ili washirikiane katika neema ya uhai tukufu. Kwa imani walikuwa wameunganika na Baba na Mwana katika umoja wa milele.

Kristo aliomba kwa ajili ya waumini wale, ambao watapata kuamini kwa ajili ya Mitume. Tunashangaa kwamba, alipoomba hao walikuwa bado hawajapatikana. Maneno yake ya sala yanathibitisha kwamba kimsingi kabisa ujumbe wa mitume ilikuwa inastahili kuaminika. Basi, nini ni kiini cha haja yake kwa ajili yetu? Je, aliomba kwa ajili ya afya zetu? Au kwa usitwi au kufanikiwa kwetu? Hapana! Alimwomba Babaye atujalie unyenyekevu na upendo, ili tuwe na umoja na Wakristo wote wa kweli. Tusije tukapata wazo kwamba tu bora kuliko wengine, au kusikia kwamba tabia ya hao wengine hatuwezi kuvumilia.

Umoja wa waumini ndiyo shabaha ya Kristo; Kanisa lililogawanyika ni kinyume cha mpango wake kwa ajili yake. Hata hivyo, umoja huo unaodaiwa na Kristo hauwezi kujengwa na mipango na taratibu za kikanisa, lakini unafungamana na sala za kiroho juu ya mambo mengine yote. Jinsi Mungu kwa asili alivyo mmoja, hivyo Kristo alimsihi sana Babaye, aunganishe waumini wote ndani ya ushirikiano huo wa Roho wake Mtakatifu, ili wote wawe salama ndani yake. Na pia Kristo hakuomba, „wawe na umoja na mimi au wewe“ lakini „ndani yetu“! Hivyo basi anaonyesha kwamba umoja huo kamili inakamilika ndani ya Baba na Mwana ndani ya Roho; hii ndiyo sura yake. Anatamani kukuinua kwenye usawa na yeye, maana nje ya ushirikiano wa Utatu hakuna lolote ila kuzimu tu.

Shabaha ya kuimarishwa ndani ya umoja wa Mungu si kwa ajili ya kujifurahisha sisi wenyewe kiroho, lakini itupatie nguvu ya kushuhudia mbele za wengine, wanaoishi mbali na Mungu hata sasa. Tungetumaini kwamba, wao nao watatambua kwamba wamekufa ndani ya dhambi na waovu katika kiburi chao, pia na wafungwa wa tamaa zao, na hivyo na wao wapate kutubu na kumgeukia Mwokozi. – Wewe unayeshikamana na Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, utajaliwa nguvu uwe mnyenyekevu wa kutosha, mwenye kupenda, katika uhuru wa kiroho kumpenda yeyote apataye kuamini, na kufurahia katika kuwepo kwao, na hivyo pamoja nao kupata kuwa ushuhuda wa thamani wa upendo wa Kristo. - Sisi sote tumehakikisha kabisa kwamba huyu mwanadamu Yesu ni Mungu. Heri Wakristo wote wangekuwa na ukweli hasa, hakuna ambaye angesalia ulimwenguni asiye Mkristo. Upendo na amani yao zingewavuta wote na kuwabadilisha. Basi tufanye bidii sana kwa haja ya Yesu kuwa na umoja! Je, unakusudia kuwa sababu kwa watu ya kutokuamini ndani ya Kanisa lililogawanyika, kana kwamba mwili wa Kristo inakuwa na vipande vipande?

YOHANA 17:22-23
„Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.“

Nini ni utukufu wa Yesu? Je, ni kule kung’aa kwake au nuru ya enzi yake? Hapana! Utukufu wake umefichwa nyuma ya unyenyekevu wake, subira na uvumilivu wake. Kila usafi wa kiroho ni kama mshale wa nuru ya utukufu wake. Basi Yohana aliona na kushuhudia, „tumeuona utukufu wake“. Hayo hakukariri kwa wakati ule Yesu alipogeuka sura wala si kwa ufufuo wake tu, lakini pia kwa ile hori ya kawaida alimozaliwa na msalaba wake jeuri. Katika hayo utukufu wa upendo safi uliweza kuonekana wazi kabisa; ambapo Mwana alijimwaga kwa kuondoa utukufu wake wa awali na kuonyesha wazi kiini cha enzi yake akiwa katika hali ya mwanadamu. Utukufu uo huo Yesu ametujalia na sisi. Roho wa Baba na Mwana alishuka juu yetu.

Kusudi la hiyo heshima tuliopatiwa haina maana ya kuringa au kujitangaza sisi wenyewe, lakini tupate kujitoa katika umoja kwa ajili ya huduma, na kukutana kwa ajili ya kushirikiana sisi kwa sisi, na tuelekee kwa shabaha ya kuwaheshimu wengine. Pamoja na shabaha hizo za kiroho Yesu alimwuliza Babaye kwa ajili ya umoja uo huo na ushirikiano ulio sifa ya Utatu Utakatifu, kutumiminia na tabia hizo. Upendo wa Mungu ndiyo kipimo cha kujaribu Kanisa. Ni yeye tu anayetutengeneza tuwe katika sura yake ya milele.

Kweli kabisa, Mungu katika ukamilifu wake huishi ndani ya Kanisa lake. (Efeso 1:23; Kol 2:9) Au unapungukiwa ushujaa wa kutamka maneno yaliyomo katika kifungu kile cha maandiko, „Ndani ya Kristo huishi ukamilifu wa uungu kimwili, nasi tumo kamili ndani yake.“ Ushuhuda huo wa kitume ndiyo thibitisho kwamba, maombezi ya Yesu kabla ya kufa kwake yamejibiwa. Tunamwabudu na kumtukuza Bwana, kwa sababu hatatudharau sisi ingawa tuliharibika na tu wenye hatia tena na tena; lakini alitusafisha na kututakasa, na kujiunga nasi, ili na sisi tuishi maisha yake matukufu.

Yesu alikuwa anategemea kabisa kwamba, sisi tutaweza kukamilika katika upendo na unyenyekevu. Basi na tupendane na kuheshimiana sisi kwa sisi! Sio kukamilika katika ustawi, uwezo au hekima, bali rehema na upendo na upole ndiyo sifa anazotamani kuziona ndani yetu. Huruma na kuchukuliana ilikuwa ni shabaha yake ya kwanza aliposema, „Mwe wakamilifu jinsi Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu“. Agizo hilo linajumlisha makusudi yake ya kupenda hata maadui. Lakini katika sala yake ya maombezi alikusudia hatua nyingine ya juu zaidi katika kukamilika: alitamani umoja wa kiroho ndani ya Kanisa na pamoja na Mungu. Roho hatatuongoza kwenye hali ya kujiangalia kwa ndani au kujitenga na watu, bali kwenye ushirikiano na watakatifu. Umoja ulivyo ndani ya Utatu ndiyo mfano wetu. Hatutamshuhudia Mungu vizuri ulimwenguni, tusipokuwa na umoja. Jinsi watu wapekee walivyoonyesha sura ya Mungu katika Agano la Kale, zaidi sana Kanisa pamoja na washiriki wake tungeonyesha wazi sura ya Utatu Utakatifu, ambayo ni umoja.

Hali ya upatano ndani ya Kanisa inawaingia watu wa dunia, ili waone kwamba tunatoka kwa Mungu. Wataanza kutambua kwamba Mungu ni pendo. Sio maneno matupu au maelezo marefu sana yanayoumba imani ndani yao. Bali ni furaha katika mkusanyiko wa watoto wa Mungu yanayosema zaidi na kwa hali bora kuliko mahubiri marefu. Basi, hivyo Roho Mtakatifu aliwaunganisha wale wa Kanisa la kwanza Yerusalemu katika hali halisi ya umoja wa kiroho.

SALA: Asante sana, Bwana Yesu kwa kutuongoza sisi tusiostahili tuifikie imani ndani yako. Ulitufanya sisi tuwa watumishi wako kwa ushuhuda wa upendo wako. Tunakuabudu, kwa sababu ulitusafisha na kututayarisha tuweze kuwa washiriki wa mwili wako wa kiroho. Utuwekee shina na msingi katika upendo wa Utatu Utakatifu. Tunakutukuza na kukusifu tukikuomba utujalie nguvu tuishi ndani ya makanisa yetu katika umoja wa utendaji ulio na uhai wako.

SWALI:

  1. Jambo gani Yesu alitaka kwa Babaye kwa ajili ya fadhili yetu?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 13, 2015, at 12:02 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)