Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 084 (The new commandment)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 3 - Nuru yang’aa ndani ya shirika la Mitume (Yohana 11:55 - 17:26)
B - Mambo yaliyofuatana na chakula cha Bwana (Ushirika utakatifu) (Yohana 13:1-38)

3. Agizo mpya kwa ajili ya Kanisa (Yohana 13:33-35)


YOHANA 13:33
„Enyi watoto wadogo, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta; na kama vile nilivyowaambia Wayahudi ya kwamba, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja; kadhalika sasa nawaambia ninyi.“

Baada ya Baba alipokuwa ametukuzwa kiroho, Yesu atuongoza kupitia kati ya namna na misingi ya imani yetu. Hayupo tu pamoja nasi kimwili, bali anaishi mbinguni. Kristo aliyefufuka ndiyo jambo la uhakika kabisa kuliko mambo yote duniani. Yeye asiyemfahamu au kumwamini, huyu ni kipofu na anatangatanga, lakini yule amwonaye ndiye atakayeishi na kupokea uzima wa milele.

Yesu aliwajulisha wanafunzi wake kwamba, yeye ataenda mahali ambapo wao hawataweza kumfuata. Hakumaanisha kwamba hawataweza kumfuata wakati wa kushitakiwa mbele ya baraza, wala kwenye kaburi wazi, lakini habari ya kupaa kwake mbinguni. Baba alikuwa amesema, „Ukae kwa mkono wangu wa kulia hadi nifanye adui zako kuwa chini ya nyayo zako.“ Yesu hakupotea tu usoni pa wafuasi wake, lakini aliwajulisha mapema habari ya kifo na kufufuka kwake, sawa na habari ya kupaa kwake mbinguni, ambapo hakuna mwanadamu awezaye kuingia kwa bidii yake mwenyewe. Alitabiri hayo mambo mbele ya Wayahudi, lakini walishindwa kuelewa. Je, wanafunzi wake sasa waliweza kuelewa habari ya saa hiyo ya kusalitiwa? Aliwafanya wawe washiriki katika kumwabudu Baba na Mwana, ili wao wasizame ndani ya masikitiko na ya huzuni ya mbeleni. Je, watategemea uaminifu wake, kwamba hatawaacha? Na ya kwamba uhodari wao wa kawaida hautakosa?

YOHANA 13:34-35
„Amri mpya nawapa, Mpendane: Kama vili nilivyowapenda ninyi, ninyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.“

Yesu aliwelewa kwamba wanafunzi wake hawajamfahamu sana sana, kwa vile Roho alikuwa hajamiminwa juu yao. Bado walikuwa na namna ya upofu bila nguvu ya kutegemea, wala kuwa na msukumo wa kupendana kweli, „maana Mungu ni upendo na akaaye ndani ya upendo, hukaa ndani ya Mungu na Mungu ndani yake“. Utatu Utakatifu ndiyo upendo. Kwa vile upendo kati ya nafsi tatu za Utatu Utakatifu unazaa umoja unaodumu daima, Yesu apenda jambo hilo linalobeba Utatu Utakatifu, nalo lipate kuingia kabisa ndani ya binadamu; na hivyo chemchemi ya utakatifu ipate kuimarika ndani ya wanafunzi wake.

Hivyo basi Yesu aliwasihi wanafunzi wake kuwa na upendo wao kwa wao, ambao ni kiungo cha Kanisa lake. Hakuwapangia mambo kumi wasiotakiwa kutenda, jinsi ilivyokuwa wakati wa Agano la Kale, bali agizo moja tu linalounganisha amri takatifu zote zingine. Upendo ndiyo utimilifu wa sheria (au torati au amri kumi ). Kama vile Musa alivyowapa watu maagizo ya kukataza (usi …..), Kristo anatuchochea tutende mambo ya kupendeza hakika, jinsi mwenyewe alivyowapa mfano. Upendo ndiyo kiini cha uhai wa Kanisa. Mahalo ambapo Kanisa halionyeshi upendo, basi litakoma kuwa kanisa.

Upendo ndiyo siri ya nafsi ya Kristo. Alikuwa na huruma kwa ajili ya kondoo walioenda kutangatanga, jinsi mchungaji mwema alivyofanya, na alimhurumia yule kondoo mmoja aliyepotea kabisa. Aliwavumilia wanafunzi wake kwa subira na upole. Kristo aliweka upendo kuwa ni mkataba wa Ufalme wake. Yeye apendaye hukaa ndani ya rehema ya Yesu, lakini aliye na chuki, basi yuko upande wa Shetani. Upendo huvumilia wala haujivuni. Unasubiri na kutegemea yote mema, hata toka kwa adui, jinsi walivyoeleza mitume yetu tabia hiyo ndani ya barua zao mara kwa mara. Upendo wa Mungu haukosei hata kidogo; ndiyo kiungo cha ukamilifu.

Kwa ajili ya Kanisa hakuna kabisa sadaka nyingine ya kufaa badala ya upendo. Tunapojizoeza kufanya huduma tutafaa kuwa wanafunzi wake. Tunajifunza jinsi Yesu alivyoongoza habari ya upendo wa utendaji. Twaishi chini ya msamaha wake, hivyo twaweza kuwa radhi kwa ajili ya wengine bila kununa. Kama ndani ya shirika la watu wa Mungu hakuna anayetamani ukuu, na kama wote wanafurahi kwa sababu Roho wa Kristo amewaunganisha, basi mbingu inawashukia hapo duniani, na Bwana wetu aliye hai huimarisha Makanisa yanayojaa upendo ndani ya Roho Mtakatifu.

SWALI:

  1. Kwa nini upendo ni dalili la pekee linalowatofautisha Wakristo?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on September 01, 2014, at 04:41 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)